Tuwasaidie wanawake wanaotembeza matunda na watoto mgongoni

Tuwasaidie wanawake wanaotembeza matunda na watoto mgongoni

Tatizo wengi wao kama sio wote ni wale waliokuwa wakishauriwa juu ya mienendo yao walikuwa wana jibu kwa dharau kuwa wasiingiliwe na kupangiwa maisha.
Na wengine walisha fuatwa na wanaume sahihi na wenye nia thabiti ya kuanzisha nao familia waka wakataa tena kwa nyodo badala yake wakaenda kudete na waume za watu na vijana wachoma CD na vijana wanyoa viduku.

Acha walipie upumbavu wao walio ufanya labda wanaweza kuwa mfano mzuri kwa hao watoto wao na mabinti ambao bado ni wadogo.
Kutoa ni moyo tuendelee kuwaunga mkono kwenye hizo biashara zao za kujishikiza inawezekana Kuna wakati wanalala njaa matajiri wote duniani kote wanatoa kwa wawahitaji bila kujali nani anaenda kuzitumia
 
Nyie ndiyo mnafanya watu waamini watoto huja na baraka.

Una maisha magumu unazaa ili iweje sasa?Njia zote hizo za uzazi wa mpango!

Kila mtu awe responsible na matokeo ya starehe zake!
 
Kutoa ni moyo tuendelee kuwaunga mkono kwenye hizo biashara zao za kujishikiza inawezekana Kuna wakati wanalala njaa matajiri wote duniani kote wanatoa kwa wawahitaji bila kujali nani anaenda kuzitumia
Nitanunua kitu kama nitakuwa na uhitaji nacho na si kwa huruma.
 
Moja ya jambo kubwa tunapaswa kuwaeleza watu ni kuwa MTOTO NI GHARAMA.
Elimu ya watu kuhusu uzazi wa mpango ni ndogo sana.
Watu wanajipatia watoto tuu bila mpangilio maalumu mwisho wa siku anateseka sababu ya watoto au kuwatesa watoto kwasababu huwezo hana.

Una mkuta mama stendi amekaa anauza karanga za mia mia alafu mgongoni ana mtoto pembeni kalala mtoto mwingine Alafu kushoto kasimama mmoja ameshika dawa za mbu.. Ukiangalia watoto walivyopangana ni kama age ya mwaka mmoja mmoja..
Unajiuliza hivi kwanini hizi shida anazitaka? Why watoto watatu ndaji ya miaka mitano? Kipato chenyewe hakuna kitu cha maana.
 
Baba wa watoto wako wapi? Kuna Wakati natamani mno kuwaonea huruma lakini nyuma yao kuna wengi wameyataka na kukaidi ushauri wa wakubwa
Anko umeongea point kubwa sana kwa kujua au kutojua sio wote unakuta wengine walikua na ndoa zao kabisaa wakaishia kuzichezea dunia inawapiga wengine walikua hawashikiki la mwazini wala la mnadi swala, wengine kweli ambao ni wachache ni maisha magumu kweli kweli
 
Nakerekwa sana na watu maskini wanaozaa watoto bila kuwa na uwezo wa kuja kuwahudumia.

Wanaleta viumbe duniani waje wateseke bila sababu yeyote.

Ingekuwa inawezekana, Watu maskini wasizae kabisa.

Maana hawa ndio wanaongeza idadi ya maskini wengine duniani na gharama za serikali kuhudumia maskini wapya kila siku.
Huu ni ukweli kabisa lakini wengi watakupinga.
 
Usimuonee sana huruma mwanamke, kama angekuwa kinyume na hivyo alivyo asingekuwa na huruma .

Huku kwetu tunakoishi kuna dada mmoja alikua na maisha ya kawida sana yalio karibu na kuwa duni.

Kula na kuvaa kulala kwake kulikuwa jwa kubahatisha sana, huruma za wenye nyumba na madalali ndio zilimfanya apate sehemi ya kulala, alikua anapitiziza kodi hata miezi hadi sita bila kulipa kodi, alikua anatia huruma sana ukimsikiliza na kumuona.

Sijui ilikuawaje au kitu gani kilitokea kwa yule dada , na hapa ndio nakubaliana na Natafuta Ajira kwamba nusu saa inatosha kabisa kubadilisha maisha ya mwanamke moja kwa moja.

Huyo dada alipata pesa amejenga apartment kadhaa na anapangisha kwa kodi ya mwaka na haitaji maelezo!

Juzi tu alikua analia na kupiga magoti kwa mwenye nyumba amvumilie mwezi mmoja leo ana nyumba ukimuomba hata kwa magoti ulipie miezi sita hakuelewi.

Mwanamke anatia huruma na anakuwa mnyenyekevu sana akiwa na uhutaji, ila akifanikiwa hata kidogo tu amakuwa na kiburi na mwenye roho mbaya sana.
 
Ukatili ni kuleta kiumbe duniani kije kiteseke wakati mtu anajua kabisa yeye hana uwezo wa kuhudumia mtoto pindi atakapo zaliwa.

Watu maskini bora wakose kabisa uwezo wa kuzaa.

Ndio maana Afrika umaskini hauishi na hautakaa uishe, kwa sababu ya watu maskini kuendelea kuzaliana kuongeza idadi ya maskini wengine duniani.
Tulishasema san umu mtu kama hana uwezo asizae mwisho wa siku nikuja kuteseka kwa mtot atakae zaliwa tukaoneoana hamnazo kichwani

Na wengine waoasema kila mtot ako na riski yake 🤣
 
Umpe mimba umtelekeze halafu unakuja kivingine eti eeh ?

Hapa mtaani waumza mbogamboga wote wana watoto mgongoni, je baba zao mko wapi ?
 
Umpe mimba umtelekeze halafu unakuja kivingine eti eeh ?

Hapa mtaani waumza mbogamboga wote wana watoto mgongoni, je baba zao mko wapi ?
Baba zao tupo ila hao wadogo zako walitujibu hivi" mwanaume utakua wewe ? Wanaume wakiitwa na wewe utatoka babuu nipishe hata ukiniacha leo wenzako leo leo wananiweka ndani" basi hiko ndicho kilitokea bhana
 
Mwanamke wa kuonewa huruma ni mama yako tu na mama mjane ambaye pengine hana watoto au watoto hawana
uwezo kwa sababu kutopata malezi ya baba nk.

hao wengine sinaga muda nao nitanunua tu kama nahitaji lakini si kwa sababu etii ana mtoto.
sababu yako haina mantiki kabisa.
 
Kimsingi wa kuwasaidia ni wengi..kweli wale wamama wanatia huruma, na pia vijana na wazee wanaume huwa ktk mapambano yao..nao wako ktk magumu
 
kama huyu ndugu yangu ukimkuta achana naye anabwebwa habebeki,nilichogundua ni kwamba kiasili hana akili
 
Back
Top Bottom