Nahonyo
JF-Expert Member
- Dec 28, 2012
- 5,550
- 5,379
Dawa ni kuto tunza picha/video na SMS kwenye Simu futilia mbali huko.Sad story: Tuko kwenye group ya familia, familia 5 tofauti tofauti, Sio ukoo, Humo kuna Wababa, wamama na watoto.
Mama mmoja wa familia moja akatuma kwenye group clip ya ngono, mbaya zaidi ni anal. Sijui alikuwa anamtumia nani masikini.
Group lilipoa siku 5 mfululizo hakuna aliyecomment chochote, yule mama sijui nani alimshtua akafuta baadae.
Mpaka leo hii binafsi sina uhakika aliyefungua ile video, na ambae hakufungua, Sina uhakika kama mama yangu na kaka yangu mkubwa walifungua, (maana hawa ndio niliowawaza sababu ndio wanaonihusu)
Mama yangu ni kama hajui kilichotokea, sina hakika na kaka yangu na siwezi anzisha huo mjadala na yeye…. Nilipita kwenye hiyo stress as if mimi ndiye niliyetuma, sijajua aliyetuma alijisikiaje na familia yake. Nisiwe mnafiki binafsi niliifungua ile clip maana sina auto download , deliberately niliidownload nikaangalia nikafuta .
Swali langu kichwani hadi leo, nani alidownload nani hakudownload 😂
Mimi Simu zangu watoto wangu nawapa kwenda kutoa pesa, hivyo Password wanazijua hivyo Situnzi kitu ambacho siku moja kitanivunjia heshima.