Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Rais wa sasa Alikuwa nani wakati Magufuli anaharibu uchumi wa Nchi!?!

Au waliharibu nae!? Kama ni hivyo Roho ya uharibifu ipo Ikulu [emoji27]

Tuikatae na kuikemea....Nchi na Uchumi unaangamia...
 
Sasa na wewe unaniuliza swali tena wakati mimi nimekuuliza unitajie fedha zinakopwa na Samia zinafanyia nini? Hilo Gazeti ni kipindi cha Magufuli na siyo Samia, Mpango alikuwa Waziri wa Magufuli na fedha alizokopa Magufuli ndiko zilikoenda inajulikana na tunaona na siyo SGR tu hata Bwawa la Nyerere pia, sasa za Samia pesa anazokopa zinaenda wapi ? Zinafanyia nini ?
Hizo fedha zimesainiwa kipindi cha magufuli na zinaendelea kuingia kwa awamu mpaka sasa kadri ujenzi unavyoendelea. Zinaingia kama mkopo kwa Samia na zinatekeleza mradi uleule.

Hapa jaribu kujifunza project financing utaelewa ninachoandika.
 
Asilimia 67 wanataka kama hutaki utalipa kwa lazima,wengi ndio huamua.
hii sio kesi hata vyama vingi 80% walikataa, lakini 20% walishinda. Mandeleo hayataki mawazo ya watu wengi watu wachache wenye akili watalisha nyie wengi msio jielewa. Na humu JF its only and only place watu wana dare kuzungumza openly. Tunajua nyie mnaolipwa kufunika mawazo pia mmmo na mahali hapa ndio kazini kwenu. ndio mana tulitaka namba hao 67% waweke facts na namba zao humu uone.
 
Hizo fedha zimesainiwa kipindi cha magufuli na zinaendelea kuingia kwa awamu mpaka sasa kadri ujenzi unavyoendelea. Zinaingia kama mkopo kwa Samia na zinatekeleza mradi uleule.

Hapa jaribu kujifunza project financing utaelewa ninachoandika.

I don’t believe you, unakwepa kwepa tu na kuzunguka zunguka, yaani fedha zikopwe miaka iliyopita ziendelee kuingia tu siyo vipi kuhusu gharama ha kuservice huo mkopo? Siyo kwamba ni rahisi kutolewa kwa mara moja? Lakini bado haujasema Samia anakopa kufanyia nini?
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Acha uongo hizi tozo zimekuja mala baada ya samia kuchukua huu mkopo uliomtoa ndugai kwenye uspika
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
😂😂😂

Huyu sasa alikuwa wapi pindi hayo yote yakifanyika? Au ni muter au blind
 
I don’t believe you, unakwepa kwepa tu na kuzunguka zunguka, yaani fedha zikopwe miaka iliyopita ziendelee kuingia tu siyo vipi kuhusu gharama ha kuservice huo mkopo? Siyo kwamba ni rahisi kutolewa kwa mara moja? Lakini bado haujasema Samia anakopa kufanyia nini?
Hapa nadhani hauelewi utaratibu wa mega project financing.. fedha zinaingizwa kwa awamu kulingana na utekelezaji unavyoendelea.

Samia anakopa hela kuendeleza miradi iliyopo. Unadhani kuna cash mahali magufuli ametunza ndio wanachukua kuendeleza ujenzi?

Kama huamini nitajie mradi wowote uliosimama.
 
Kwa hiyo anakopa mara mbili? Kama zilishakopwa na zinaingizwa kwa awamu ulivyosema na makubaliano yako kuna haja gani ya yeye kukopa tena?
 
Kwa hiyo anakopa mara mbili? Kama zilishakopwa na zinaingizwa kwa awamu ulivyosema na makubaliano yako kuna haja gani ya yeye kukopa tena?
Kwahiyo serikali ikisaini mkataba wa mkopo maana yake mkopo unakuwa umeshaingia wote mara moja?

Fedha inahesabika kama ni mkopo ikishaingia kwenye bank na ndio inaingia kwenye rekodi za deni.

Kwahiyo kwenye hizo trilioni karibu saba ambazo zilisainiwa wakati magufuli yupo zinaendelea kuja na kusoma kama deni la taifa kila mwaka zinapoingia.

Otherwise kama mahela yote hayo yangekuwepo si wangeshakuwa wamemaliza dar moro toka enzi zile 2018 wakati magu yupo?
 
Asubuhi hii nimetuma 55000/= kwa mama kupitia simbanking, nimekatwa 5500/=...

Kwa lugha rahisi ni kwamba makato au gharama za kutuma hiyo pesa ni 10% ya nilichomtumia mama.

Nikiendelea kutumia hii simbanking basi CRDB mje mnivishe kibao cha "ZUZU" nimekaa palee Kariakoo Gerezani.

View attachment 2338227
Hapa boss hujajianika kweli?
 
Kwahiyo serikali ikisaini mkataba wa mkopo maana yake mkopo unakuwa umeshaingia wote mara moja?

Fedha inahesabika kama ni mkopo ikishaingia kwenye bank na ndio inaingia kwenye rekodi za deni.

Kwahiyo kwenye hizo trilioni karibu saba ambazo zilisainiwa wakati magufuli yupo zinaendelea kuja na kusoma kama deni la taifa kila mwaka zinapoingia.

Otherwise kama mahela yote hayo yangekuwepo si wangeshakuwa wamemaliza dar moro toka enzi zile 2018 wakati magu yupo?

Mpaka hapo sina shida, lkn kwa nini sasa raisi Samia anakopa tena kama tayari ilishakopwa kwa makubaliano kwamba fedha zitaingia kwa awamu? Na alipokopa hakuna niliposoma kwamba ni kwa sababu ya mradi xyz alioukuta, sababu za Mikopo yake zinaandikwa nyingine kabisa na hazina uhusiano na miradi iliyonzishwa na Magufuli, kama una chanzo kinachoonyesha raisi Samia kakopa kiasi kadhaa kwa ajili ya mradi xyz unaweza kuniwekea hapa …
 
Nimetuma 100,000 kwenda tigo pesa kwa simbanking, VAT sh. 974.70, govt levy sh. 1,009.00, TMS CHARGE TIGO 5,415.00, wenye akili timamu nimekatwa sh 7,398.7 kwa transaction hii moja tu. Pesa ilitoka kwa mshahara ambao wajuba walishakata PAYE. ni 7.4%. Mwaka 2017 kwa muamala kama huu nilikuwa naktwa sh. 2,360 maana yake sh. 5,038 imeongezwa kwa kipindi cha miaka mitano. Hali ya uchumi na inflation ni kubwa sasa kuliko ilivyokuwa 2017.

Jinsi mambo yanavyokuwa magumu tigo nimetoa sh 5,000 makato ni sh. 1,010 ambayo ni 20.2% hii ni zaidi ya 18% VAT. Tujuzane hapa mambo haya ya kukatana pesa tulizotolea jasho yataisha lini? Kwanini mnatukata kwa kiasi hiki kwa value ipi mnayotuongezea? Wale ambao mnalipwa kwa kushadadia na kujibu humu hata hili na nyie linawagusa pia, twendeni kwa namba kwanza.

Maisha sasa ni ghali mno na watunga sera lazima wawe flexible, kama mashirika ya kimataifa yanaona hali ngumu na kutoa nafuu kwa nini hawa viongozi wetu wanaweka pamba masikioni na kulazimisha kuendelea na mipango yao tu?! Maana hata midege tumelazimishwa kuyanunua bila kuona hali halisi na midude inaleta hasara. Reli toka waanze kujenga hawamalizi tu(Dar, Moro tu) politiks kila kukicha na wanatutwisha gharama bila sababu matokeo yake hata makampuni ya simu na yao yanatupiga pia.
Mtizame kiranja mkuu machoni,ndo utajua Nini Maana ya mlegezo
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Vyovyote utakavyo leta utetezi mfilisi haondoi ukweli kuwa JPM alitendea haki rasilimali za nchi kwa kuendesha miradi na ikanonekana wazi kuliko huyu aliyeruhusu kila mwenye ukwasi wake kufanya biashara za aina yoyote, kutengeneza filamu ya kuvutia watalii, kutoza tozo nyingi juu ya nyingine lakini hakuna chochote kinachoonekana zaidi kujigamba kwamba kafungua nchi akibebwa na mtangulizi wake ambaye miradi yote iliyopo ndiye mwasisi wake

Mradi wake alioleta ni chanjo ya UVIKO, kutengenea filamu ya kuvutia watalii, kutengeneza pesa kupitia tozo juu ya tozo bila kujali anayetozwa anamudu au hapana huku akipulizia upepo kwamba amefungua nchi na kurejesha demokrasia.

Siku nyingine jitafakari kuleta hoja yako yenye kumshambulia JPM unamwongezea uadui na chuki huyo raisi wako
 
58 siyo mara 2 ya 32,
Kama ulisoma hesabu ungemuelewa nadhani hujasoma namba ndio Mana. Namba Ina Tabia ya kukaribisha ama makadirio. 32*2=64 so take 64-58=6 ,58/32 = 1.8125 so hii ukikaribisha Ni almost Mara mbili mkuu. Kadiria katika kiwango kimoja. Pia hajasema exactly kuwa Ni twice yake Bali karibia unajua Mana ya karibia Ni approximately.
So ametumia mathematical language.

Samahani mie Niko kwa upande wa hesabu na sio hoja zenu.
I wanted to give out the clarification of mathematical language he/she used to express his/her argument/ideas.
Kama unabisha let us talk mathematically hapo tutakuwa marafiki Ila sio baina Samia and jpm
 
inabidi tubadilike. tujifunze kuishi kwa bajeti, yaani unapanga bajeti zako za mwezi, unadraw pesa benki mara moja tu. huko benki unaacha akiba tu. Matumizi ya kila siku unachimbia nje ya nyumba. La sivyo sisi wenye vimishahara uchwara ukiwa na tabia ya kuingia atm kila wakati, utajikuta 40% ya mashahara wako umeilipa serikali
Ndio ninavyofanya pesa ya matumizi madogo madogo inakaa nyumbani.

Huko nakwenda mara chache.
 
Mpaka hapo sina shida, lkn kwa nini sasa raisi Samia anakopa tena kama tayari ilishakopwa kwa makubaliano kwamba fedha zitaingia kwa awamu? Na alipokopa hakuna niliposoma kwamba ni kwa sababu ya mradi xyz alioukuta, sababu za Mikopo yake zinaandikwa nyingine kabisa na hazina uhusiano na miradi iliyonzishwa na Magufuli, kama una chanzo kinachoonyesha raisi Samia kakopa kiasi kadhaa kwa ajili ya mradi xyz unaweza kuniwekea hapa …
Samia amekopa fedha nyingi za imf na wb kwa ajili ya kupambana na makali ya covid, ujenzi wa madarasa na kiasi vita ya ukraine. Pia ameendelea kutumia baadhi ya hizi fedha kulipa madeni ya ndani kama wazabuni na pssf.

Mikopo mingine ni kwenye muendelezo wa phases za ujenzi wa reli (maana phase nyingine walikuwa bado wanatafuta fedha), kigongo busisi, barabara, bwawa la umeme etc
 
Una chanzo kinachoonyesha raisi Samia kakopa fedha kwa ajili daraja la Busisi, Barabara au Bwawa la Umeme? Hizo za IMF na World Bank najua, ila ningependa kujua chanzo kinachoonyesha mahali raisi Samia kakopa kwa ajili ya Bwawa la Umeme au barabara kubwa yoyote ile!
 
Back
Top Bottom