Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Haueleweki unaongea nini..

Mimi ninaonesha namna magufuli alivyoanzisha tatizo la nchi kukopa sana baada ya kuharibu uwekezaji nchini. Huyu Samia ni incompetent hivyo hawezi kusimamia nchi kwa hali ilivyo. Anatakiwa rais mwenye akili kubwa.
pole sana
 
mungu wenu alishasemaga kuwa ashauriki, na ukimshauri umeharibu kabisa, kuna wakati PM alisema ashapata wanunuzi wakorosho, yeye akamjibu hataki kusikia habari hizo,ashamuamuru CDF maroli yaende kusini kusomba korosho,

Kilichofuatia baada hapo kila mtu anajua, soko la korosho likashuka na wakulima walitiwa umasikini wakutisha, mzee akawa anaogopa hata kutaja neno korosho, alikuwa one Man show

Why hawakuondoka?
 
Samia amekopa fedha nyingi za imf na wb kwa ajili ya kupambana na makali ya covid, ujenzi wa madarasa na kiasi vita ya ukraine. Pia ameendelea kutumia baadhi ya hizi fedha kulipa madeni ya ndani kama wazabuni na pssf.

Mikopo mingine ni kwenye muendelezo wa phases za ujenzi wa reli (maana phase nyingine walikuwa bado wanatafuta fedha), kigongo busisi, barabara, bwawa la umeme etc
Championship ungeanza kwa kumuandika Mama au Rais Samia hata kama anapitisha sheria za wale wapigaji bila kuangalia madhara yake..
 
Miradi hii hii inayoenda spidi ya kobe ?

Mbona enzi za JPM spidi ya at miradi tulikuwa tunaiona bila hizo tozo ?
Nitajie mradi wowote uliokamilika kipindi cha magufuli ukiondoa brt ambayo kila kitu kimeandaliwa na kikwete, flyover ya ubungo iliyojengwa na world bank na ile ya tazara iliyojengwa na wajapani.
 
Unaona sasa kumbe ni empty air, hauna chochote cha ku back up unayoyasena na uko subjective lkn hauna unachoweza kuonyesha na unategemea anachosema raisi Samia? Mpaka leo hii ulitegemea chochote positive kumhusu Magufuli akiseme hata kama kipo? BTW kuhusu hazina Gavana wa Benki Kuu alishasema kuhusu fedha za kigeni ambazo nchi inazo zinatosha kuendesha nchi kwa miezi 6, hiyo ni Benki Kuu ilisema, karibia mwaka uliopita, hatujui hali ikoje sasa hivi!
Kama hujaelewa katika maelezo yangu yote basi tukubali kutokubaliana.
 
Jamaa hebu kuwa mkweli na muungwana. Deni la taifa lilikuwa trilioni 32 mwaka 2015 na lilikuwa trilioni 58 wakati magufuli anafariki. Yaani alizidisha karibu mara mbili deni la serikali kwa miaka mitano.

Moja ya sababu iliyonifanya nimchukie sana magufuli ni tabia yake ya kusema uongo. Amekopa sana afdb, world bank, imf na mbaya zaidi mpaka mikopo kwenye mabenki ya biashara lakini majukwaani anasema hela za ndani. Watanzania kwa ujinga wao wanamuamini. Hata michango ya pssf alikuwa hapeleki hivyo deni la ndani pia liliongezeka sana.
32T to 58T hii unaweza kusema alizidisha karibu mara mbili wewe mbwea
 
Rais wa Sasa amekuta Nchi haina fedha, Magufuli aliharibu uchumi wa Nchi kwa miradi mfululizo na mikopo ghali ya riba kubwa na ya muda mfupi
Weka ushahidi wa hayo uliyosema kama mleta mada alivyofanya....acha kupiga mdomo!
 
Mikopo, tozo, Kodi hakuna matokeo yoyote. Zaidi tunaona misafara ya viongozi ikiongezeka, wakiagana na kupokeana uwanja wa ndege karibu serikali nzima, kila wiki, posho, vikao, nk. Matumizi yasiyo na tija kwa Taifa.

Wabane matumizi serikali yasiyo ya lazima, watuonyeshe kila senti inapokwenda, wasikilize wananchi wanapowapa ushauri jinsi ya serikali kuongeza kipato chake.


Itafikia wakati kila mtu analipa 60%, 70% ya kipato chake kwa serikali kwa speed hii ya kuongeza tozo, Kodi halafu hakuna chochote kinachofanyika kwa faida ya Taifa.
 
Kuna mtu anaudhi anakasirisha kusema et Rais kaikuta nchi haina pesa!!!
Hakuna kipindi viongozi wa shamba hili la bibi wanakula maisha kama awamu hii dhaifu, wapigaji hawana wanaemuofia wapo huru hawajali na wanafuraha na familia zao zipo salama hawana mashaka.
Tunaoonekana mang'ombe (wapiga kura) ndio tunahangaika na kulialia kila uchao.
Tozo zozote haziwahusu na hawazijali kwakuwa ni kitu kidogo mno kutokana na wanachovuna ktk shamba la bibi.
 
Weka ushahidi wa hayo uliyosema kama mleta mada alivyofanya....acha kupiga mdomo!
We ushaidi unashindwa kuutafuta humu mtandaoni , mbona kila kitu kipo wazi kabisa,

Tembelea website za vyombo mbalimbali vya habari utakuta ushaidi kibao wa habari hata za miaka kumi nyuma
 
Huyo mama karithi tatizo ambalo hana uwezo wa kulitatua hasa ukiweka vita ya ukraine pamoja na athari za covid.
Covid ipi ? Hii Covid ambayo imemfanya apate fungu la kutosha na kujenga madarasa ambayo ndiyo yamekuwa wimbo ?

Na vita vipi ? ambavyo watu walinukuliwa kwamba vitatupa fursa ya kusafirisha gesi ?
 
Jibu hoja makato ya tozo na watoa huduma yapi makubwa?
Sasa unataka watoe huduma bila gharama ? Hapo ukitoa overheads na Kodi wanayotozwa na serikali hio hio (ambayo imeongezeka) unategemea bado charges ziwe ndogo kuliko yule anayechukua bila cost yoyote ?
 
Kwani Ndugu Huwezi. kutoq Hela zakoUkaweka Ndani kwenye. kibubu. ?

Maana Siku hizi Safe Box zinauzwa Tu Town
Akilipwa salary inaingia kwenye kibubu ? Au akimtumia mzazi wake kijijini atatuma kwa njia ya Posta ?
 
Ngosha hakutaka kushauriwa kwa lolote, kwa lawama zinamfaa peke yake,

Samia Ni Rais Bora kwa afrika
Kama washauri ndio hawa fisi walamba asali, thank god alikuwa hashauriki..., hawa hata wasiosikiliza vilio vya wananchi ndio wasikilizaji ?
 
Sasa unataka watoe huduma bila gharama ? Hapo ukitoa overheads na Kodi wanayotozwa na serikali hio hio (ambayo imeongezeka) unategemea bado charges ziwe ndogo kuliko yule anayechukua bila cost yoyote ?
Sasa huoni gharama za watoa huduma ni kubwa kuliko uhalisia? Yaani kuwezesha kutuma pesa ndio wakate elfu 6?

Yet unalaumu tozo ya serikali 1600,uko serious kichwani wewe?
 
Sasa huoni gharama za watoa huduma ni kubwa kuliko uhalisia? Yaani kuwezesha kutuma pesa ndio wakate elfu 6?

Yet unalaumu tozo ya serikali 1600,uko serious kichwani wewe?
Kwenye faida ya hio miamala serikali wanawalipa ngapi ?, na umecheki overheads zao ni kiasi gani na shareholders wanalipwa ngapi ?

Huwezi kuwapangia watu bei bila kufanya due dilligence na kuangalia all costs involveld... Na kama ni rahisi sana kufanya kwanini Serikali isifanye hata kwa tshs elfu 2 na kukeep all the profits ?
 
Back
Top Bottom