Tuzioneni tozo kwa facts na namba, zinaumiza hapa wenye namba tu

Makali gani ya Covid wakati hata ugonjwa haukuwa tishio sana nchini. Zaidi ya kuwafyeka Elites na wazee kadhaa wa kadhaa.

Maumivu ya Covid wala hayakuhitaji loans sababu hata lockdown hatukuwa nayo. Kwa aibu kubwa hizo hela zimesingiziwa ni za Covid ila zilivyotua wameelekezea kwenye madarasa na zahanati. Ila ukiskia ya tozo zinafanya kazi hio hio.
 
Uwezo wako wa kufikiria ni mdogo..

Kwa hiyo wanafunzi waliomaliza form six na kuomba chuo mwaka huu wanakuwa na account za nini na pesa hawana walikuwa tegemezi.kwa wazazi?

Nimekupa Takwimu za serikali kwamba miamala iliongezeka na sekta ya mawasiliano ilirekodi ukuaji mkubwa Kwa mwaka ulioisha wewe unaleta blaa blaa..

Serikali imeshusha tozo Kwa sababu 2,moja mfumuko wa gharama za maisha umekuwa mkubwa Kwa sababu za vita na pili sababu ya pili ni kuongeza wigo zaidi kwa watumiaji wengi..

Na Ili kuleta uwiano ndio maana wameongeza tozo banks,ingekuwa tozo zinaathiri uchumi wangezifuta na Wala wasingeweka tozo mmpya banks na vinga'amuzi..
 
Hata Magufuli nae alikuta hali hio hio! Kwahio inaonesha ni kawaida raisi akiwa anakaribia kusepa madarakani anazoa hela zote 😂😂😂
 
Ilimradi utetee ujinga tu, shenz type 2
 
Hata Magufuli nae alikuta hali hio hio! Kwahio inaonesha ni kawaida raisi akiwa anakaribia kusepa madarakani anazoa hela zote 😂😂😂
Magufuli alikuwa muongo hakuna hazina iliyokuwa tupu bali zilikuwa kiki kama kawaida yake..

Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani..

Samia kakuta Hazina imekauka sio kwa sababu ya watu kuzoa bali Nchi ilikuwa kwenye hali mbaya ya uchumi,udokozi ukifanyika kidogo ila sio kwa kiwango cha kuzoa hazina yote..

Nimewaambia bila Serikalini kupata mkopo wa dharura wa covid 19 Ili ku stabilise shilingi na kuimarisha forex reserves Nchi ingeshindwa kuagiza bidhaa muhimu..

Pia pesa zile zilisaidia kuleta liquidity kwenye uchumi
 
Kumbe kufungua nchi = Kuachilia mafisadi na wezi wawe huru kufanya wizi na unyang'anyi kwa baraka zake.zote
 
yani wewe kila kitu cha awamu hii unatetea umekuwa chawa hadi unakera
 
Ila yeye Samia ndio alikuta hazina Empty? Mwehu kweli wewe, na zile hela walizodokoa in billions siku kadhaa baada ya mzee kufa zilitoka kwenye pochi ya Samia?

Hakuna raisi ambaye alikuwa serious na kukusanya hela kama Magufuli. Tena hela safi sio zile za mauzo ya madawa wala ushenzi wowote ikiwemo ujangili na kutorosha wanyama kwenda arabuni.

Magufuli ndie alianzisha system ya GePG na system zingine za electronics za kuchukua hela moja kwa moja bila kupitia wadokozi waliozoea cash in hand. Yeye ndio aliwageuza wahasibu kuwa raia wa kawaida sana. Hela zote alikuwa anakusanyia hazina halafu mnasema eti hazina haikuwa na hela huku hajawi kumrusha hata mtumishi mmoja mshahara wake?

 
Uwezo wako wa kufikiria ni mdogo..

Kwa hiyo wanafunzi waliomaliza form six na kuomba chuo mwaka huu wanakuwa na account za nini na pesa hawana walikuwa tegemezi.kwa wazazi?
Kweli naongea na zezeta au robot na sio mtu, kwahio wakifika chuo ndio sio tegemezi tena ? Au wakiwa form six huko boarding hawatumiwi pesa ? Hivi wewe unaishi practically au maisha ya kinadharia....
Nimekupa Takwimu za serikali kwamba miamala iliongezeka na sekta ya mawasiliano ilirekodi ukuaji mkubwa Kwa mwaka ulioisha wewe unaleta blaa blaa..
Wewe unaleta takwimu bila kuangalia uhalisia ndio nyie mkiambiwa mmeshiba wakati mnasikia njaa mtaona ni sawa tu sababu fulani kasema basi ni sawa..... Ingawa mtaani uliza wakala yoyote wa Pesa kuhusu kupanda au kushuka kwa transactions atakwambia nadhani ndio utaacha kuamini kila pumba na propaganda inayotoka kwenye midogo wa wanasiasa...
Serikali imeshusha tozo Kwa sababu 2,moja mfumuko wa gharama za maisha umekuwa mkubwa Kwa sababu za vita na pili sababu ya pili ni kuongeza wigo zaidi kwa watumiaji wengi..
kwahio walivyopandisha mwanzo wigo wa watumiaji ulikuwa umetosha wakaamua upungue ?

Na Ili kuleta uwiano ndio maana wameongeza tozo banks,ingekuwa tozo zinaathiri uchumi wangezifuta na Wala wasingeweka tozo mmpya banks na vinga'amuzi..
Hawa walamba asali nothing they do makes sense..., kuna vitu wanafanya unajua kabisa they can not be out of touch to such an extent kwahio jibu ni they dont care..., ila huko ni kuwa myopic as marginalizing majority hata wao maisha yao yatakuwa hatarini..., sababu hawatapata muda / amani ya kutumia mazao ya unyonyaji wao wakati wamezungukwa na wasionacho....
 
Nitajie mradi wowote uliokamilika kipindi cha magufuli ukiondoa brt ambayo kila kitu kimeandaliwa na kikwete, flyover ya ubungo iliyojengwa na world bank na ile ya tazara iliyojengwa na wajapani.
GePG alianzisha Kikwete?
 
😂😂 Hiyo system ni nzuri sana.. tuliibuni pale eGA
Na hilo ni baada ya so many years kudharau wataalamu wetu wenyewe😂! Kuonyesha dharau zaidi Makamba kaenda kukodi system kwa billion 69! Magufuli ndie angekuwa raisi the day jamaa amefanya hilo ndio ingekuwa siku yake ya mwisho kupanda V8 ya Wizarani😂
Ila kwakuwa mama yuko madarakani na kabariki ufisadi, watu wanajifanyia watakavyo tozo zikija kusomwa mkeka wake na CAG utacheka.
 
Yeah kuna zile kasumba za kutowaamini wazawa. Kuna project moja ya tcra hapo tulifanya miaka kadhaa iliyopita nikashangaa sana vitu vya kawaida kabisa wameleta consultant kutoka sweden nadhani na kuwalipa mamilioni ya dola kwa kazi ambayo wataalamu wetu hapo voda na tigo wangeweza kuifanya.
 
Consultant ni upigaji tu wala sio kingine
 
Ccm mbere kwa mbere.

Hii inawahusu wafuasi wa chadema tu. Sisi wa Ccm hayo makato tunaona mkilalama tu mitandaoni.
Andamaneni sasa muone mtapigwa mpaka mchakae🤣🤣
 
Wazalendo wezi
 
Katika kosa sifany ni kurusha kutoka simbank kwend mobil.yelewiiii ni wanakata.sijajua ni kwanin ila duh
rushia elfu 1 kutok mobile nmb makato 804.hee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…