Hili jambo limesumbua sana wazazi, na shule zingine huwezi kiuamini kama wanafanya mchezo huo kwa sababu ni shule za dini mno,ila watoto wakiwa pale, wanaanziana huo mchezo mchafu.
Hivi hizo shule hazina waalimu? hawana intelijensia ya shule, mbona wakifanya uchunguzi wanafunzi wenyewe wanajuana kuwa huyu wa fulani na yule wa fulani? watu hadi wanapata shida watoto wao wakiwa wanasoma huko.
Nini kifanyike? wanaume wameoa wake wengi tu mitaani huko wakiwa shule walikuwa wake wa wanawake wenzao na walikuwa wanalelewa. kuna shule moja walikamata binti anasaga wenzie hadi ana zana katambea nazo kwenye begi toka nyumbani.
Hebu mliosoma shule za girls tu tuambieni, hali uwa ipoje huko? kwa wanaume mchezo mchafu huwa haupo kabisa ukiondoa masterbation.
Soma Pia: Vijana wengi wameathiriwa na kujichua na kusagana
Mifumo ya shule na taratibu za shule ni mifumo inayofanana sana na mifumo ya magereza na wakati mwingine ni mibaya zaidi mana inajenga kizazi cha watu waoga na wasioweza kusema ukweli na kukemea uovu.
Walimu ni wakali sana na wanaona ufahari kuogopwa sana na wanafunzi.
Sasa mwanafunzi anayemuogopa mwalimu kuliko hata polisi anawezaje kumweleza matatizo yake au hata kusema yale yanayofanywa au anayofanyiwa na wenzake.
Dunia imejaa watu waovu na kinga ya uovu ni siri .
Kila mahali ni siri tu kuficha uovu badala ya kuuweka wazi.
Kuna mwalimu wa shule ya msingi alimpa mtoto wa darasa la tano mimba . Wenzake wengi wanajua kuwa ni kweli akafunguliwa kesi na akasimamishwa. Chama cha walimu lilisimama kidete kumtetea mwalimu mwenzao na kumwekea mawakili mpaka akashinda na kurudi kazini.
Nikajiuliza sasa hiki chama mbona hakipiganii maslahi mengine ya walimu? Nikajua Kumbe wanafunzi hawana mtetezi wa kupigania maslahi yao!!
Mwanafunzi amebakwa na mwalimu lakini juhudi za kutafuta haki ya mwanafunzi inakosekana hivyo mtuhumiwa anaambiwa kubwa hana hatia na mwanafunzi anakosa haki yake hata kudai fidia.
Kwa hiyo wanafunzi wa kike kusaganya ni kutokana na mifumo ya kimagereza ya shule zetu . Mwalimu na mwanafunzi anayetafuta elimu akiwa shuleni ni kama askari magereza na mfungwa ambaye ni muhalifu.
Shule nyingi siku hizi hazina vipindi vya michezo na kazi za nje za mikono kuanzia saa tisa kila siku .
Na pia walimu wa kike ndio wanaolia wakatili zaidi kwa wanafunzi wa kike jambo linalowafanya wakose pa kusemea na kueleza changamoto zao.
Ushauri wangu kwa serikali:
Kiundwe chombo maalumu cha kusimamia na kusikiliza changamoto za wanafunzi mashuleni kwani na vyuoni ili kubaini mapema matatizo na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa .
Wanafunzi wakarifi wanaweza kupelekwa shule za watoto watukutu ili wakaishi kama wafungwa ili wale wema waishi kwa amani na ustarabu kuliko kuwachanganya mbwa mwitu na kondoo. Hasa Private school kuna watoto mpaka mafreemason.