Tafadhali wote wenye ushahidi au taarifa juu ya huu ukatili wanitumie ujumbe kwenye namba 0765345777 au 0734124191 ili tuelewe vizuri zaidi tupange uchunguzi kwa hatua zaidi. Na iwapo jambo hili lipo, huu ni unyanyasaji wa kijinsia na tukimpata au kuwapata hawa makatili, watatutajia mnyororo mzima uchukuliwe hatua. Aidha , taarifa zitasaidia kumulima utaratibu mzima wa hizi huduma.
Lakini ndugu wanawake na mabinti, jilindeni na huduma ambazo hazina usajili au utaratibu rasmi popote pale, ni hatari.
Naitwa Dkt Gwajima Dorothy Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu. Ahsante Sana.