Ubalozi wa Marekani: Mbowe ameshambuliwa kikatili, wakumbushia pia shambulio la Tundu Lissu huku kukiwa hakuna hatua zilizochukuliwa

Anayesema haki ya kutupigia kelele hawana anajidanganya, USA wanatupa misaada lazima watupangie conditions hahaha, tungekua hatutaki kelele kwanza tuwe matajiri wenyewe hiyo misaada tusihitaji tena. Kwa sasa hivi hata bajeti yetu yenyewe inategemea sana misaada yao lazima watupangie wanavyotaka, wana principle zao na wanataka nchi zote wanazozisaidia zifate.

NI kama wewe mtu akija anahitaji msaada flani, mtu mlevimlevi hela unajua ukimpa ataenda kuharibu, lazima umuwekee conditions sio kumuacha afanye analotaka. Marekani na hata UK wanatufanyia hicho hicho.

So stop complaining, fanya kazi tuwe matajiri tuache kuwategemea ndipo wataacha kutupigia kelele. As of now ni haki yao kabisa kulalamika
 
Hatimaye tunaowaita kuwa ni mabeberu wazidi kuunguruma dhidi ya matukio ya kihuni ya kushambuliwa viongozi wa upinzani yanayoshamiri nchini.
View attachment 1473622
Hawa nao wanabweka bweka tu kama mbwa koko wakapambane kwanza na Rais wao Trump kashindwa uongozi kashindwa na corona pia kazi kubwatuka tu mzungu toka lini akawa na mapenzi ya dhati na mtu mweusi kama sio unafiki
 
Usa hana haki ya kunyoshea Tanzania mkono nchiambayo maaskari wanaua Wananchi wake barabarani ndio inanyoshea Tanzania mkono
Wapeleke upumbafu kwao


Mbowe aache maisha ya kihuni yeye ni kiongozi
Vipi wale Watanzania 7 wasio na hatia waliouawa na POLICE kule Kagera Jana?Nani wa kuwasemelea?Tunasikia ni majambazi,mahakama gani iliyowahukumu?Who investigated their case?
Watanzania tusipende kushabikia vya wengine ilhali kwetu panawaka moto.Haki ni kama mafuta,ukiyatia kwenye Maji yatazama kwanza lakini yatarudi juu. Tutendeane kama tupendavyo kutendewa.
 
“Ninachoweza kusema mbele ya vyombo vya habari ni kwamba Mhe.Freeman Mbowe hakuwa peke yake wakati tukio hili linatokea, nisingependa kuingia kiundani kwamba alikuwa na nani na aliyekuwa naye ameona nini”. Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika.
Maccm yanaleta porojo wakati shahidi yupo
 
Walevi lazma mteteane tu ,pombe kanywa mwingine lawama apate mwingine
😊
 
Polisi wanauwa sana tu huko Marekani ni kawaida.
Hebu jaribu kufananisha rank ya uhalifu:Tanzania na US.Askari wa Marekani kutumia nguvu kupita kiasi yamkini inasababishwa na hali yao ya uhalifu ipo juu(though is not justified) .Tanzania Akwilina alikuwa na hatia gani au wale viongozi wa chadema walijihami kwa silaha mpaka warushiwe risasi iliyompata Akwilina?David Mwangosi kupigwa risasi na polisi alikuwa amejihami kwa silaha nzito?
 
Post bora Dunia nzima
Unamaanisha hata wasukuma tunaompinga JPM na Ndugayi nasi ni wanyama ??

Unapopinga uovu wa mtu fulani usihusisshe kabila lake unataka kusema wasukuma na wagogo wote ni wanufaika wa huu udhalimu wa JPM.

Be reasonable.
Kaka niunganishe kundi la Wasukuma tunaompinga JPM na Ndugai.

Asante.
 
Usa hana haki ya kunyoshea Tanzania mkono nchiambayo maaskari wanaua Wananchi wake barabarani ndio inanyoshea Tanzania mkono
Wapeleke upumbafu kwao


Mbowe aache maisha ya kihuni yeye ni kiongozi
Kwahiyo kwa akili yako, unataka kuifananisha USA na hii shit hole country? Au una maana tofauti?
 
Wasalaam wanabodi,

Nimeona twit ya UBALOZI WA MAREKANI wakilaani au KUSIKITISHWA na kuvamiwa na kuumizwa kwa mbunge na kiongozi wa upinzani bungeni Mh Freeman Aikael Mbowe.

Kitu ambacho kimenishangaza ni kuwa UBALOZI huo umesema moja kwa moja kuwa mh Mbowe kashambuliwa ilhali taarifa za uchunguzi bado hazija toka na swala lenyewe bado lipo katika uchunguzi.

Je, wao wamepata wapi uhakika kuwa mh Mbowe kavamiwa? Je ni sawa kwao kutoa taarifa kabla vyombo vinavyohusika kutoa taarifa?

Kwa kuwa kumekuwa na conspiracy nyingi tu juu ya tukio hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…