Mkuu Ngogo ukitoka Bukoba pitia hapo Nyamagana ufanye tathmini kwa kijana wetu Pambalu. Ukimaliza hapo njoo hapa Shinyanga umtathmini dada yetu Salome Makamba! Mwaka huu ma CCM yanapumulia mashine!
Hakuna uchaguzi rahisi lakini Gambo hawezi kumshinda Lema hata kama akifanya kampeni bila nguo, kingine ambacho wana Arusha wanamkataa Gambo ni kwa vile alitumia madaraka yake vibaya sana kwa kushiriki kukomoa wapinzani akiwemo Lema na alichangia sana kukwamisha juhudi za mbunge ikiwemo sakata la Hospitali ya Mama na mtoto.Mkuu ww ni mkazi wa arusha? Kama sio mkazi vunga basi msimchukulie poa gambo. Lema anakazi ya kufanya sio kirahisi kama unavyodhani
Mchaga kuwa mbunge Dar inawezekana pasi na shaka,ila mzaramo kuwa mbunge moshi au Arusha hiyo haiwezekani na ikiwezekana basi itakua ni dharau kubwa sana.Kwa hiyo Mzaramo sio mtu,mbona Chadema ina wagombea ubunge wanne Dar kutoka mkoa mmoja wa kaskazini.
Chuga ndimi zenu.
Haa😁😂😀Hakuna uchaguzi rahisi lakini Gambo hawezi kumshinda Lema hata akifanya kampeni bila nguo
Mchaga kuwa mbunge Dar inawezekana pasi na shaka,ila mzaramo kuwa mbunge moshi au Arusha hiyo haiwezekani na ikiwezekana basi itakua ni dharau kubwa sana...
Umejikaza kweli mpaka ukaandika haya.Mrisho Gambo atamgaragaza Lema saa 4 asubuhi!
Kwa nini usianzishe thread yako? Ukisikia kudandia gari kwa mbele ndio huku, haya inahusiana vipi na Gambo kugaragazwa asubuhi na mapema na Lema?Duniani hasa mataifa ya afrika kinapokaribia kipindi cha chaguzi mbalimbali kwenye haya mataifa, baadhi ya makundi huingiza pesa haramu kufadhili vyama ,au makundi mbalimbali ili yaunde serikali kwa makubaliano flaniflani yenye lengo la kuweka watu wao ambao watakua -remoted.
Fedha hizo huingizwa nchini si kwa ajili ya kufanyia kampeni ,bali hutumika kuandaa vikundi mbalimbali vya kihalifu kwa lengo la kufanya hujuma na mashinikizo flani yenye maslahi ya wachache na si kwa nchi husika .
Niipongeze serikali hasa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuliona hilo mapema sana .
Ifahamike vyama hasa vikubwa vya upinzani nchi kwa mujibu wa sheria vinapokea ruzuku kila mwezi, na pia huchangishana ,kazi ya fedha hizo ni pamoja na kuzitunza kwa ajili ya chaguzi mbalimbali ukiwemo na uchaguzi mkuu wa mwaka huu .
Inasikitisha kuona mgombea anatoka hadharani kulalamika ya kwamba pesa imezuiliwa kuingia nchini ,ooh! wafanyabiashara tuliokuwa tunawategemea wamehama nchi ,ni kina nani hao waliohama nchini ?na wanapodhamini uchaguzi nini matarajio yao kama si ukwepaji wa kodi?,
Suala la kujiuliza kwanini pesa hizo zije kipindi hiki cha uchaguzi ?,nani mfadhili wa hizo pesa ?anatarajia nini kwa anaowafadhili?,imani yangu kuna nia ovu dhidi ya taifa.
Uchaguzi ni mchakato wa muda mrefu wenye maandalizi ya kina yalioratibiwa kwa ustadi makini sana .
Namalizia kwa kusema wote ambao mnagombea dhamira zenu ni kujinufaisha binafsi na si taifa mtashindwa kwa aibu sana
Mzaramo huyo, halafu tuna hasira na wazaramo bado tunamkumbuka waziri Jafo alivyowaengua maelfu ya wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, bloody good morning!Huyo siyo Mzaramu na ukabila usipewe nafasi
Kwenye uchaguzi huu; kuna majimbo matatu magumu kutabiri mshindi Tanzania; Arusha mjini ni mojawapoHeshima sana wanajamvi,
Mbio za ubunge katika jiji letu la Arusha sasa zipo wazi kabisa kiasi kwamba hata kipofu ni rahisi kujua na kufahamu nani atashinda ubunge.
Mara baada ya Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo kupitishwa na kamati kuu kugombea ubunge Arusha Mjini kulikuwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wanaCCM kindakindaki. Wengi walijiuliza kulikoni kamati kuu kupitisha jina la mgombea ambae tayari alishasemwa hadhani na mheshimiwa Rais na hata Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr Bashiru.
WanaCCM wengi walikubaliana pengine kamati Kuu iliangalia nani mwenye uwezo wa kushinda nafasi ya ubunge na kuviweka vigezo vingine kando ikiwemo tuhuma za rushwa, uchonganishi (kiwanja cha Msikiti Mkuu Bondeni), kukwamisha ujenzi wa stand mpya, kuhujumu ujenzi wa shule mbali mbali kwa kisingizio cha udogo wa viwanja na nk.
CCM iliamini na kujiaminisha kwamba Mrisho Mashaka Gambo angewavusha salama katika uchaguzi mkuu, hapakuwemo mgombea mwingine wa kumzidi yeye.
Katika hali ya kushangaza sana kama si kusikitisha Mrisho Gambo Mashaka amepwaya kweli kweli, zile amri zake za ukuu wa Mkoa hazifui dafu katika kuomba kura. Mrisho bila ngoma,mdundiko na wacheza show hawezi kufanya mkutano,Mrisho bila kukusanya watu toka kata mbali mbali za wilaya ya Arusha Mjini,Arumeru hawezi kufanya mkutano, Mrisho Gambo bila usaidizi wa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa hawezi kufanya mkutano. Mrisho Gambo yuko hoi bin taaban kisiasa na kiuchumi. Matajiri wengi wamejiweka kando na kampeni zake hawataki kutoa fedha tena wanamwangalia kama gari bovu.
Zipo tuhuma sijui zimetoka wapi, sijui nani kazianzisha zimesambaa kwa kasi ya ajabu juu ya kuungua soko la Samunge loooh hata kuandika naogopa soko la Samunge ni kaa la moto si mtaji tena wa Mrisho.
Naomba kuwasilisha.
Ngongo safarini Bukoba kwasasa nipo Katerero sokoni.
Tena katika sisi mazuzu anatuongoza huyo aliyetoa hoja akijiona anajua kumbe hajuiShida kubwa ya Watanzania mara nyingi ni kujifanya wajuaji... unajua kwamba kufadhiliwa wakati wa kampeni iko kisheria?
Una fikiri wangeropoka hadharani hao unaowaongelea?
Swali lako kwamba wanatarajia nini wakifadhili mgombea... nikuulize kwanza, achana na wafadhili wa nje, kwa nini wafadhili wa ndani watoe support kwa chama cha siasa yoyote ile? Na iko halali kisheria kabisa!!
Shida hamwelewi maana mapana ya demokrasia na jinsi kufanikisha demokrasia, tumeiokota tu kutoka kwa nchi za magharibi lakini hatuwezi ku-apply kikamilifu kwa sababu bado fikra zetu ni finyu.. halafu mabavu yanatumika na wenye nchi kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi ni mazuzu tu, upende usipende.
Sent using Jamii Forums mobile app
Dar siyo ya wazaramo, wazaramo kwao Pwani Dar es salaam wenyewe waarabu na sisi wajanja tuliohamia. Wametoka milima ya Matombo wakazaramiaKwa hiyo Mzaramo sio mtu,mbona Chadema ina wagombea ubunge wanne Dar kutoka mkoa mmoja wa kaskazini.
Chuga ndimi zenu.
..mbona makongoro nyerere alikuwa mbunge wa arusha mjini na alimshinda mchaga felix mrema?
..watu wa arusha wanataka wagombea wenye amsha-amsha kama makongoro nyerere, au godbless lema.
..ccm mmekosea kumsimamisha mrisho gambo ambaye anaonekana kuwa na aibu na yuko legelege.
Endelea kujitafutia matatizo.Dar siyo ya wazaramo, wazaramo kwao Pwani Dar es salaam wenyewe waarabu na sisi wajanja tuliohamia. Wametoka milima ya Matombo wakazaramia
Kwa kusema kweli? Dhamira yangu ni kusema kweli daima fitina kwangu mwiko. Nikosoe kwa hojaEndelea kujitafutia matatizo.