Uchache wa Waombaji Kazi kwa Post za Assistant lecturers

Ni kweli kabisa. Ila sijiskii amani kufanya hiyo kazi ya ulecturer. Amani ipo kwenye biashara zaidi na siasa.
Nimepewa tender ya kusupply unga wa muhogo non food grade tani 300 na price ni 700,000/= per tone price at factory gate.

Tuchangamkie au wewe unataka biashara gani?
 
Kwa mliosomea fani za educational psychology, educational guidance and counseling, special and inclusive education, early childhood education Hadi masters level hizo nafasi Bado zinakosa wajazaji wa nafasi
 
Nakuunga mkono mkuu.

Mimi nilifanya interview (Tutorial Assistant) Mzumbe Morogoro mwezi Agosti ila sikufanikiwa kuitwa ajili ya Oral interview. Tuliokuja kwa ajili ya nafasi za Tutorial Assistants tulikuwa wengi kila kozi (20+, 100+ na wengine 200+ kwa ajili ya nafasi 2 tu). Ila waliokuja kwa ajili ya interviews za Assistant Lecturers walikuwa wachache sana (3, 5, 10, nk). Katika kozi moja ya masters, alikuja mmoja tu kufanya interview kwa ajili ya nafasi ya Assistant Lecturer - sikumbuki kama alifanikiwa kupita au la.
Hivi karibuni nimesikia kuwa Mzumbe iliwachukua wote waliokuja kwa ajili ya interview (nadhani ni Assistant Lecturers) kule kwenye campus yao ya Dar es Salaam.

Sijui kwa nini serikali haiwaruhu basi hata vyuo vyenyewe viwe na mandate ya kuajiri Tutorial Assistants (iwe ni part time au full time, iwe ni volunteering, contract au permanent, nk).
Best students tupo tu mtaani tunapambana na hali zetu. Nadhani kwa hali hii, GPA za wanafunzi zitaanza kushuka (kwani siku hizi continuing students wanatuona sisi graduates wengi tuna 3.8+ GPAs lakini hazina maana kwani ajira serikalini adimu na hata tukiitwa kutoboa ni ngumu sana). Tunapoelekea sasa tutaanza kuwa kama Nigeria (vyuo vyingi, students wengi, graduates wengi ila ajira chache sana).
 
Vijana mjiajiri, mkumbuke hata hivyo vyuo ni mali za watu
Dada ungefaa sana uwe Assistant Lecturer chuoni. Haiwezekani nafasi zinakuwa re-advertised hadi mara 3 halafu watu kama nyie hamna mpango kabisa hata kuja ku'apply huko mbeleni. Endelea kufanya biashara zako na kuwaajiri watu ila nafasi za chuoni zikitokea sio vibaya ku'apply.
Vyuo ni mali za watu lakini watu hao hawafanyi jitihada zozote kubadilisha sera na mifumo iliyopo sasa. Watu kama nyie mkiingia huko mnaweza mkafanyika chachu ya kuleta mabadiliko halisi ndani ya miaka michache.

Vijana tunawahitaji, mkumbuke hata hivyo baadhi ya watoto wenu au wa ndugu zenu wanategemea kupata ajira vyuoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…