Kenya 2022 Uchaguzi wa Kenya ulianza vizuri ni nini kimeusibu?

Kenya 2022 General Election
Mimi ni mkenya, kama upo karibu na tv yako cheki KTN au ingia kwenye website yao. Tume ya uchaguzi tu ndio imekubaliwa kisheria kutangaza mshindi, naamini kwamba watafanya hivyo leo hii.
why opting for KTN and not citizen tv?. tunajua media zenyu haziko sawa kwenye figures. kila media ina figure zake.
 
Kwamba kwasababu anaweza kusemwa basi hata ukilala usiku ukaota ndoto mbaya asubuhi ukiamka unamlaumu Jk???
Angalia alichosema huyo jamaa, ulichoreply kwa huyo jamaa alafu linganisha na mfano wako.
 
Mie nilimuambia yule jamaa tarehe 10 August 2022 kuwa ni mapema mno kuanza kujifaragua na ngonjera za UWAZI unless uwe mgeni na chaguzi za Africa.
 
Mbona huu uchaguzi wa Kenya walianza vizuri, watu tukajua ndani ya siku Moja mbili tutamjua Rais , lakini sasa ni takribani siku ya nne mambo bado, kunani tena?
Kwa uelewa wangu ni kwamba, yale matokeo yaliyokuwa yanatangazwa na vyombo vya habari walikua wanajumlisha idadi ya kura katika kila kituo ambapo kila kituo kikimaliza kuhesabu na kupata matokeo kilikua kinatuma hiyo form ya matokeo kwy mtandao ambapo kila mtu alikua anaweza kuipata hiyo form.

Kinachoendelea sasa ni kwamba sheria inaitaka tume ipokee nakala halisi ya hiyo form iliyotumwa kwy mtandao na kujiridhisha kuwa ndio yenyewe na ijumlishe matokeo husika. Kwa kifupi zoezi linachukua muda mrefu maana form zote hizo zinatakiwa zifike zikiwa nakala halisi kwenye tume na wahakiki na kujumlisha hizo kura. Hapo ndio zoezi linachukua muda mrefu.

Vyombo vya habari nafikiri vimeacha kutangaza matokeo kwa tahadhari kwamba endapo kutakuwa na makosa basi watu watafanya rejea kwa chombo husika na hapo inaweza leta mtafaruku usio na lazima. Imani yangu ni kwamba hakutakua na urahisi wa kufanya maperekeche maana mawakala wa vyama vyote walikuwepo vituoni na pia wapo makao makuu ya tume kushuhudia kila hatua ya uhakiki na majumuisho.

Ni maoni yangu lakini kwa namna nilivyoelewa na si lazima niwe sahihi.
 
We jamaa sijui unaumwa akili au nini. Matokeo hawajatoa lkn unalazimisha kuwa RUTO ameshinda dah [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kweli ugonjwa wa vichaa upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…