Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Ni kweli wamejipanga vya kutosha na naona pia hata observers wa jumuiya ya ulaya wako hapa na kila kitu kipo sawa na kinaendela vizuri so far.



Endelea kutumwagia habari hizi Mkuu Kieleweke . Mimi nime ingia mstuni rasmi kujua mbinu mpya za Lowasa kutaka kurudi akiwa amesha safishwa na CCM yake na TVT yetu ambayo mali ya kila mtanzania .Nitasema soon .
 
Muda sio mrefu tutaanza kupata matokeo ya baadhi ya vituo na hivyo nitajitahidi kuyaweka hapa na kuwapa taarifa za nini kinaendelea.
 
Muda sio mrefu tutaanza kupata matokeo ya baadhi ya vituo na hivyo nitajitahidi kuyaweka hapa na kuwapa taarifa za nini kinaendelea.

Tunatanguliza shukrani kwa kazi ngumu, tupo hapa tuna subiria yatakayojili huko....nadhani uchaguzi umekuwa huru na amani hakukuwa na matukio ya ajabu....
 
Zoezi zima limefanyika kwa amani hadi sasa ambapo zoezi la kufunga vituo vya kupigia kura hivyo hakuna vurugu zozote ambazo zimeripotiwa hadi kipindi hiki .
 
Tumekaa mkao wa kula sasa .Yetu macho hapa JF na masikio Kiteto
 
Kiteto kuweka historia leo

na Joseph Zablon
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAKATI uchaguzi mdogo wa mbunge wa Kiteto unafanyika leo, mji wa Kiteto na vitongoji vyake jana ulikuwa katika heka heka kubwa kutokana na shamrashamra za wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufunika za wapinzani wao, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hali hiyo iliibuka baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwisho wa kampeni za uchaguzi za Chadema zilizohitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Hali katika mitaa mbalimbali ya mji wa Kiteto ilikuwa ya uchangamfu mkubwa kwa wafuasi wa Chadema ambao baada ya kumalizika kwa mkutano huo walianza kuandamana kumsindikiza Mwenyekiti wao, Mbowe pamoja na Mgombea wa chama hicho Victor Kimesera waliokuwa katika gari moja.

Wakati wafuasi wa Chadema wakiandama kumsindikiza mgombea na mwenyekiti wao, wenzao wa CCM walikuwa wamesimama pembeni mwa barabara wakiwaangalia kwa namna ya kuwashangaa.

Hekaheka za maandamano hayo zilianza baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kumtangaza mgombea ubunge kupitia chama hicho, Victor Kimesera, mbele ya mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, umati wa wafuasi wa CHADEMA pamoja na wakazi wengine wa mji huo waliohudhuria mkutano huo, walianza kulisukuma gari lililokuwa limembeba Mbowe na Kimesera hadi hosteli za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ambako viongozi hao wamefikia.

Awali akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi huo, Mbowe alisema wakati umefika kwa wananchi wa Kiteto kupigana na umaskini na kuachana na ushabiki wa vyama kwa vile CCM kimekuwa chama cha matajiri walioko Dar es Salaam na katika miji mingine mikubwa.

“Kwa maana hiyo nawaomba wananchi wa Kiteto kutumia nafasi yenu kesho (leo) kufanya mapinduzi katika maisha yenu, kuchagua upinzani kupitia mgombea wetu Kimesera,”alisema Mbowe.

Alisema katika kipindi cha miaka 46 tangu Tanzania ilipopata uhuru, kipindi ambacho CCM kimekuwa madarakani, hakuna cha maana kilichofanyika kwa Watanzania wakiwemo wananchi wa Kiteto.

Kwamba vijana wengi waliozaliwa wakati Tanzania inapata uhuru walizaliwa katika maisha duni, wamekulia katika maisha duni na sasa wakiwa katika umri wa utu uzima bado wanaishi maisha duni.

Alisema sehemu nyingi za taifa hili hazina huduma muhimu na za msingi kama vile zahanati, barabara za kuaminika na shule za maana kwa ajili ya watoto.

“CCM ina wenyewe, ni wale wanaoishi Oysterbay, Masaki na Mikocheni na si ninyi mlioko huku vijijini, mmekuwa mkitumiwa kwa ajili ya kupiga kura,” alisema.

Mbowe ambaye jana alitumia tena helikopta baada ya juzi kushindwa kuitumia kutokana na kupata hitilafu aliweza kumnadi Kimesera katika kata nane za mji wa Kiteto ambazo ni Dodosi, Songambele, Olgune, Ongasero, Matuli, Naniroki, Njolo, Narangitomoni na Kibaya.

Kabla ya Chadema kufanya mkutano huo, CCM ilifanya mkutano wake wa kuhitimisha kampeni kaktika Shule ya Msingi Kibaya.

Katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alimnadi kwa mara ya mwisho mgombea wa chama hicho, Benedict ole Nyangolo, kwa kuwataka wapiga kura wa jimbo hilo kumpigia kura za ndiyo.

Msekwa aliwataka wana Kiteto kutochagua mgombea mwingine kwa sababu hawezi kuwaletea maendeleo. Katika mkutano huo, kikundi cha Tanzania One Theatre kilitumbuiza.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa Jimbo la Kiteto, Feston Kamombe, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba zoezi la kupiga kura litaanza saa moja asubuhi leo.

Kabla ya kufanyika uchaguzi huo leo, kumekuwa na matukio mbalimbali yasiyo ya kawaida ya kupigwa kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema na kundi la watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM.

Kufuatia vitendo hivyo, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi katika sehemu zote za Kiteto.
 
ndugu zetu jiandaeni kufuta machozi, na kutoa sababu za kushindwa maana yote tisa kumi ccm inarejesha kiti chake leo

Ikirejesha ndiyo maana ya ushindani .Lakini zengwe la huko limekuwa kubwa sana .Wanaweza kukupata lakini pia mengi yamefanywa na CCM na Serikali .
 
Mgombea CHADEMA aongoza Kiteto

UCHAGUZI mdogo wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Kiteto mkoani Manyara umefanyika jana huku mamia ya wapiga kura wakiendelea kubaki vituoni kusubiri majibu na kudhibiti udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.

Wakati tukienda mitamboni jana jioni mgombea wa CHADEMA Bw, Victor Kimesera alikuwa anangoza katika kituo cha Kibaya Mjini kwa kupata kura 573 dhidi ya mpinzani wake kutoka CCM Bw. Benedict Ole Nyangolo aliyepata kura 202.

Wagombea wengine wa SAU, Bw. Mashaka Fundi alipata kura 3 na mwenzake Bw. Juma Ali wa PTT Maendeleo alipata kura moja.

source:
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=5791
 
Haya wazee muliokuwepo Kiteto tunaomba mutu-update

Wenye data za matokeo tunaomba mutuwekee
 
Mods naomba hii iconnect na ile thread ya "Uchaguzi wa Kiteto" samahani kwa usumbufu
 
CCM wanaelekea kushinda japo kwa tofauti ndogo kama hakutakua na muujiza wowote katika maeneo machache yaliyosalia. Nadhani huu ni wakati ambao Chadema wamefanya mazoezi ya kulichukua hilo jimbo 2010 kwani CCM wakati huo kila mtu atakua anatetea jimbo lake na si wote kuhamia Kiteto. TATIZO KUBWA (SIJUI KWANINI) zaidi ya nusu ya wapiga kura hawajajitokeza kupiga kura na zaidi katika maeneo ambayo mgombea wa CHADEMA ana wafuasi wengi. Inawezekana ilikua ni mkakati maalumu wa CCM na hapo ndipo wapinzani wanapopata fundisho la kujiandaa kwa mikakati na si mambo ya "mbwembwe". CCM wanaangalia wapi ulipopasahau na hapo ndio watapita, hawana njia moja ya kupata ushindi. Wakikosa katika kampeni za kawaida watakumaliza kampeni za kimkakati, wana timu na wataalamu wa kila fani wakiwamo wanaolipwa fedha za walipa kodi (watumishi wa serikali). Tuna safari ndefu ya kutokea mabadiliko katika nchi hii.

HIVI KWA HALI YA SASA CCM ILIYOSAMBARATIKA NA KUCHAFUKA WAPINZANI WANASHINDWA!!!!!????
 
CCM wanaelekea kushinda japo kwa tofauti ndogo kama hakutakua na muujiza wowote katika maeneo machache yaliyosalia. Nadhani huu ni wakati ambao Chadema wamefanya mazoezi ya kulichukua hilo jimbo 2010 kwani CCM wakati huo kila mtu atakua anatetea jimbo lake na si wote kuhamia Kiteto. TATIZO KUBWA (SIJUI KWANINI) zaidi ya nusu ya wapiga kura hawajajitokeza kupiga kura na zaidi katika maeneo ambayo mgombea wa CHADEMA ana wafuasi wengi. Inawezekana ilikua ni mkakati maalumu wa CCM na hapo ndipo wapinzani wanapopata fundisho la kujiandaa kwa mikakati na si mambo ya "mbwembwe". CCM wanaangalia wapi ulipopasahau na hapo ndio watapita, hawana njia moja ya kupata ushindi. Wakikosa katika kampeni za kawaida watakumaliza kampeni za kimkakati, wana timu na wataalamu wa kila fani wakiwamo wanaolipwa fedha za walipa kodi (watumishi wa serikali). Tuna safari ndefu ya kutokea mabadiliko katika nchi hii.

HIVI KWA HALI YA SASA CCM ILIYOSAMBARATIKA NA KUCHAFUKA WAPINZANI WANASHINDWA!!!!!????


wakiwa wametukosa muda huu tukiwa majeruhi wasahau huko mbele
 
Ahsante Halisi,

Tutaomba more updates za matokeo kama unavyoyapata!

Kaka Ahsante na wewe. Inabidi nilale maana saa hizi, ni kulala kwa dakika chache si saa chache. Hayo ni matokeo ya saa 7.15 (01.15hrs) ambako CCM walikua wakiongoza kwa tofauti ya kura takriban 2000, lakini kasi ya Chadema ilikua kubwa kwani saa 6.06(00.06) CCM walikua wakiongoza kwa tofauti ya kura 4,000 ambazo baada ya saa moja za Chadema ziliongezeka. Lakini wakati huo sehemu kubwa walikua wamekwisha kuhesabu. Kuna UKIUKWAJI mkubwa wa taratibu katika uchaguzi huo na kwa hali ilivyo KAMA CCM watashinda itakua ni ushindi wa AIBU. Kwa idadi kubwa ya wabunge walionao hawakua na sababu ya kufanya yaliyotokea Kiteto, pamoja na kuwa ni MKAKATI WA kuzuia UPEPO wa MABADILIKO.
 
Hakuna mwenye data mpya wakulu?

mpya zilizopo kuwa chadema wameangukia pua.

tunatanguliza pole zetu kwa ndugu zetu na wamejitahidi sana ila ndio hivyo bado ni wachanga mno.

wache wajipange zaidi huenda baada ya miaka 20 wanaweza kuaminila alau kupata baadhi ya majimbo.


sasa uchaguzi umeisha tushirikiane ktk kuijenga kiteto na tanzania
 
mpya zilizopo kuwa chadema wameangukia pua.

tunatanguliza pole zetu kwa ndugu zetu na wamejitahidi sana ila ndio hivyo bado ni wachanga mno.

wache wajipange zaidi huenda baada ya miaka 20 wanaweza kuaminila alau kupata baadhi ya majimbo.


sasa uchaguzi umeisha tushirikiane ktk kuijenga kiteto na tanzania

Mbona hujazimwaga data hizo kama BREAKING NEWS?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom