UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

Eeh!! Swala ni watu wanaondaliwa katika mazingira tofauti na kuja kufanya mtihani mmoja sio sawa.

Mkenda huwezi kumlaumu kwani yeye ndo hawezi kufanya reforms za haraka katika elimu ni taratibu kaanza na hilo .
 
Haswaa.
Nimekuelewa vyema na umeelewa vyema mada yangu hapa.
 
we kinachokusumbua ni nini mpaka povu lote hili. Inaonekana una maslahi flani mmezoea mbeleko. Iacheni taasisi iamue inavyoona inafaa, tukijua wa wanafunzi bora 10 kati ya wanafunzi laki 5 inatusaidia nini. Kuja shule bora 10 kuna ligi? Matokeo yako kwenye mtandao fuatilia matokeo ya shule ambazo una-interest nazo msiingize taasisi ya serikali ktk maslahi yenu. Kwangu mimi wamechelewa sana kufuta upuuzi ule
 
Eeh!! Swala ni watu wanaondaliwa katika mazingira tofauti na kuja kufanya mtihani mmoja sio sawa.

Mkenda huwezi kumlaumu kwani yeye ndo hawezi kufanya reforms za haraka katika elimu ni taratibu kaanza na hilo .
Ndio maana sisi tumewakosoa NECTA kwa kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora huku wakija na hoja dhaifu mnoo.

Huwezi kusema mchuzi wa nguruwe ni haramu halafu hapo hapo useme nguruwe ni halali.
 
Bado unazunguka hujaelewa hoja za mtoa mada,,,kwanini wapimwe kwa mtihani mmoja angali mazingira ni tofauti??
 
Rudi usome tena hoja zangu kisha uzichambue, mambo yangu binafsi huyajui na hata ukiyajua hayatakusaidia.
 
Bado unazunguka hujaelewa hoja za mtoa mada,,,kwanini wapimwe kwa mtihani mmoja angali mazingira ni tofauti??
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
 
Ndio maana sisi tumewakosoa NECTA kwa kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora huku wakija na hoja dhaifu mnoo.

Huwezi kusema mchuzi wa nguruwe ni haramu halafu hapo hapo useme nguruwe ni halali.
Ndo maana wamtenga hawawezi kuwachanganya wanajitambua sasa
 
Umetumwa na hizo shule zinazochuja wanafunzi ili mradi tu zionekane ziko vizuri MPUUZI mkubwa wewe KIMA
 
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
Mkuu umeyaona matokeo na kuyachambua?
Walichokifanya NECTA ni kutupa matokeo yote halafu sisi wenyewe tuyape ubora!! Tukipotosha?
Logic iko wapi?
 
Enzi zetu waliokosa nafasi Shule za Serikali walikwenda Private kama Sangu, Highland etc. Hizi mbwembwe za kutangaza results kwenye Makamera hazikuwepo.
Kabisa ,ni ujuha eti kulinganisaha shule za feza na shule zetu ambazo hazina utamaduni wa kuchuka wanafunzi .Pale feza wakiona huwezi pata division one wanakuhamishia feza international
 
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
Kama huwezi kuziweka shule zote sawa katika upangaji ubora, ni vipi uzitungie mtihani mmoja, usahishe na kuzipa alama katika viwango sawa?
 
Zote zinazoshika top ten ni zile za St na nyinginezo tofauti na za vidumu. Sasa za kule atokapo ndiyo zinakuwa mkiani kabisa. Uzuri mmoja awamu hii ikimalizika tutarudi kwenye ushindani wa hizi shule kama kawaida. Leo nimechungulia shule za kibabe na matokeo kabisa yaonesha ndiyo top ten wao hata kama hazijatangazwa. Hivyo awamu hii wajiangalie Sana kwenye eneo le Elimu bara maana shule za kikrisro ndiyo zinaongoza zikifuatiwa na zinazomilikiwa na Trustees. Wivu huo waache. Mjukuu wangu shule ya Katoliki wako 138 wote ni Div I za single digits na chache Sana double digits. Mmoja wao amepata 3 alikuwa na matatizo ya kiafya toka form One. Ninashukuru Mafather hawakumuondoa wakapambama naye mpaka amepata 3. Halafu MTU anaacha kuzipambanisha kisa eti mazingira tofauti. Ñao waboreshe mazingira yao. Pesa ya kujengea tu madarasa wanatafuna, madawati wanatafuna, vyoo wanatafuna wanajenga uchichoro wa Choo. Yaani ni aibu Sana.
 
Ukitaka kujua ubora wa skuli uitakayo kila matokeo yakitoka fanya kutafuta mwenyewe siyo serikali ikuwekee ubaoni na kukutangazia skuli yako.

Wewe amka na walimu wako fanyeni recruit search alafu iteni media zote pigeni ukunga.
 
Kwa mantiki yake, Je ni sahihi kutunga mtihani mmoja wa kumpima mwanafunzi wa Feza na Kata?
Ni sahihi ,duniani kote hakuna mitihani tofauti kwa ngazi sawa ya kidato ila kulinganisha shule inayochu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…