UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

Wizara hi inaongoza kuaribu hatma za wanafunzi

Kila waziri huwa anakuja na lake kuanzia enzi za mugwai ,mam sita , professor ndalichako ,na SAS huyu wa SAS bwna mkenda ,

Itafika wakti watakuja tu na lingine haswa kwenye mitaala
 
Hakuna haja ya kuwapa mtihani sawa wanafunzi ambao mazingira ya shule, uwezo wao wa uelewa, uwezo wa familia wanazotoka kiuchumi, kiimani, n.k. ni tofauti. Wafute na mitihani shuleni. 😁
 
[emoji4]
 
Hoja zao hazijabeba logic yoyote zaidi wanatufanya tuamini kuna chuki binafsi tu inayoendelea zidi ya shule binafsi.
Halafu preliminary analysis yangu inanionesha kuwa kuna watu wa DINI A WANAFURAHIA MAAUMUZI YA NECTA KUTOWEKA RANKINGS NA DINI B WANAHOJI SANA MAAMUZI YA NECTA ... NGOJA NITENGENEZE HYPOTHESIS
 
Hiki ulichoandika ndiyo sababu kubwa na ya msingi iliyopelekea walioongoza na waliokuwa wamwisho kutotangazwa.
 
Naungana na wewe 100% naona umepiga kwenye mshono.....
 
NECTA, wangetumia hya matokeo kama njia ya kutafuta suluhu kwa Shule za Serikali, yaani ni sababu zipi zinapelekea Shule za Serikali kufanya vibaya. Mfano; 2.upungufu wa walimu(siasa imeshaingilia kati hili suala kiongozi). 2.Vifaa vya kujifunzia yaani vitabu n.k,
3.makazi ya walimu. licha ya walimu kuwa ni wachache, hawakai jirani na maeneo ya kazi kutokana uhaba wa Nyumba.
4. Masilahi duni. Mishahara ya walimu ni kidogo hii hupelekea walimu kufanya kazi kwa ufanisi mdogo.
Hivyo: necta ingetumia haya matokea kuboresha/kurekebisha mapungufu yalioko kwenye Shule za public na sio kuogopa kutoa matokea kwa ranking za Shule.
 
Hivi developed country huwa Zina asses vipi matokeo any one with experience
 
Ndo maana huwezi kuwaweka sawa katika kupanga list ,ndo kafuta ni hatua na tangu mwanzo walikuwa wanajua kwamba hawatokuwa sawa Kwa zile wanasoma mazingira tofauti
Kwanini wasingetungiwa mitihani tofauti kama issue ni mazingira kutofanana? Kama issue ni mazingira basi wangezitenga kulingana na mazingira wwkatangaza top ten kwa kila kundi mfano private school, government special school na hizi nyingine
 
Kwanini wasingetungiwa mitihani tofauti kama issue ni mazingira kutofanana? Kama issue ni mazingira basi wangezitenga kulingana na mazingira wwkatangaza top ten kwa kila kundi mfano private school, government special school na hizi nyingine
Labda wawatungie tofauti angalau.
 
Wapo sahihi... Top 10 inakusaidia nini wewe mlalahoi, huwezi kupeleka watoto wako Feza boys, wakati hata michango tu ya shule ya kata huwezi kutoa
 
Ila Tanzania tunaburuzwaa haswaa, haya mambo ya kubadirishiwa utaratbu kwa hoja hoja dhaifu ni kukoseana Adabu sana
 
Wizara hi inaongoza kuaribu hatma za wanafunzi

Kila waziri huwa anakuja na lake kuanzia enzi za mugwai ,mam sita , professor ndalichako ,na SAS huyu wa SAS bwna mkenda ,

Itafika wakti watakuja tu na lingine haswa kwenye mitaala
Nyie hamjui yaliyoko katika shule za private waulizeni walimu watawaambia yanayotendeka huko
Watoto weny wanatunika kuingia pesa lakini hawapati kile kinachotakiwa zaidi ya kukariri
1. Umeshawahi kuona syllabus ya mwaka mzima inamalizwa kufundishwa kwa miezi mitatu
Kwa madai ya kufanya revision miezi iliyobaki
Na hyo revision ni kukaririsha naswaki ya nyuma yaliyowahi kutolewa na baraza la mitihani .Sasa ulimoeleka mtoto shule akafanye revision na kujibu maswaoi au apate Maarifa yatakoyomsaidia katika maisha yake ya baadae

2 njia za ufundishaji za kumshurikisha mwanafunzi hazipo
Ndio maana ya kupata product isiyoweza kujitegemea kwa chochote
.application ya kile wanachofundishwa hakuna katika maisha Yao kabisa
Watoto wanatoka wa A lakini hakuna kitu WANAWEZA wakati syllabus yetu ikifuatwa vizuri na njia za ufundishaji zinazotakiwa mbona mtoto anaweza kumaliza form four na akawa
Fundi umeme
Fundi fridge nk

3. Wizi wa mitihani , angalia walimu wanavyooambana kuwapa majibu watoto .hiyo yote ni kwa sababu ya kuhakikisha kuwa shule yake inafanya vizuri unapata wanafunzi wengi
Wakuu wa shule pamoja na walimu wanapambana kwa njia yoyote Ile kuhakikisha wanawapa majibu watoto
Mitihani hii walimu wanapambana kutoa mitihani kwa watoto ilimradi tu shule yake ionekane imefaulu
Angalia primary schools walimu wanashikwa choini wanatoa majibu kwa watoto
.binafsi nashukuru sana kwa maamuzi ya baraza la mitihani
Kabla ya kuandika chochote fanta utafiti huko mashuleni
Mimi nimeacha kufundisha private school mwaka Jana lakini nimefanya kazi huko kw miaka kumi najua sana
 
Kwanini wasingetungiwa mitihani tofauti kama issue ni mazingira kutofanana? Kama issue ni mazingira basi wangezitenga kulingana na mazingira wwkatangaza top ten kwa kila kundi mfano private school, government special school na hizi nyingine
Hoja ya mazingira ni ya kipuuzi, kuna mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya kata na hata wanafunzi wengi kutoka familia maskini huwa wanaongoza kama best students...........hawa mbona mazingira hayajawaathiri? hapa kinachofichwa ni shule za upande uleee kuonekana kuwa na ufaulu hafifu miaka nenda rudi.​
 
Hivi ndivyo walivyofanya NECTA. Kama kuna uchambuzi unaweza kufanywa lkn NECTA wamejitoa. Uchambuzi wowote utakuwa sahihi ikiwa utafuata vigezo. Sioni tatizo hapo.
 
Ilichokifanya serikali ni kana kwamba haitaki ushindani na kwa lugha ingine ni kwamba imekataa kujifunza. Hakuna maajabu yeyote zaidi ya kuweka walimu competent kwenye shule za kata na kuwa finance vizuri. Watoto watafaulu tu, mbona Kibaha inafaulisha, ilboru kama kawaida.

Kuna mahali serikali inafanya uzembe na dawa sio kuficha ukweli kwamba inafanya uzembe. Wekeni walimu bora na muwalipe vizuri muone kama wanafunzi hawatafanya vizuri. Shule haina vyoo walimu wana lindi la madeni mtaani sababu mshahara finyu unategemea elimu inakuwaje bora. Mwalimu hana utulivu wa akili kwanini asimalizie hasira kwa mwanafunzi kumpiga stiki za visigino.

Wenzenu private wanalipa 1.5 to 2M na wanahakikisha bonus zipo kwa matokeo mazuri zaidi. Utakosaje motisha wakati unajua ukizalisha A's swala la uongozi wa shule kukuzawadia gari na hela ni jambo la kawaida.
 
Unataka watangaze shule bora na wanafunzi bora hao wanafunzi bora wakimaliza elimu zao ajira utawapa wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…