Amani iwe nanyi Wadau.
kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.
Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020...