Uchambuzi: Kwanini Israel hawezi shindwa vita mashariki ya kati?

Siku yaja Warabu wataungana na Kisha kumtolea uvivu Israel, hata USA akiingilia kati haitasaidia kitu.
 
Muhammed ndie aliwaunganishwa Waarabu wakapigana wakiwa One force na kushawishiwa na Dini yao Mpya wakati huo ndio walishinda Vita kadhaa na mpaka leo huwa wanahadithiana their past glory.

Baada ya hapo Mwarabu hajawahi kushinda Vita yoyote zaidi ya kupokea kipigo.
 
We jamaa; na zile ndege za kivita zilizo pigwa na kuteketezwa uwanjani kabla hazijaruka nayo utasema propaganda? Rais aliyeuawa na aliyekuja baadae nani alikua pro 🇺🇸 USA? Bora ungenambia kwamba Israeli bila msaada wa USA haiwezi pekee yake kuliko hi propaganda ulioandika hapa
 
Israhehell ni sapot tu ya mabwana zake hana ajabu lolote
 
Mbona unaongea kinafiki ndugu unageuza geuza maneno embu elezea vizuri na kiukweli ile vita ya omkipuri ni Misri aliomba mwishoni Marekani amshawishi israel asikilimalizie kikosi cha 3 maana israel alibakiza km 112 afike cairo
Ndo propaganda zenyewe ninazoziongelea, kuna Academic source yoyote ile inayosuport Hili? Sababu kuna vitabu vingi na Historia nyingi kwamba Sharon (huyo ambae wanasema alikaribia kuteka Cairo) alipigwa vibaya mno na kushindwa kuteka Ismailia na Jeshi jengine la Israel lililokuwa linaenda Suez kuwa Massacred.

Pia outcome za vita
1. Israel Alikubali kurudi Sha Sinai
2. Golda kajiuzulu
3. Waziri wa Ulinzi kajiuzulu.

Unashindaje vita halafu utoe eneo unaloshikilia? Unashindaje vita Na viongozi wako wote wa juu wanajiuzulu?




Maneno ya General wao mwenyewe

David Elazar said: “We could not along ten days of fighting to overcome any of Egyptian armies. The second army resisted and prevented us ultimately to reach Ismailia city. As for the third army, in spite of our encircling them they resisted and advanced to occupy in fact a wider area of land at the east. Thus, we can not say that we defeated or conquered them.”

Kuna Details nyingi za hii Vita zipo kwenye Vitabu ukisoma, ila media za kawaida ni mwendo wa Propaganda tu.
Hebu Soma na wewe uelewe, hata google tu kidogo ujue Yom kipur war ni nini maana unachanganya madesa
 
Hakuna chochote kilichoandikwa hapo kinachopinga mimi nilichoandika, hapo imeelezewa tu kijuu juu.

David Elazar said: “We could not along ten days of fighting to overcome any of Egyptian armies. The second army resisted and prevented us ultimately to reach Ismailia city. As for the third army, in spite of our encircling them they resisted and advanced to occupy in fact a wider area of land at the east. Thus, we can not say that we defeated or conquered them.”

Hio Statement ya General wa Israel mwenyewe unaweza kuipinga kwa Evidence?

Hio vita ya Suez Iliofanyika 24-25 ndio ilikua vita ya mwisho kwenye Yom Kipur Israel walivamia Suez na kupigwa Vibaya Mno


So mkuu Israel wameshinda Yom kipur kwenye media tena miaka ya Karibuni, watu waliokua Hai muda huo wote wanajua walipigwa.
 

Blame others everything but yourselves.
 
Usisahau inapata support ya fedha na silaha kutoka US na nchi za Magharibi.
Usitoke nje ya mada. Katika vita kila nchi husaidiwa na mshirika wake.


Hata hamas na hizbolah wanasaidiwa na Iran. Wasaidiwe au wasisaidiwe haiondoi ukweli huu ulioandikwa na anti-Israeli.
 
Mkuu umetoa hoja KISHABIKI zaidi nakujificha kwenye kichaka cha Ant- Israel

Ipo hivi...... ISRAEL HAIPIGANI VITA NA NCHI YOYOTE KWA SASA.

Kilichopo ni kwa kwamba Israel imewakalia kimabavu Wapalestina na kuna baadhi ya vikundi vya kiislam vikiungwa mkono na Iran vinajaribu kuwatetea kupigania haki za wapalestina
 
waarabu wao si wanapatia urusi?
kumbuka urusi nae yupo katika vita hivyo sio rahisi na yeye kutoa msaada mkubwa kwa mkupuo kwa washirika wake pia kumbuka nchi yeyote inayoonekana inaunagna kijeshi na uruisi nchi za mgharaibi mara moja humuwekea vikwazo hivyo nichi nyingi zinaogopa kuonyesha ushirikiaono wao dhahir
 
Kiongozi umeeleza vema sana....ambaye hajaelewa hataelewa Tena...ukiangalia strategicaly hata vita vya Gaza utagundua hamas Wana rocket tu..na mibomu ya kutega ardhini...hata ndege moja tu ya kivita hawana
by the way,roketi ni kwa ajili ya kupiga short range na ndizo hizi vikundi vinavyo nyingi sana ila makombora wanayo lakini sio mengi sana wakati makombora ndio muhimu sana kwa kuwa yana akili kwa maana huwekwa chip na kuwa guided yaende kutua au kupiga wapi na spidi yake ni kali mara nyingine air defense system hushindwa kuzitungua lakini roketi zenyewe hazina akili na ni rahisi kutunguliwa na ADS.
 
Elewa kwamba bila mkataba wa Camp David Sinai isingerejeshwa kwa Misri na hilo liko wazi.
 
Elewa kwamba bila mkataba wa Camp David Sinai isingerejeshwa kwa Misri na hilo liko wazi.
Kuanzia 1967 mpaka 1973 hakuna mwaka hata mmoja ambao Egpty hajamwambia Israel arudishe hilo eneo na kila mwaka Israel walikataa, hivyo Egpty aka force na kuanzisha hivyo vita. Baada ya kuona Maji ya Shingo ndio Usa akaingilia na kuweka huo mkataba, so Angeshinda Israel hivyo vita angeendelea na msimamo ule ule kukataa kurudi Sha Eneo la Egpty, ila sababu alipigwa ilibidi akubali kurudisha hilo eneo.

Kabla ya Vita kuanza objective ni kurudisha eneo lao, baada ya Vita kuisha Egpty kapewa eneo lake, sijui kitu gani kigumu hapa kwako kuelewa.
 
SAWA kwa ufafanuzi mkuu
 
Alishawahi kuchangiwa na mataifa 22 ya kiarabu mwaka 1967 akawapiga kwa siku 6 na mwaka 1973 misri na syria ziliingia vita vya ommukipuri na israel akapigana na nchi mbili kwenye uwanja wa vita na kuibuka mshindi sasa hayo nayo ni makundi?
Kwa propaganda tunazoziona saivi .,wazan zaman hazikuepo?
Afazal saiv technology imeongezeka kila kitu tunajionea
 
Sitaki kuamini kwamba wewe ni mjinga ila naamini kwamba udini ndio unakusumbua.

Masharti makubwa mawili ya Misri kurejeshewa jangwa la Sinai yalikuwa ni:-

1. Misri waitambue taifa la Israel na watambue haki ya kuwepo kwa taifa hilo.
2. Misri kuacha vitendo vyote vya uhasama dhidi ya taifa la Israel.

Baada ya aliyekuwa rais wa Misri marehemu Anuar Sadat kukubali na kusain mkataba huo ndipo Israel ilipowarejeshea Sinai na kupelekea mataifa hayo kuanzisha uhusiano wa kibalozi.

Endapo Sadat asingesain huo mkataba basi hadi leo Sinai ingekuwa mikononi mwa Israel kama Golan ilivyo mikononi mwa Israel hadi leo baada ya Syria kukataa kufanya mazungumzo ya amani.

Hivyo acha upotoshaji, Camp David Accords imesainiwa mwaka 1979 mimi nikiwa form two na nilikuwa nikiifuatilia sana hivyo huwezi kunidanganya kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…