Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam


Mungu hana nafsi 3 ,hayo ni makosa

 

 
Maalim ISSA wenu aliezaliwa chini ya mtende atakuwa ndio alikuwa nabii wenu wa mwisho,,,,,Hakuna mahali popote pale ambapo YESU KRISTO aliwahi kuwa nabii,,,Wala sicho alichokijia....Usichanganye maandiko ya kiislam na Ukristo,,,Utaendelea kufeli
 
Wewe huna uwezo wa kunifundisha Mimi ukristo,,,labda uwafundishe waislam wenzio,,, maelezo Yako na hoja zako unapotumia biblia unakuwa kama mtoto wa madrasa.Yako anticlockwise,,,na yamekaa shalow.
 
Robert Heriel
Unapoandika andiko muhimu kama hili jikite kwenye research kabla hujaandika.
Usiandike kwa hisia.

1. Sio kweli kuwa Dini ya Ukristo na uislam asili di dini ya kiyahudi.

2. Ibrahimu hajawahi kuwa Myahudi.

3. Ibrahimu, Isaka na Yakobo walikuwa Waebrania

4. Tatizo utakuja na ubishi mwingii tafuta hicho kitabu
 
Maalim ISSA wenu aliezaliwa chini ya mtende atakuwa ndio alikuwa nabii wenu wa mwisho,,,,,Hakuna mahali popote pale ambapo YESU KRISTO aliwahi kuwa nabii,,,Wala sicho alichokijia....Usichanganye maandiko ya kiislam na Ukristo,,,Utaendelea kufeli

Kuna aya nyingi katika Agano Jipya zinazounga mkono utume/unabii wa Yesu.

Zifuatazo ni aya chache tu miongoni mwa aya hizo:

katika Mathayo 21:11, watu wa zama za Yesu wamerekodiwa wakimchukulia Yesu kuwa ni mtume:

“Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.”

Katika Marko, 6:4,

imeelezwa kuwa Yesu amejitaja yeye mwenyewe kuwa ni mtume:

“Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, ispokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani kwake.”

Katika aya zifuatazo, Yesu anachukuliwa kuwa ametumwa akiwa ni mjumbe.

Katika Mathayo 10:40, imedaiwa Yesu amesema kuwa:

“Awapokee ninyi, anipokee mimi, naye anipokeaye mimi, ampokea aliyenituma.”

Katika Yohana 17:3, pia, Yesu alinukuliwa akisema: “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
 
Nachojua, El alikua mungu wa caanan, Abraham amekuja caanan ndipo akaanza kuabudu mungu wa caanan,, Abraham siyo myahudi wala hajawahi kuabudu dini ya kiyahudi, dini ya kiyahudi imeanza baada ya waisrael kurudishwa toka utumwani babel na mfalme wa persia, cyrus,, ambae ndie aliwajengea hekalu na kutuma waalimu kuwafundisha dini,
Moses siyo mwanzilishi wa dini ya kiyahudi,, dini ya kiyahudi inaabudu mungu tofauti na El,, wao wanaabudi yahwew,,
Moses alupikimbilia jeddah baada ya kumuua mtumishi wa farao,, alikwenda akajiunga na dini iliyokua ikiabudiwa na wa medianite aliejulikana kama yahwew,,
Hawa wa median ni uzao wa mke wa tatu wa Abraham aliekua akiitwa , Kedari,
Baba mkwe wa moses ndiyo aliembatiza moses kufuata imani ya wa median,
Uyahudi ni dini iliyoibuka kwa kuchanganya imani mbalimbali za kijadi za mesopotamia
 
Wewe huna uwezo wa kunifundisha Mimi ukristo,,,labda uwafundishe waislam wenzio,,, maelezo Yako na hoja zako unapotumia biblia unakuwa kama mtoto wa madrasa.Yako anticlockwise,,,na yamekaa shalow.

Mimi sikufundishi dini nakuwekea ushahidi wa biblia unaweza kukubali au kukataa hiyo ni hiari yako lakini biblia ndivyo inavyotuambia
 
Myahudi kwa imani yao anaweza kuingia msikitini lakini siyo kanisani,, Netanyahu huwezi muona anatia mguu kanisani,, kiimani yao wayahudi wanaamini wakristo huabudu sanamu,,
Sasa cha ajabu hata wao wanaaendaga kusali kwenye mabaki ya ukuta wa kambi ya jeshi la mkoloni wa kirumi..
 
Maalim ISSA wenu aliezaliwa chini ya mtende atakuwa ndio alikuwa nabii wenu wa mwisho,,,,,Hakuna mahali popote pale ambapo YESU KRISTO aliwahi kuwa nabii,,,Wala sicho alichokijia....Usichanganye maandiko ya kiislam na Ukristo,,,Utaendelea kufeli

Biblia inaeleza vizuri sana kwamba:

Akajibu, akasema sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).

2. Na uzima wa milele ndiyo huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. (Yohana 17:3).

3. ... bali yeye ndiye aliyenituma. (Yohana 8:42).

4. ... Bali baba aliyenipeleka. (Yohana 14:24).

5. ... Wewe ndiye uliyenituma. (Yohana 17:8-14, 21-22)

6. Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe, kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo. Na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka. (Yohana 5:30, 6:38, 4:36).

Isitoshe siyo hayo tu, bali Injili zote zimejaa aya zinazoeleza kwamba Yesu ni Mtume tu.

Kwa faida zaidi ninataja hapa aya chache tu. (Mathayo 21:46, 21:11, 9:37. Marko 9:35, Luka 4:43, 24:19. Yohana 13:20, 12:44-50, 7:16-17, 6:44, 7:28-33, 8:16- 18, 26-29, 9:4,19:17, 6:14, 15:22, 16:5,17:21-25, 4:19- 24-44
 
Ongeza dawa hii

Huyo Sheikh wenu Amefanana na nyie wafuasi wa dini,,,badala ya kuuongelea uislam anapoteza TU mda wake kumuongelea Yesu,,Paulo na injili,,,huo mda sijui hua mnaupata wapi mnapoteza TU mda???

Hivi mnajua kwamba Mungu wenu Allah Subhana Wataalah ana mabinti watatu,,,Al lata,,Al uza na Al manata.??? Mbona msitumie mda wenu vizuri kuwasoma mabinti wa Mungu wenu?
 

Mwenyewe Bwana yesu alijua mipaka ya utume wake.


Kwa hiyo alisema:


1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).


2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli. “Akasema si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia m’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).


3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
(Mathayo 10:5-6).


4. Baadhi ya Wakristo mnadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe.

Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu.
Yeye amesema kwamba:


“Lakini watakapo wafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).


5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba:


“Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).


6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49. 7.


Bwana Paulo ambaye ni mpinzani na mhalifu (anti Christ) wa Bwana Yesu, baada ya kuchukia alianza mahubiri nje ya Wasiraeli.


Biblia inasema kwamba:


“Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na bila neno, aliwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo ,walipopingana naye na kumtukana Mungu akakung'uta mavazi yake, akawaambia, damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni safi; tangu sasa ninakwenda kwa watu wa mataifa. (Matendo 18:5-6).


Baadhi ya Wakristo mnayo shauku ya kugonganisha aya za Biblia. mnasema kwamba Bwana Yesu aliagiza kwamba
“Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” (Mathayo 28:19).


1. Najibu kwamba aya hii inapinga maagizo yote ya Bwana Yesu yaliyotajwa juu. Kwahiyo haiwezi kuwa agizo la Yesu wala aya ya Injili.


2. Ya pili aya hii imeandikwa mwishoni mwa Injili ya Mathayo, na nitathibitisha baadaye kidogo kwamba aya za mwanzo na za mwisho za kila kitabu ni za kuongezwa baadaye. Aya zile siyo aya sahihi za Biblia.


3. Ya tatu katika aya 28:19 ya Mathayo neno mataifa limetumika kwa maana ya mataifa ya Israeli.
Kama Biblia inavyosema kwamba:


“Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. (Luka 2:1).


Kaisari Augusto alikuwa mtawala wa Roma tu. Hakuwa na mamlaka yoyote nje ya nchi yake juu ya ulimwengu.
Katika aya hii amri iliyotolewa kwa ajili ya ulimwengu na ya nchi ya Roma tu iliyokuwa chini ya utawala wa Kaisari wala siyo ulimwengu wote.


Hivyo ndivyo inavyoeleweka kauli ya Bwana Yesu aliposema: “Enendeni mkawafanye mataifa yote (ya Waisraeli) kuwa wanafunzi. (Mathayo 28:19).
 
Huujui ukristo mkuu na ufahamu wako hauwezi kuuelewa Ukristo,,yaani wewe ni kama ni computer ni pentium 3,,,Na ukristo ni software inataka Window 10...ndio maana ulichoandika hapa hakieleweki kabisa,,,ni vioja.
 
Huujui ukristo mkuu na ufahamu wako hauwezi kuuelewa Ukristo,,yaani wewe ni kama ni computer ni pentium 3,,,Na ukristo ni software inataka Window 10...ndio maana ulichoandika hapa hakieleweki kabisa,,,ni vioja.


John 9:17

Then they turned again to the blind man, “What have you to say about him? It was your eyes he opened.”

The man replied, “He is a prophet.”
 
Anzia hapa.
Kuna mahali uko sahihi na kuna mahali umechanya
Post yako inazua mjadala mpya.
Je tunajua maana ya NABII NA MTUME?

tukijibu hili tutajua Yesu ndiye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…