Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

"Au mnasema kuwa ibrahim na ismail na is-haqa na yaaqub na wajukuu zao walikuwa mayahudi au wakristo? waambie: je, nyinyi ndio mnajua zaidi au allah? na hakuna mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeuficha ushahidi alionao utokao kwa allah,na allah si mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya."
Qur'an 2:140


"Hakuwa ibrahim myahudi wala mkristo, lakini alikuwa mwongofu muislamu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."
Qur'an 3:67


"Enyi watu wa kitabu! kwanini mnabishana juu ya ibrahim na hali ya kuwa taurati na injili havikuteremshwa isipokuwa baada yake? basi hamzingatii?."
Qur'an 3:65


"Tizameni! nyinyi mlibishana katika yale mliyokuwa mna elimu nayo, basi kwanini mnabishana katika yale msiyokuwa na elimu nayo? na allah ndiye mjuzi na nyinyi hamjui kitu."
Qur'an 3:66


Haya ni madai ya zamani sana na ni madai mepesi na dhaifu mno ijapokuwa mwandishi atajaza kurasa nyingi kwa maandishi yasiyo na hoja wala uzito wowote, ibrahim ndiye baba wa mitume waliotumwa kwa wana wa israeli na mtume wetu pia, je alikuwa dini gani? hali ya kuwa uyahudi na ukristo havikutokea isipokuwa baada ya kutumilizwa mussa na yesu, au ibrahim alikuja baada yao? na atakuja vipi baada ya vitukuu vyake?.

Uislamu ndio dini waliokuja nayo mitume wote tangu aadam alayhi ssalaam mpaka muhammad alayhi ssalaam na ndio ujumbe pekee waliokuja nao, kuwa watu wamuabudu allah peke yake pasi na kumshirikisha na chochote na wajiepushe na kumuabudu shetani, huu ndio ujumbe wao, na hajapatapo kuja mtume yeyote na ujumbe kuwa watu wamuabudu yeye na roho mtakatifu na baba yao, ama kusema uyahudi umezaa uislamu na ukristo huku ni kuchanganya taarifa kwa ajabu kabisa.

Karibu kwa mjadala kama una malengo ya kujifunza.
 
Mkuu japo sitaki kuingilia mjadala wenu ila unapotafsiri maneno ya kiarabu ushirikishe na ubongo wako.

فالرمل هو: الإسراع في المشي مع تقارب الخطى.

hilo neno arramalu ambalo umezusha tafsiri yake hapo juu eti ni kupiga ramli basi nikufahamishe maana yake ni kufanya haraka katika mwendo kwa hatua fupi fupi, na hili mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake alilifanya kama ulivyonukuu hapo juu, kuwa alitembea haraka baina ya jiwe jeusi na jiwe jeusi kwa kama mizunguko mitatu na sio alipiga ramli, kiarabu sio kizigua mkuu hii ni lugha pana mno yenye kuhitaji misingi mizuri ya utambuzi sio unajitafsiria tafsiria tu, usifute tu comment kwa aibu wacha watu waje washuhudie aibu yako.

ama ramli imeharamishwa katika Qur'an na hadithi zake mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake, ukirudi kunijibu uje umejipanga usije kututia aibu tena.
 


Nyumba/Hekalu la MUNGU Mwenyezi katika Quran Tukufu na Biblia.


Unabii juu ya Waislamu watamsujudia MUNGU kwa njia ya Hekalu lake Takatifu. Angalia unabii wa "nitafanya" na "kuelekea":


Zaburi 138:2
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, na kulisifu jina lako kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza jina lako na neno lako kuliko vitu vyote.



Pia, njia ya Utakatifu kuelekea Makka ilitabiriwa kikamilifu katika Biblia. Huu hapa ni mfano kutoka kwa wengi kuhusu Uarabuni:



Uchakachuwaji NT ulirekodiwa miaka 200+ baada ya Yesu. Ukristo umejaa uchakachuwaji wa kanisa. Wanafunzi walikuwa na migogoro wao kwa wao. Timu za Paulo dhidi ya Peter zilikuwa zikiita wengine kuwa wamelaaniwa, , waongo, wa shetani!
 

Isaya 60

1 Ondoka, uangaze; kwa maana nuru yako imekuja, na utukufu wa BWANA umekuzukia.

2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; lakini BWANA atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako.

3 Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

4 Inua macho yako pande zote, utazame; wote wanakusanyika pamoja, wanakuja kwako;

5 Ndipo utakapoona na kutiririka pamoja, na moyo wako utaogopa na kukunjuka; kwa sababu wingi wa bahari utageuzwa kukujia, nguvu za mataifa zitakuja kwako.

6 Wingi wa ngamia utakufunika, ngamia wa ngamia wa Midiani na Efa; wote kutoka Sheba watakuja; wataleta dhahabu na uvumba; nao watatangaza sifa za BWANA.

7 Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;


Ili kumsaidia msomaji wa Kiyahudi na Mkristo kuelewa zaidi njia ya Kiislamu ya Ibada, ningependa kwanza kuwasilisha yafuatayo kutoka katika Biblia:

Mwanzo 28:16-18
16 Yakobo alipoamka katika usingizi wake, akawaza, Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Akaogopa, akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Hapa si kwingine ila Nyumba ya MUNGU;
18 Kesho yake asubuhi na mapema Yakobo akalitwaa jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.

Waamuzi 20:18
18 Wana wa Israeli wakapanda kwenda Betheli (Nyumba ya Mungu katika Kiebrania) na kuuliza kwa Mungu. Wakasema, Ni nani kati yetu atakayekwenda kwanza kupigana na Wabenyamini? Bwana akajibu, Yuda atakwenda kwanza.

1 Mambo ya Nyakati 6:47-49
47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48 Ndugu zao Walawi walipewa kazi nyingine zote za hema la ibada, yaani, Nyumba ya Mungu.
49 Lakini Haruni na wazao wake ndio waliotoa dhabihu juu ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa na juu ya madhabahu ya uvumba kwa ajili ya mambo yote yaliyofanywa katika Patakatifu pa Patakatifu pa kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, kulingana na yote ambayo Mose mtumishi. wa Mungu alikuwa ameamuru.


"Hakika tulimpa Ibrahim eneo la Nyumba (ya Al-Kaaba), tukasema: Usinishirikishe na chochote, na itakase Nyumba yangu kwa wanao izunguka. Au simama, au uiname, au usujudu (humo kwa kuswali) na utangaze Hija kwa watu, watakujia kwa miguu na (wamepanda) juu ya kila namna ya ngamia, wameegemea safari katika milima mirefu na ya mbali. njia kuu; (Qur’ani Tukufu, 22:26-27)”


Kama tunavyoona kwa uwazi, "Nyumba ya MUNGU"Mwenyezi imetajwa katika Biblia na Quran Tukufu. Kusujudu kwa Mwenyezi Mungu katika Nyumba yake au kwa njia ya Nyumba yake (kama unaishi mbali) ndiyo njia sahihi zaidi ya Ibada kwa mujibu wa Biblia na Quran Tukufu.
 
Unajua Kemet wewe? Unajua utaratibu wa imani za wa Kemet? Unamjua Amin-Ra, Osiris, Isis na Hotuba? Unaijua Ma at?

Jifunze kwanza hivyo vitu vichache ndo uje hapa kutueleza habari za uyahudi, ukiristo na uislam. mbali na hapo somo lako ni baridi.
 
Unaposema El,,,Kuna El ohim,,,El shadai,,,El Adonai nk,,,,,Kama kwako El ni Allah na maana ya Allah ni Mungu nisaie kujua kama Kuna huyo Mungu wenu Allah Subhana Wataalah kwenye biblia,,,au unithibitishie kwamba katika majina 99 ya Allah Subhana Wataalah lipo hata jina Moja lenye kuhusiana na Yehova/El Adonai au El shadai,,, baada ya hapo ndio tunaweza kuanza safari ya kwenda Saudi Arabia kujihakikishia kwamba Al kaaba ilijengwa na watu wa kabila la Waqureish au ilijengwa na Ibrahim... Kwamba huyo alieabudiwa Al kaaba ndie alieabudiwa Yerusalem???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiwango chako Cha kukaririshwa ni kizuri,,kama ungekuwa ndege lazima ungekuwa kasuku.. Sikulaumu maana huwezi kufikiria zaidi ya hapo labda kwa sababu ya ijaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Elimu bila malipo

 
Sasa mbona kiwango chako cha Sunday school kimeshindwa kujibu hoja zangu ambazo unadai nimekaririshwa ?
Paulo ni mtume wa kipekee aliewahi kutokea,,,na mchango wake katika injili ni outstanding/Unquestionable na pia hauwezi kuwa challenged na muislam yoyote hata marehemu Muhammad.Injili alioipotosha labda ni injili ya kiislam ya baraba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu bila malipo

Hapa hujanielewa,,,nisome vizuri Tena.Allah Subhana Wataalah ana majina 99,,,na akasema kwenu nyie wafuasi wake kwamba ""atakaejua jina lake la 100 ataingia peponi,,,Sasa wewe maalim nilitaka unionyeshe jina la Yehova,,au shadai au Elohim au Adonai katika hayo majina 99 ya Subhana Wataalah..Kukukumbusha ni kwamba Allah ni cheo sio jina,,,Maana 3 za ALLAH ni Mungu (cheo),,mzee na chai.Kwa hio nyie waislam Mungu wenu ni Subhana Wataalah,,,jina lake la kwanza,,,mengine pia wayajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii madam nimeiona Leo lakini Iko sahihi kabisaa ktk uislam mnyama akichinjwa na myahudi anaruhusiwa kuliwa kabisaa Kwa kua anachinja akiomba Kwa Dua ya Mungu mmoja
Mengi umeyasema ya kweli kabisaa ingawa miye sio mtu wa kubishana ila Iko sahihi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Naona umeamua kuunga unga,,,unataka kutuambia Hilo jiwe yakobo alilolimiminia mafuta ndio Hajar Al aswad?? Unalitetea jiwe lenu mnalolisujudia kama wapagani waliokuwa kabla yenu sio???
Kitu Cha msingi usitafute uhalali wa kusujudia jiwe lenu kwenye biblia ila tafuta uhalali wake kwenye Quran na ujiulize kama Allah Subhana Wataalah alikasimu uungu wake kwenye hilo jiwe Hadi mnalisujudia na kulibusu au yeye ni muongo na anatafuta njia ya kuwakataa at the end of day.

Mwisho swali la msingi mnalotakiwa mjiulize siku zote mkiwa hai ni hili ""Allah Subhana Wataalah ni nani""'???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya mapenzi ya Mungu Tu mpendeze Mungu Tu. Tenda mema Ishi kwa Haki na Mtegemee Yeye Muwezeshi muabudu yeye Katika Roho na kweli.

Aya mengine Tumejitungia Utaratibu na ustaharabu tu lakini Mungu ana angalia zaidi niliyo hainisha hapo juu.

Sio kazi yangu kukulazimisha Kuniamini au kutoniamini Baki katika Uliaminilo.
 
Soma history ya Paulo vizuri Iko yote ndani ya biblia usisikilize wanaomchukia na pia ondoa chuki dhidi yake na bila shaka utaweza kusoma nyaraka zake.Kwa kifupi Paulo alikuwa na Ego ilio juu ila baadae alikuja kuwa humble baada ya kumwelewa vizuri Kristo Yesu,,pia alikuwa mtume miongoni mwa mitume wa YESU KRISTO na alichaguliwa special kwa ajili ya mataifa eg Greece,, Cyprus,,Syria,,Italia, Macedonia uturuki nk huko kote ndie alieifikisha injili,,alibatiza kwa maji na kwa roho mtakatifu na alikufa kishahidi na bila shaka yupo mahali pa amani.Hakubadili torati ila aliikamilisha kama ilivyotakiwa iwe,,,na alikuwa akiijua torati kwa moyo ndio maana aliisimamia kwa usahihi Hadi alipokutana na neema akabadilishwa na akawa Bora zaidi.Na kazi alioifanya imekuwa na ubora usiofifia.

Ninyi hamumpendi kwa sababu mnadhani ana chuki na Sheria lakini yeye alichokifanya ni kuileta njia mpya ya utekelezaji wa Sheria bila Sheria kuwa dominant force ilio against na utekelezaji wake,,eg Umeambiwa usizini lakini tamaa ya kuzini ni kubwa kuliko Sheria ya kuzini..Sasa yeye anamfundisha muamini njia ya kuweza kutekeleza Sheria ya kutokuzini,,kuiba,,kuuwa pasipo na kutumia nguvu za mwili au akili.
Paulo waislam mnamchukia kwa sababu hamumuelewi maandiko yake na Ile Hali ya nyie kutokukubali ukweli kwamba uislam hauko kwenye biblia,,, uislam unajitegemea wenyewe na hauna uhusiano wowote na ukristo....Nyie mnatakiwa mkomae na Muhammad,,Seydina Ali,, Seydina Umar,,Abu hureira nk..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakukumbusha TU,,zaburi ya mfalme makini Daudi (King David) imeandikwa miaka yapata 2000 kabla hakujakuwa na dini inayoitwa uislam..Kwa hio hakukuwa na Muhammad,, Quran Wala Mungu wenu Allah Subhana Wataalah.Kwa hio ni Kitendo Cha utapeli wa maneno kutumia maneno ya zaburi kuuongelea uislam usiojisimamia wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo unayofundishwa msikitini yanayohusu ukristo Uwe na tabia ya kuyapitia wewe binafsi na kuyachuja usiyabebe kama yalivyo maana yanakufanya unakuwa kama kasuku.Wallah nakwambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…