Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

"Au mnasema kuwa ibrahim na ismail na is-haqa na yaaqub na wajukuu zao walikuwa mayahudi au wakristo? waambie: je, nyinyi ndio mnajua zaidi au allah? na hakuna mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeuficha ushahidi alionao utokao kwa allah,na allah si mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya."
Qur'an 2:140


"Hakuwa ibrahim myahudi wala mkristo, lakini alikuwa mwongofu muislamu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."
Qur'an 3:67


"Enyi watu wa kitabu! kwanini mnabishana juu ya ibrahim na hali ya kuwa taurati na injili havikuteremshwa isipokuwa baada yake? basi hamzingatii?."
Qur'an 3:65


"Tizameni! nyinyi mlibishana katika yale mliyokuwa mna elimu nayo, basi kwanini mnabishana katika yale msiyokuwa na elimu nayo? na allah ndiye mjuzi na nyinyi hamjui kitu."
Qur'an 3:66


Haya ni madai ya zamani sana na ni madai mepesi na dhaifu mno ijapokuwa mwandishi atajaza kurasa nyingi kwa maandishi yasiyo na hoja wala uzito wowote, ibrahim ndiye baba wa mitume waliotumwa kwa wana wa israeli na mtume wetu pia, je alikuwa dini gani? hali ya kuwa uyahudi na ukristo havikutokea isipokuwa baada ya kutumilizwa mussa na yesu, au ibrahim alikuja baada yao? na atakuja vipi baada ya vitukuu vyake?.

Uislamu ndio dini waliokuja nayo mitume wote tangu aadam alayhi ssalaam mpaka muhammad alayhi ssalaam na ndio ujumbe pekee waliokuja nao, kuwa watu wamuabudu allah peke yake pasi na kumshirikisha na chochote na wajiepushe na kumuabudu shetani, huu ndio ujumbe wao, na hajapatapo kuja mtume yeyote na ujumbe kuwa watu wamuabudu yeye na roho mtakatifu na baba yao, ama kusema uyahudi umezaa uislamu na ukristo huku ni kuchanganya taarifa kwa ajabu kabisa.

Karibu kwa mjadala kama una malengo ya kujifunza.
 
Wewe lazima utakuwa Jinni Mwislamu.
Unamnukuu mtu anaongea jambo fulani.
Badala ya kumjibu unaongea jambo lingine kabisa.

Umeongea habari ya UTATU.
Nimekuambia hakuna habari ya UTATU kwenye Biblia.
Labda UTATU wako.

Unaninukuu badala ya kueleza huo UTATU umeutoa wapi, unaongea habari nyingine kabisa.

Hii ni tabia ya Majini.

Jini linaongea tu jambo lolote lile ilimradi liharibu mjadala.

Jini linaongea utumbo ili lisikilizwe na kuharibu habari.

Ndio maana Majini wengi wamesilimu na kuwa Waislamu ili watu waache kumwabudu Mungu na badala yake waliabudu Jiwe Jeusi la Maka (Aswadi) na kusadiki ndilo linalo ondoa dhambi.

Mambo ya Walawi 26:1
Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Jami` at-Tirmidhi 857

Jabir narrated:

"The Prophet performed Raml from the (Black) Stone to the (Black) Stone for three (circuits), and he walked four (circuits).
Mtume anapiga Ramli hadharani...![emoji848]
Halafu ukiweka andiko kama hili unaambiwa unachuki na Dini.
Mambo ya ajabu sana.
Mtume mchawi anasilimisha Majini kila uchao ndio na mimi niwe mfuasi wake.

Gavana, Lini unaenda Maka kulisujudia Jiwe Jeusi ili likuondolee dhambi kama alivyofanya Mtume wa Majini ?
Mkuu japo sitaki kuingilia mjadala wenu ila unapotafsiri maneno ya kiarabu ushirikishe na ubongo wako.

فالرمل هو: الإسراع في المشي مع تقارب الخطى.

hilo neno arramalu ambalo umezusha tafsiri yake hapo juu eti ni kupiga ramli basi nikufahamishe maana yake ni kufanya haraka katika mwendo kwa hatua fupi fupi, na hili mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake alilifanya kama ulivyonukuu hapo juu, kuwa alitembea haraka baina ya jiwe jeusi na jiwe jeusi kwa kama mizunguko mitatu na sio alipiga ramli, kiarabu sio kizigua mkuu hii ni lugha pana mno yenye kuhitaji misingi mizuri ya utambuzi sio unajitafsiria tafsiria tu, usifute tu comment kwa aibu wacha watu waje washuhudie aibu yako.

ama ramli imeharamishwa katika Qur'an na hadithi zake mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake, ukirudi kunijibu uje umejipanga usije kututia aibu tena.
 
Wewe lazima utakuwa Jinni Mwislamu.
Unamnukuu mtu anaongea jambo fulani.
Badala ya kumjibu unaongea jambo lingine kabisa.

Umeongea habari ya UTATU.
Nimekuambia hakuna habari ya UTATU kwenye Biblia.
Labda UTATU wako.

Unaninukuu badala ya kueleza huo UTATU umeutoa wapi, unaongea habari nyingine kabisa.

Hii ni tabia ya Majini.

Jini linaongea tu jambo lolote lile ilimradi liharibu mjadala.

Jini linaongea utumbo ili lisikilizwe na kuharibu habari.

Ndio maana Majini wengi wamesilimu na kuwa Waislamu ili watu waache kumwabudu Mungu na badala yake waliabudu Jiwe Jeusi la Maka (Aswadi) na kusadiki ndilo linalo ondoa dhambi.

Mambo ya Walawi 26:1
Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Jami` at-Tirmidhi 857

Jabir narrated:

"The Prophet performed Raml from the (Black) Stone to the (Black) Stone for three (circuits), and he walked four (circuits).
Mtume anapiga Ramli hadharani...![emoji848]
Halafu ukiweka andiko kama hili unaambiwa unachuki na Dini.
Mambo ya ajabu sana.
Mtume mchawi anasilimisha Majini kila uchao ndio na mimi niwe mfuasi wake.

Gavana, Lini unaenda Maka kulisujudia Jiwe Jeusi ili likuondolee dhambi kama alivyofanya Mtume wa Majini ?


Nyumba/Hekalu la MUNGU Mwenyezi katika Quran Tukufu na Biblia.


Unabii juu ya Waislamu watamsujudia MUNGU kwa njia ya Hekalu lake Takatifu. Angalia unabii wa "nitafanya" na "kuelekea":


Zaburi 138:2
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, na kulisifu jina lako kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza jina lako na neno lako kuliko vitu vyote.



Pia, njia ya Utakatifu kuelekea Makka ilitabiriwa kikamilifu katika Biblia. Huu hapa ni mfano kutoka kwa wengi kuhusu Uarabuni:

arabia_will_rejoice_isaiah35_1.png


Uchakachuwaji NT ulirekodiwa miaka 200+ baada ya Yesu. Ukristo umejaa uchakachuwaji wa kanisa. Wanafunzi walikuwa na migogoro wao kwa wao. Timu za Paulo dhidi ya Peter zilikuwa zikiita wengine kuwa wamelaaniwa, , waongo, wa shetani!
 
Wewe lazima utakuwa Jinni Mwislamu.
Unamnukuu mtu anaongea jambo fulani.
Badala ya kumjibu unaongea jambo lingine kabisa.

Umeongea habari ya UTATU.
Nimekuambia hakuna habari ya UTATU kwenye Biblia.
Labda UTATU wako.

Unaninukuu badala ya kueleza huo UTATU umeutoa wapi, unaongea habari nyingine kabisa.

Hii ni tabia ya Majini.

Jini linaongea tu jambo lolote lile ilimradi liharibu mjadala.

Jini linaongea utumbo ili lisikilizwe na kuharibu habari.

Ndio maana Majini wengi wamesilimu na kuwa Waislamu ili watu waache kumwabudu Mungu na badala yake waliabudu Jiwe Jeusi la Maka (Aswadi) na kusadiki ndilo linalo ondoa dhambi.

Mambo ya Walawi 26:1
Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Jami` at-Tirmidhi 857

Jabir narrated:

"The Prophet performed Raml from the (Black) Stone to the (Black) Stone for three (circuits), and he walked four (circuits).
Mtume anapiga Ramli hadharani...![emoji848]
Halafu ukiweka andiko kama hili unaambiwa unachuki na Dini.
Mambo ya ajabu sana.
Mtume mchawi anasilimisha Majini kila uchao ndio na mimi niwe mfuasi wake.

Gavana, Lini unaenda Maka kulisujudia Jiwe Jeusi ili likuondolee dhambi kama alivyofanya Mtume wa Majini ?

Isaya 60

1 Ondoka, uangaze; kwa maana nuru yako imekuja, na utukufu wa BWANA umekuzukia.

2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; lakini BWANA atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako.

3 Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

4 Inua macho yako pande zote, utazame; wote wanakusanyika pamoja, wanakuja kwako;

5 Ndipo utakapoona na kutiririka pamoja, na moyo wako utaogopa na kukunjuka; kwa sababu wingi wa bahari utageuzwa kukujia, nguvu za mataifa zitakuja kwako.

6 Wingi wa ngamia utakufunika, ngamia wa ngamia wa Midiani na Efa; wote kutoka Sheba watakuja; wataleta dhahabu na uvumba; nao watatangaza sifa za BWANA.

7 Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;


Ili kumsaidia msomaji wa Kiyahudi na Mkristo kuelewa zaidi njia ya Kiislamu ya Ibada, ningependa kwanza kuwasilisha yafuatayo kutoka katika Biblia:

Mwanzo 28:16-18
16 Yakobo alipoamka katika usingizi wake, akawaza, Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Akaogopa, akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Hapa si kwingine ila Nyumba ya MUNGU;
18 Kesho yake asubuhi na mapema Yakobo akalitwaa jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.

Waamuzi 20:18
18 Wana wa Israeli wakapanda kwenda Betheli (Nyumba ya Mungu katika Kiebrania) na kuuliza kwa Mungu. Wakasema, Ni nani kati yetu atakayekwenda kwanza kupigana na Wabenyamini? Bwana akajibu, Yuda atakwenda kwanza.

1 Mambo ya Nyakati 6:47-49
47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48 Ndugu zao Walawi walipewa kazi nyingine zote za hema la ibada, yaani, Nyumba ya Mungu.
49 Lakini Haruni na wazao wake ndio waliotoa dhabihu juu ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa na juu ya madhabahu ya uvumba kwa ajili ya mambo yote yaliyofanywa katika Patakatifu pa Patakatifu pa kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, kulingana na yote ambayo Mose mtumishi. wa Mungu alikuwa ameamuru.


"Hakika tulimpa Ibrahim eneo la Nyumba (ya Al-Kaaba), tukasema: Usinishirikishe na chochote, na itakase Nyumba yangu kwa wanao izunguka. Au simama, au uiname, au usujudu (humo kwa kuswali) na utangaze Hija kwa watu, watakujia kwa miguu na (wamepanda) juu ya kila namna ya ngamia, wameegemea safari katika milima mirefu na ya mbali. njia kuu; (Qur’ani Tukufu, 22:26-27)”


Kama tunavyoona kwa uwazi, "Nyumba ya MUNGU"Mwenyezi imetajwa katika Biblia na Quran Tukufu. Kusujudu kwa Mwenyezi Mungu katika Nyumba yake au kwa njia ya Nyumba yake (kama unaishi mbali) ndiyo njia sahihi zaidi ya Ibada kwa mujibu wa Biblia na Quran Tukufu.
 
Anaandika Robert Heriel,

Ukristo na Uislam ni watoto wa baba mmoja aitwaye Uyahudi.
Licha ya kuwa Ukristo ulitangulia kabla ya Uislam lakini Uislam kwenye ishu ya maadili upo makini zaidi kuliko Ukristo, na dini hizo zote mbili baba yao ni dini ya Kiyahudi (Judaism).

Ukisema Ukristo ni mtoto mtundu au mkaidi aliyegundua mavumbuzi mengi hautokuwa unakosea. Labda kwa vile ni mtoto wa kwanza. Uislam ni lastborn wa Uyahudi ambao umeendelea kushika baadhi ya Falsafa na principles za baba yake.

Dini ni maadili ambayo yamejengwa kwa msingi wa imani. Kuamini katika miungu, lakini lengo kuu la dini ni ishu ya maadili.

Ukristo na Uislam hauwezi kusimama wenyewe bila kutegemea Uyahudi, hiyo haiwezekaniki kwani huyo ndiye baba yao. Hata hivyo kama utatazama kwa jicho lisilo la makengeza, unaweza kuona bila ya shaka kuwa Ukristo unahangaika kujitegemea wenyewe pasipo kufuata misingi ya baba yake Uyahudi.

Licha ya kuwa lastborn Uislam anaonekana kuwa alimpinga na hamtaki baba yake Myahudi lakini ukiangalia mtazamo na falsafa zake bado zinajikita kwa baba yake. Wakati huo Ukristo yeye kwa vile ni firstborn ambaye kisheria ndiye mrithi kwa nje anaonekana kumkubali baba yake Myahudi lakini kimatendo na kifalsafa anampinga baba yake.

Baada ya watoto kukua wanahama na kwenda kuanzisha miji yao. Ukristo boma/mji wake aliuita KANISA
Uislam boma/mji wake akauita MSIKITI. Wakazaliwa watoto, Ukristo ukazaa Wakristo wakati Uislam ukazaa watoto Waislam ambaye babu yao ni Uyahudi.

Falsafa chache za baba Uyahudi ukilinganisha na watoto wake wawili:
1. Mungu ni mmoja,
Ukristo hauamini katika Mungu mmoja isipokuwa mmoja katika utatu Mtakatifu. Baba, mwana, na roho mtakatifu.

Uislam unaungana na Baba yake Uyahudi kuwa Mungu ni mmoja na wapekee asiye na mshirika. Yaani hakuna cha utatu wala upili. Katika falsafa hii Ukristo unapingana na baba yake huku Uislam ukiungana na Baba yake.

2. Mungu ni mtakatifu/msafi
Ukristo: Mtoto huyu anasema kwa mdomo jambo hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu wa mwili na mavazi.

Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Ukristo umejijenga zaidi katika kanuni ya kusafisha ndani zaidi kuliko nje. Lakini umesahau kuwa uchafu unatokea nje kwenda ndani.

Ukristo unaruhusu mtu kula jambo lolote kwa imani, siyo ajabu Ukristo mtu kula nguruwe au panya au mbwa kwa sababu ni kwa imani.

Uislam: Mtoto huyu anasema mdomoni na kutekeleza kwa vitendo. Falsafa na kanuni hizi amezitoa kwa baba yake aitwaye Uyahudi. Mungu ni msafi/mtakatifu na anataka watu wake wawe watakatifu/wasafi.

Uislam umeiga tabia ya baba yake kugawa vitu visafi na vichafu. Kipi chafaa kula na kipi hakifai. Uislam hauwezi kula uchafu.

3. Ndoa na mahusiano.
Ukristo: Mtoto huyu amemuasi baba yake dhahiri shahiri. Uyahudi kuna sheria ya talaka lakini Ukristo kaamua kuiweka kapuni. Hii inafanya watu wawe watumwa kwenye mahusiano yasiyo na tija.

Ikiwa siyo lazima kuwa na mahusiano na Mungu iweje iwe lazima ukioa mke au kuolewa na mume muishi maisha yote? Ndoa ni mkataba wa hiyari kwasababu unahusu upendo. Upendo ni hiyari, kama watu watapishana waachane. Uyahudi unaeleza hivyo, Ukristo hautaki.

Ukristo huyu mtoto kapingana na baba yake. Uyahudi haukatazi mtu kuoa wake wengi, unaruhusu ndiyo maana kunasheria zinazohusu mtu atakayetaka kuoa wake wengi.
Ukristo hautaki na umepinga jambo hilo.

Uislam: Mtoto huyu licha ya kuonekana kama muasi kwa babaye lakini bado anatumia kanuni zilezile za baba yake.
Mtoto huyu anaruhusu Talaka kama kuna mambo yanaenda ndivyo alivyo. Pia mtoto huyu anaruhusu wake wengi ingawaje ameweka kikomo kuwa ni wake wanne.

4. Mavazi
Ukristo: Mtoto huyu anatumia u-firstborn wake vibaya. Ukristo unaruhusu mtu avae atakavyo kwani Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo wa mtu.
Siyo ajabu wafuasi wa Ukristo kuwaona wakivaa nguo zisizo na stara.

Hii ni tofauti na baba yake Uyahudi ambaye alikuwa na sheria za mavazi na kusisitiza watu wavae kwa adabu hasa wanawake wajistiri kutokana na maumbile yao kuwa na ushawishi.

Uislam: Mtoto huyu mwenye madeko ambaye yeye kila kitu lazima aone anaonewa, yeye anaungana na baba yake katika hilo. Uislam unazingatia maadili ya mavazi. Wafuasi wa mtoto huyo wamekuwa wastaarabu/waungwana sana katika hilo.

5. Mwanaume ndiye kuhani.
Ukristo: Ukristo kadiri siku zinavyoenda unazidi kuonyesha kupuyanga na kutumia urithi wa u-firstborn vibaya kama alivyofanya Esau. Ukristo unaruhusu mtu yeyote kuwa kuhani hata kama ni mwanamke. Wakati baba yake Uyahudi jambo hilo kwake kamwe lisingewezekana.

Nafasi ya mwanaume kwenye Ukristo huchukuliwa kuwa sawa na mwanaume. Wakati mzee Uyahudi hilo kwake lilikuwa ni ushetani.

Uislam: Ni kufuru kubwa kwa mtoto wa kike kusimama madhabahuni kuwahutubia wanaume. Hilo uislam alilichukua kama lilivyo na analitekeleza. Uislam umempa nafasi kubwa mwanaume kama ilivyo kwa baba yake Uyahudi.

6. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.
Ukristo: Unatanabaisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kupitia kwa Bikra Maria aliyepewa mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Hoja hii ndiyo mzizi wa utatu mtakatifu na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu, ilhali hilo kamwe hata kwa akili ya panzi haliwezekaniki.

Baba yao Uyahudi kama ungesikika ukisema maneno hayo, basi ilikuwa umeamua kutaka kuuawa kwa kupiga mawe kwani ungekuwa umekufuru na kufanya dhambi kubwa mno.

Uislam: Mtoto huyu yeye anabaki na msimamo wa baba yake kuwa Mungu hajazaa wala hajazaliwa. Na Hilo ni kosa kubwa la kukufuru.

7. Neema
Ukristo: Ukristo huu ndiyo msingi namba moja yaani huwezi tenganisha Ukristo na neema.
Kwamba mtu akifanya kosa basi anastahili kupewa nafasi ya pili, neema pasipo kuhukumiwa.
Wakati baba yake Uyahudi yeye kanuni yake ni haki. Kwamba mtu akikosea basi aadhibiwe, na mtu akipatia basi apewe zawadi yake (thawabu).

Uyahudi ulijikita kwenye mwili na roho. Wakati Ukristo unajikita katika roho pekee. Hii ni kumaanisha kinachopewa neema ni roho sio mwili. Yaani mtu akiomba neema ya msamaha, basi roho yake ndio ipewe second chance lakini mwili uadhibiwe.

Lakini wafuasi wa Ukristo wakalazimisha kuwa mwili na roho vyote vipewe neema😂😂. Huku wakishikilia kanuni isemayo usihukumu usije ukahukumiwa au samehe saba mara sabini. Wakisahau kuwa mwili ndio unafanya makosa wakati huo roho ndiyo hufanya dhambi😂😂. Mwili huadhibiwa na dunia kwa makosa yake wakati huohuo roho huadhibiwa na Mungu kwa dhambi zake.

Uislam: Mtoto huyo yeye kafuatisha kwa kiasi kikubwa kanuni na sheria na falsafa za baba yake. Mwenye makosa aadhibiwe kulingana na makosa yake na vile sheria zisemavyo.

Zingatia, binadamu hawezi kusamehe dhambi isipokuwa Mungu. Ila anasemehe makosa kwa sababu ya mwili ndiyo hufanya makosa na roho ndiyo itendayo dhambi. Kumaanisha, roho ndiyo inamuasi Mungu halafu mwili unamfanyia makosa binadamu mwenzako au kiumbe au mazingira yanayokuzunguka.

8. Hukumu
Ukristo: Mtoto huyu anajieleza kuwa atakayehukumu ulimwengu ni Kristo/Yesu.
Na Yesu ndiye atakuwa mtawala wa kila kitu. Hii ni tofauti na falsafa ya baba mtu Uyahudi. Yeye anajua Mungu ndiye mtawala na ndiye atakayehukumu viumbe vyake kwa haki. Zingatia neno viumbe inamaanisha vinavyoonekana na visivyoonekana. Hata Yesu pia ni kiumbe.

Uislam: Huyu mtoto anaungana na baba yake Uyahudi kwa kusema, hukumu atakayoitoa ni Mungu. Na kila kiumbe atahukumiwa kulingana na yale aliyoyafanya.

9. Urithi na mirathi
Ukristo: Umejikita zaidi katika mambo ya kiroho na kusahau mambo ya kimwili. Ukristo unajikita katika urithi wa Ufalme wa mbinguni pekee. Ilhali baba yake akijikita kwa yote mawili.
Uyahudi ilitoa utaratibu wa namna ya kurithisha mali kwa haki, na namna ya kutoa mirathi endapo mtu atakufa.

Ukristo jambo hilo limeachwa liamuliwe kidunia, hapohapo dunia kwa mujibu wa Ukristo inaongozwa na shetani😂😂. Unaona mambo hayo!

Uislam: Mtoto huyu kamuiga baba yake na kuongeza baadhi ya vitu. Kajikita kiroho na kimwili.
Urithi na mirathi kwa uislam imefafanuliwa namna itakavyogawiwa. Uislam haujaliacha jambo hilo liamuliwe na walimwengu kwani shetani ndiye mlimwengu mwenyewe.

Mpaka hapo sina la ziada, siyo kazi yangu kukuambia kipi chakuamini au kipi ni sahihi na kipi sio sahihi. Nilikuwa naeleza habari za watoto hao wawili wenye wafuasi wengi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Unajua Kemet wewe? Unajua utaratibu wa imani za wa Kemet? Unamjua Amin-Ra, Osiris, Isis na Hotuba? Unaijua Ma at?

Jifunze kwanza hivyo vitu vichache ndo uje hapa kutueleza habari za uyahudi, ukiristo na uislam. mbali na hapo somo lako ni baridi.
 
Abraham alipofika caanan, alianza kumuabudu El( Allah),, Hajra na mwanae ishmael walihama kutoka caanan na kuishi Jeddah, arabia,, huko Abraham alijenga hiyo Al kaaba,, fast forward miaka maelfu mbele,, wakazi wa maeneo hayo waliendelea kuabudu hapo kwa style za kipagani,, hadi wakati wa mohamed,, hivyo alkaaba imekuwa BerthEl(Bayt Allah) tangu enzi za Abraham,, kwa mujibu wa simulizi
Unaposema El,,,Kuna El ohim,,,El shadai,,,El Adonai nk,,,,,Kama kwako El ni Allah na maana ya Allah ni Mungu nisaie kujua kama Kuna huyo Mungu wenu Allah Subhana Wataalah kwenye biblia,,,au unithibitishie kwamba katika majina 99 ya Allah Subhana Wataalah lipo hata jina Moja lenye kuhusiana na Yehova/El Adonai au El shadai,,, baada ya hapo ndio tunaweza kuanza safari ya kwenda Saudi Arabia kujihakikishia kwamba Al kaaba ilijengwa na watu wa kabila la Waqureish au ilijengwa na Ibrahim... Kwamba huyo alieabudiwa Al kaaba ndie alieabudiwa Yerusalem???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa ni Thomas Jefferson aliyesema: “Paulo alikuwa great Coryphaeus na mpotoshaji wa kwanza wa Injili ya Yesu”.


Mikanganyiko

(1)

Kwa hiyo hakuna mtu atakayehesabiwa haki mbele zake kwa kushika sheria; bali kwa njia ya sheria tunafahamu dhambi. ( Warumi 3:20 )

Imepingwa na:

Kwa maana si wale waisikiao sheria walio waadilifu mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaotangazwa kuwa waadilifu. ( Warumi 2:13 )


(2)

Mchukuliane mizigo, na kwa njia hii mtaitimiza sheria ya Kristo. (Wagalatia 6:2)

Imepingwa na:

Maana kila mmoja na awe na mzigo wake mwenyewe. ( Wagalatia 6:5 )

(4)

Kwa maana Kristo alikufa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Aliuawa katika mwili, lakini akahuishwa na Roho, (1 Petro 3:18).

Imepingwa na:

Mtu mwovu ni fidia ya wenye haki, na msaliti kwa ajili ya wanyofu. ( Mithali 21:18 )

(5)

Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi, kwa maana Mungu atawahukumu wazinzi na wazinzi wote. ( Waebrania 13:4 )

Imepingwa na:

Lakini ukioa hutakuwa umetenda dhambi; na bikira akiolewa hatakuwa ametenda dhambi. Lakini wale wanaofunga ndoa watapata taabu nyingi katika maisha haya, nami nataka niwaepushie haya. ( 1 Wakorintho 7:28 )

(7)

Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na upendo wake unakamilishwa ndani yetu. ( 1 Yohana 4:12 )

Imepingwa na:

Nikamwona Bwana amesimama juu ya madhabahu; nami nitawaua walio wa mwisho wao kwa upanga; ( Amosi 9:1 )

(8)

Kama niliyafunika makosa yangu kama Adamu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu; (Ayubu 31:33)

Imepingwa na:

Wala Adamu hakudanganywa, bali mwanamke alidanganywa akawa katika hali ya kukosa. ( 1Timotheo 2:14 )

Mstari huo unasema kwamba Adamu alitenda dhambi, lakini Agano Jipya linasema kwamba Adamu hakutenda dhambi, bali Hawa pekee ndiye aliyetenda dhambi.


Kulingana na Yesu, Paulo alikuwa mnafiki:


“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki, mnafunga ufalme wa mbinguni mbele ya watu.
Ikilinganishwa na

Ndipo Paulo, akijua ya kuwa baadhi yao ni Masadukayo na wengine Mafarisayo, akapaza sauti katika baraza, akisema, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana wa Farisayo; nasimama mbele ya hukumu kwa ajili ya tumaini langu katika ufufuo wa wafu. ." ( Matendo 23:6 )

Paulo anataka watu wawe wenye dhambi!

Laiti kama watu wote wangekuwa kama mimi. Lakini kila mtu ana karama yake mwenyewe kutoka kwa Mungu; mmoja ana kipawa hiki, mwingine ana kile. 1 Wakorintho 7:6-7

Hili ni neno la kutegemewa linalostahili kukubalika kabisa: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi, ambao mimi ni mbaya zaidi kati yao. ( 1 Tim. 1:15 )

Paulo anashuhudia kwamba hakuna kitu kizuri ndani yake:


Paulo anazidi kujichanganya


(1) Mungu Kamili au Mungu Aliye Tupu:


“Kristo Yesu ambaye, ingawa alikuwa yuna namna ya Mungu, hakuona kuwa kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa” (Wafilipi 2:6).

Imepingwa na:

“Maana katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae (Wakolosai 1:19).


(2) Mungu au Mpatanishi au Hakuna:


“Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu” (1 Timotheo 2:5).

Imepingwa na:

"Lakini hakuna haja ya mpatanishi katika kesi ya mmoja, na Mungu ni mmoja" (Wagalatia 3:20).


(3) Sheria Iliyofutwa au Sheria Iliyozingatiwa:

“Akaukomesha ule uadui kwa kuibatilisha sheria ya amri pamoja na kanuni zake” (Waefeso 2:14).

Imepingwa na:

“Je, tunaipindua Sheria kwa imani hii? La hasha! Kinyume chake, tunashika Sheria.” ( Warumi 3:31 )


(4) Haki; na Sheria au bila Sheria:


"Hakuna mwanadamu hata mmoja atakayefanywa kuwa mwadilifu mbele za Mungu kwa kushika sheria" (Warumi 3:20).

Imepingwa na:


“Kwa maana si wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali wale waitendao sheria watahesabiwa haki” (Warumi 2:13).

(5) Wokovu; kwa Kuungama au kwa Vitendo:


"Ukimkiri Yesu kwa midomo yako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka" (Warumi 10:9).


Imepingwa na:


“Kwa maana yeye (Mungu) atamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi ya kutenda mema watatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, atawapa uzima wa milele” (Warumi 2:6).


(Chanzo: Roshan Enam, Mfuate Yesu au Mfuate Paulo? uku. 65-55)


(6)


Anaitikisa dunia kutoka mahali pake na kufanya nguzo zake zitetemeke. ( Ayubu 9:6 )



Imepingwa na:


Aliiweka dunia juu ya misingi yake; haiwezi kamwe kusogezwa. ( Zaburi 104:5 )


(7)

Kizazi kimoja kinapita, na kizazi kingine kinakuja, lakini dunia hudumu milele. ( Mhubiri 1:4 )

Imepingwa na:

Dunia imepasuliwa, dunia imepasuliwa, dunia inatikisika kabisa. Nchi inayumba-yumba kama mlevi, inayumba-yumba kama kibanda katika upepo; ni nzito sana juu yake hatia ya uasi wake kwamba inaanguka—haitasimama tena. ( Isaya 24:19-20 )

(8)


Kisha Petro akaanza kusema: “Sasa natambua jinsi ilivyo kweli kwamba Mungu hana upendeleo bali huwakubali watu kutoka katika kila taifa wanaomwogopa na kufanya yaliyo sawa.

Imepingwa na:

Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki yake mwenyewe, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. ( 1 Petro 2:9 )
Kiwango chako Cha kukaririshwa ni kizuri,,kama ungekuwa ndege lazima ungekuwa kasuku.. Sikulaumu maana huwezi kufikiria zaidi ya hapo labda kwa sababu ya ijaza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaposema El,,,Kuna El ohim,,,El shadai,,,El Adonai nk,,,,,Kama kwako El ni Allah na maana ya Allah ni Mungu nisaie kujua kama Kuna huyo Mungu wenu Allah Subhana Wataalah kwenye biblia,,,au unithibitishie kwamba katika majina 99 ya Allah Subhana Wataalah lipo hata jina Moja lenye kuhusiana na Yehova/El Adonai au El shadai,,, baada ya hapo ndio tunaweza kuanza safari ya kwenda Saudi Arabia kujihakikishia kwamba Al kaaba ilijengwa na watu wa kabila la Waqureish au ilijengwa na Ibrahim... Kwamba huyo alieabudiwa Al kaaba ndie alieabudiwa Yerusalem???

Sent using Jamii Forums mobile app

Elimu bila malipo

 
Sasa mbona kiwango chako cha Sunday school kimeshindwa kujibu hoja zangu ambazo unadai nimekaririshwa ?
Paulo ni mtume wa kipekee aliewahi kutokea,,,na mchango wake katika injili ni outstanding/Unquestionable na pia hauwezi kuwa challenged na muislam yoyote hata marehemu Muhammad.Injili alioipotosha labda ni injili ya kiislam ya baraba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu bila malipo

Hapa hujanielewa,,,nisome vizuri Tena.Allah Subhana Wataalah ana majina 99,,,na akasema kwenu nyie wafuasi wake kwamba ""atakaejua jina lake la 100 ataingia peponi,,,Sasa wewe maalim nilitaka unionyeshe jina la Yehova,,au shadai au Elohim au Adonai katika hayo majina 99 ya Subhana Wataalah..Kukukumbusha ni kwamba Allah ni cheo sio jina,,,Maana 3 za ALLAH ni Mungu (cheo),,mzee na chai.Kwa hio nyie waislam Mungu wenu ni Subhana Wataalah,,,jina lake la kwanza,,,mengine pia wayajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii madam nimeiona Leo lakini Iko sahihi kabisaa ktk uislam mnyama akichinjwa na myahudi anaruhusiwa kuliwa kabisaa Kwa kua anachinja akiomba Kwa Dua ya Mungu mmoja
Mengi umeyasema ya kweli kabisaa ingawa miye sio mtu wa kubishana ila Iko sahihi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Isaya 60

1 Ondoka, uangaze; kwa maana nuru yako imekuja, na utukufu wa BWANA umekuzukia.

2 Maana, tazama, giza litaifunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; lakini BWANA atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako.

3 Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

4 Inua macho yako pande zote, utazame; wote wanakusanyika pamoja, wanakuja kwako;

5 Ndipo utakapoona na kutiririka pamoja, na moyo wako utaogopa na kukunjuka; kwa sababu wingi wa bahari utageuzwa kukujia, nguvu za mataifa zitakuja kwako.

6 Wingi wa ngamia utakufunika, ngamia wa ngamia wa Midiani na Efa; wote kutoka Sheba watakuja; wataleta dhahabu na uvumba; nao watatangaza sifa za BWANA.

7 Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;


Ili kumsaidia msomaji wa Kiyahudi na Mkristo kuelewa zaidi njia ya Kiislamu ya Ibada, ningependa kwanza kuwasilisha yafuatayo kutoka katika Biblia:

Mwanzo 28:16-18
16 Yakobo alipoamka katika usingizi wake, akawaza, Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Akaogopa, akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Hapa si kwingine ila Nyumba ya MUNGU;
18 Kesho yake asubuhi na mapema Yakobo akalitwaa jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.

Waamuzi 20:18
18 Wana wa Israeli wakapanda kwenda Betheli (Nyumba ya Mungu katika Kiebrania) na kuuliza kwa Mungu. Wakasema, Ni nani kati yetu atakayekwenda kwanza kupigana na Wabenyamini? Bwana akajibu, Yuda atakwenda kwanza.

1 Mambo ya Nyakati 6:47-49
47 mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48 Ndugu zao Walawi walipewa kazi nyingine zote za hema la ibada, yaani, Nyumba ya Mungu.
49 Lakini Haruni na wazao wake ndio waliotoa dhabihu juu ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa na juu ya madhabahu ya uvumba kwa ajili ya mambo yote yaliyofanywa katika Patakatifu pa Patakatifu pa kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, kulingana na yote ambayo Mose mtumishi. wa Mungu alikuwa ameamuru.


"Hakika tulimpa Ibrahim eneo la Nyumba (ya Al-Kaaba), tukasema: Usinishirikishe na chochote, na itakase Nyumba yangu kwa wanao izunguka. Au simama, au uiname, au usujudu (humo kwa kuswali) na utangaze Hija kwa watu, watakujia kwa miguu na (wamepanda) juu ya kila namna ya ngamia, wameegemea safari katika milima mirefu na ya mbali. njia kuu; (Qur’ani Tukufu, 22:26-27)”


Kama tunavyoona kwa uwazi, "Nyumba ya MUNGU"Mwenyezi imetajwa katika Biblia na Quran Tukufu. Kusujudu kwa Mwenyezi Mungu katika Nyumba yake au kwa njia ya Nyumba yake (kama unaishi mbali) ndiyo njia sahihi zaidi ya Ibada kwa mujibu wa Biblia na Quran Tukufu.
Naona umeamua kuunga unga,,,unataka kutuambia Hilo jiwe yakobo alilolimiminia mafuta ndio Hajar Al aswad?? Unalitetea jiwe lenu mnalolisujudia kama wapagani waliokuwa kabla yenu sio???
Kitu Cha msingi usitafute uhalali wa kusujudia jiwe lenu kwenye biblia ila tafuta uhalali wake kwenye Quran na ujiulize kama Allah Subhana Wataalah alikasimu uungu wake kwenye hilo jiwe Hadi mnalisujudia na kulibusu au yeye ni muongo na anatafuta njia ya kuwakataa at the end of day.

Mwisho swali la msingi mnalotakiwa mjiulize siku zote mkiwa hai ni hili ""Allah Subhana Wataalah ni nani""'???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya mapenzi ya Mungu Tu mpendeze Mungu Tu. Tenda mema Ishi kwa Haki na Mtegemee Yeye Muwezeshi muabudu yeye Katika Roho na kweli.

Aya mengine Tumejitungia Utaratibu na ustaharabu tu lakini Mungu ana angalia zaidi niliyo hainisha hapo juu.

Sio kazi yangu kukulazimisha Kuniamini au kutoniamini Baki katika Uliaminilo.
 
Soma history ya Paulo vizuri Iko yote ndani ya biblia usisikilize wanaomchukia na pia ondoa chuki dhidi yake na bila shaka utaweza kusoma nyaraka zake.Kwa kifupi Paulo alikuwa na Ego ilio juu ila baadae alikuja kuwa humble baada ya kumwelewa vizuri Kristo Yesu,,pia alikuwa mtume miongoni mwa mitume wa YESU KRISTO na alichaguliwa special kwa ajili ya mataifa eg Greece,, Cyprus,,Syria,,Italia, Macedonia uturuki nk huko kote ndie alieifikisha injili,,alibatiza kwa maji na kwa roho mtakatifu na alikufa kishahidi na bila shaka yupo mahali pa amani.Hakubadili torati ila aliikamilisha kama ilivyotakiwa iwe,,,na alikuwa akiijua torati kwa moyo ndio maana aliisimamia kwa usahihi Hadi alipokutana na neema akabadilishwa na akawa Bora zaidi.Na kazi alioifanya imekuwa na ubora usiofifia.

Ninyi hamumpendi kwa sababu mnadhani ana chuki na Sheria lakini yeye alichokifanya ni kuileta njia mpya ya utekelezaji wa Sheria bila Sheria kuwa dominant force ilio against na utekelezaji wake,,eg Umeambiwa usizini lakini tamaa ya kuzini ni kubwa kuliko Sheria ya kuzini..Sasa yeye anamfundisha muamini njia ya kuweza kutekeleza Sheria ya kutokuzini,,kuiba,,kuuwa pasipo na kutumia nguvu za mwili au akili.
Paulo waislam mnamchukia kwa sababu hamumuelewi maandiko yake na Ile Hali ya nyie kutokukubali ukweli kwamba uislam hauko kwenye biblia,,, uislam unajitegemea wenyewe na hauna uhusiano wowote na ukristo....Nyie mnatakiwa mkomae na Muhammad,,Seydina Ali,, Seydina Umar,,Abu hureira nk..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyumba/Hekalu la MUNGU Mwenyezi katika Quran Tukufu na Biblia.


Unabii juu ya Waislamu watamsujudia MUNGU kwa njia ya Hekalu lake Takatifu. Angalia unabii wa "nitafanya" na "kuelekea":


Zaburi 138:2
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, na kulisifu jina lako kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza jina lako na neno lako kuliko vitu vyote.



Pia, njia ya Utakatifu kuelekea Makka ilitabiriwa kikamilifu katika Biblia. Huu hapa ni mfano kutoka kwa wengi kuhusu Uarabuni:

arabia_will_rejoice_isaiah35_1.png


Uchakachuwaji NT ulirekodiwa miaka 200+ baada ya Yesu. Ukristo umejaa uchakachuwaji wa kanisa. Wanafunzi walikuwa na migogoro wao kwa wao. Timu za Paulo dhidi ya Peter zilikuwa zikiita wengine kuwa wamelaaniwa, , waongo, wa shetani!
Nakukumbusha TU,,zaburi ya mfalme makini Daudi (King David) imeandikwa miaka yapata 2000 kabla hakujakuwa na dini inayoitwa uislam..Kwa hio hakukuwa na Muhammad,, Quran Wala Mungu wenu Allah Subhana Wataalah.Kwa hio ni Kitendo Cha utapeli wa maneno kutumia maneno ya zaburi kuuongelea uislam usiojisimamia wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Kisha wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ambao Yesu aliwaambia waende.


17 Walipomwona, walimsujudia; lakini wengine walitilia shaka.


18 Kisha Yesu akaja kwao na kusema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.


19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na hakika mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

Mathayo 28:16-20

Sasa hebu tujadili aya hizi ambazo zimeingizwa kwenye maandishi na sio asili yake.


Ukosoaji wa kwanza ambao unaweza kuelekezwa kwenye kifungu hiki ni kwamba licha ya umuhimu wake, haijatajwa katika Injili zingine tatu ambazo zote zinasimulia kisa cha Kristo kuingia Yerusalemu akiwa amepanda punda.

Je, kupanda kwake punda ni muhimu zaidi kuliko kutaja utatu, ambao haukutajwa na yeyote kando na Mathayo?

Hakika, sura ya mwisho ya Injili ya Marko inataja ushauri aliotoa kwa wanafunzi, lakini haitaji utatu ambao umetajwa tu katika Mathayo, kama Marko anavyosema:

“Akawaambia, ‘Nendeni ulimwenguni kote mkaihubiri habari njema kwa viumbe vyote.


16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka, lakini asiyeamini atahukumiwa."

Marko 16:15

Hii inaonyesha kwamba wazo la utatu limeingizwa na sio asili
Kifungu hiki ni kitu ambacho kimeongezwa, kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa Magharibi pia:

1.

Wells asema hivi: “Si uthibitisho kwamba wanafunzi wa Kristo walikubali Utatu.”

2.

Adolf Harnack anasema katika kitabu chake The History of Dogma:

"Wazo hili la utatu ambalo linazungumza juu ya "Baba, Mwana na Roho Mtakatifu" ni jambo la kushangaza ambalo halikutamkwa kwenye midomo ya Kristo. Haikuwepo wakati wa Mitume. ... Zaidi ya hayo, haikutajwa kamwe hadi hatua ya baadaye katika ukuzaji wa mafundisho ya Kikristo na Kristo hakuzungumza kamwe juu yake alipokuwa akihubiri na kufundisha baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. Paulo pia hakujua jambo hilo, kwa sababu hakunukuu chochote alichodai kuwa kilitoka kwa Kristo ambacho kilihimiza kueneza Ukristo kati ya mataifa mengine.”

3.

Ukweli kwamba wazo hili halikuwa la asili linathibitishwa na wasomi wa Biblia na wanahistoria wa Ukristo, kama ilivyosemwa na Askofu Mkuu Cyril Salim Bustros -- Askofu Mkuu wa Kikatoliki wa Baalbek na viunga -- ambaye alisema:

“Wasomi wa Biblia wanafikiri kuna uwezekano mkubwa kwamba agizo hili ambalo Injili inasema lilitamkwa na Yesu halikutoka kwa Yesu mwenyewe; bali ilikuwa ni kanuni iliyosemwa kuwatayarisha watu kwa Ubatizo katika jamii ya Wagiriki. Ubatizo katika miaka ya mapema ya Ukristo ulitolewa ‘katika jina la Yesu Kristo’ [ Matendo 2:38; 10:48] au ‘katika jina la Bwana Yesu’ [ Matendo 8:16; 19:5]. Kwa hiyo wanahistoria wanaiona kuwa inaelekea zaidi kwamba kanuni ya ubatizo wa Utatu ilikuwa muhtasari mfupi wa kujitayarisha kwa ubatizo. Hivyo walienda mbali zaidi na kutia ndani jina la Yesu ‘Mungu Baba na Roho Mtakatifu’.”

Al-Laahoot al-Maseehi wa’l-Insaan al-Mu‘aasir (Uungu wa Kikristo na Mwanadamu wa Kisasa), Askofu Mkuu Cyrille Salim Bustros, 2/48

4.

Mwanahistoria Eusebius wa Kaisaria aliponukuu kifungu hiki cha Injili ya Mathayo, hakutaja humo “Baba” au “Roho Mtakatifu”; badala yake alisema: “Walikwenda katika mataifa yote ili kueneza Injili, wakitegemea nguvu za Kristo ambaye aliwaambia: ‘Nendeni mkawafundishe mataifa yote kwa jina langu.’”

Tareekh al-Kaneesah (Historia ya Kanisa), Eusebius wa Kaisaria, uk. 100

5.

Jambo lingine linalothibitisha hilo ni ukweli kwamba katika hati ya Kiebrania ya Injili ya Mathayo iliyogunduliwa hivi majuzi -- ambayo awali iliandikwa kwa Kiebrania -- maandishi haya hayapo. Hili lilizingatiwa na Dk G. Reckart, Profesa wa Theolojia katika Chuo cha Biblia cha Kitume cha Theolojia cha Kaufman, Texas, kama ushahidi wa uhakika kwamba kifungu hiki kimeongezwa kwenye Injili ya Mathayo. Alisema: “Kanisa Katoliki limedanganya kwa hiari kuhusu Mathayo 28:19 na Wakatoliki kwa ujumla (kutia ndani Othodoksi ya Mashariki) wameudanganya ulimwengu. Kila mtu aliyebatizwa kwa ubatizo huu wa uongo amekufa amepotea na bila wokovu.”

Dk. Reckart anatuambia juu ya idadi ya maandiko ya Agano Jipya ambayo yanazungumza juu ya ubatizo katika jina la Yesu Kristo pekee, kama katika maneno ya Petro katika mahubiri yake maarufu:

“Tubuni mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu. Nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”

Matendo 2:38

Wasamaria walibatiza kwa jina la Yohana Mbatizaji. Walipomsikia Paulo, “wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu” (Matendo 19:5). Paulo hakuwaomba wabatizwe kwa jina la Baba na Roho Mtakatifu; aliridhika na ubatizo katika jina la Yesu.

6.

Historia ya wanafunzi inathibitisha kwamba hawakuwa na ujuzi wa maandishi haya, kwa sababu hawakutoka kwenda kuwaita watu kama walivyoamrishwa na Kristo katika andiko hili linaloitwa; bali aliwaagiza waepuke kumwita yeyote isipokuwa Wayahudi.

(a)
“Hao kumi na wawili Yesu aliwatuma akiwapa maagizo yafuatayo: ‘Msiende kati ya watu wa Mataifa wala kuingia katika mji wowote wa Wasamaria.




6 Afadhali nendeni kwa kondoo waliopotea wa Israeli’”

Mathayo 10:5-6

(b)

Hilo lapatana na uthibitisho wa kihistoria unaorudi nyuma hadi karne ya pili W.K., ambao unapinga ule uitwao Utume Mkuu wa kuyaita mataifa na kuyabatiza katika jina la utatu, kama vile mwanahistoria wa kanisa Apollonius alivyosema: “Nilijifunza kutoka kwa wale waliotangulia. vizazi ambavyo Kristo, kabla ya kupaa kwake mbinguni, aliwaagiza Mitume wake wasiende mbali na Yerusalemu kwa miaka kumi na miwili.”

(c)

Wanafunzi walifuata maagizo ya Kristo na hawakuondoka Palestina isipokuwa hali iliwalazimu kufanya hivyo. "Na wale waliotawanyika kwa ajili ya mateso kwa ajili ya Stefano, wakasafiri hata Foinike, na Kipro, na Antiokia, wakihubiri ule ujumbe kwa Wayahudi tu" (Matendo 11:19). Kama wangemsikia Kristo akiwaagiza kuyaita mataifa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, wangetoka nje kwa kutii maneno yake, bila kipingamizi chochote, kuwaambia mataifa juu yake.

(d)
Petro alipoitwa na yule mpagani Kornelio ili kujua juu ya Ukristo kutoka kwake, kisha akawa Mkristo mikononi mwa Petro, wanafunzi wengine walipinga hilo, lakini akawaambia: “Akawaambia, Mnajua ya kwamba ni kinyume cha sheria yetu kwa Myahudi kushirikiana na mtu wa mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha nisimwite mtu awaye yote najisi au najisi” (Matendo 10:28). Lakini hakusema kwamba Kristo alikuwa amewaagiza kufanya hivyo; bali alisema: “… sisi tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.




42Akatuamuru tuwahubiri watu” (Matendo 10:41-42), yaani, kwa Wayahudi pekee. Aliporudi Yerusalemu, alikabiliwa na shutuma nyingi zaidi, “waumini waliotahiriwa wakamlaumu 3na kusema, ‘Uliingia katika nyumba ya watu wasiotahiriwa ukala pamoja nao!’ ( Matendo 11:2-3 ) . Ndipo Petro akaanza kuwaambia juu ya ndoto aliyoona ambayo ilihalalisha kula kwake pamoja na watu wa mataifa (Matendo 11:4-10). Naye akawaambia jinsi Roho Mtakatifu alivyomjia na kumwambia aende: “Roho akaniambia nisisite kwenda pamoja nao, akafuatana nami pia” (Matendo 11:12).

Baada ya hoja hii ya kina na yenye kusadikisha kutoka kwa Petro, wanafunzi walikubali kwenda kwake kwa wasiotahiriwa. “Waliposikia hayo hawakuwa na mapingamizi zaidi, wakamsifu Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata Mataifa toba liletalo uzima” (Matendo 11:18).

Kwa kuzingatia hilo, watu hawa wote, akiwemo Petro, hawakujua lolote kuhusu andiko la Mathayo linaloagiza kubatiza mataifa yote kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kwanini hivyo? Kwa sababu Kristo hakusema na wao hawakusikia. Kama Kristo angelisema, kusingekuwa na haja yoyote ya kulaumiwa na kukemewa.

7.

Zaidi ya hayo, Wanafunzi walikubaliana na Paulo kwamba atawaita watu wa mataifa mengine wakati wao watawaita waliotahiriwa, yaani Wayahudi. Paulo anasema:
“Badala yake, waliona kwamba nimekabidhiwa jukumu la kuhubiri injili kwa watu wa mataifa [lit. wasiotahiriwa], kama vile Petro alivyokuwa kwa Wayahudi [lit. waliotahiriwa].




8Kwa maana Mungu, ambaye alikuwa akifanya kazi katika huduma ya Petro akiwa mtume kwa Wayahudi, alikuwa akifanya kazi pia katika huduma yangu kama mtume kwa watu wa mataifa. 9Yakobo, Petro na Yohana, watu waliojulikana kuwa nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa ushirika, walipoitambua neema niliyopewa. Wakakubali sisi twende kwa Mataifa, na wao kwa Wayahudi”

Wagalatia 2:7-9.

Kwa hiyo wangewezaje kwenda kinyume na amri ya Kristo -- ikiwa andiko la Mathayo ni la kweli -- na kujiepusha kuwaita mataifa, kisha waachie hilo kwa Paulo na Barnaba pekee?

Mambo haya yote yanathibitisha maandishi katika Mathayo kuwa ya uwongo na yanathibitisha kwamba ni maandishi ya kutunga ambayo hayawezi kuhusishwa kikamilifu na Kristo.
Mambo unayofundishwa msikitini yanayohusu ukristo Uwe na tabia ya kuyapitia wewe binafsi na kuyachuja usiyabebe kama yalivyo maana yanakufanya unakuwa kama kasuku.Wallah nakwambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom