Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Nimeisoma tena kitabu kizima chenye pages zaidi ya 500 kikieleza mwanzo mwisho historia ya Qu'ran mpk kukusanywa na mambo mengine kuhusu Qu'ran kama uchambuzi ,aya zilizofutwa hukumu ,jinsi ilivyokusanywa Ktk lahaja na kwa nini iwe hivyo na nyingine kuteketezwa kila kitu nimesoma.

Vipi ulitaka kusemaje ?
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa hakuna kitabu kilichoshushwa wala nini na pia kwenye uandishi kuna mkono wa binadamu. Kwa sababu hiyo inawezekana kabisa kila kilichoandikwa kimetokana tu mawazo yao tu,wakaongeza wanayojua na kupunguza wanayoyataka na pengine zile Copy zilizochomwa ndo zilikuwa sahihi zaidi. Tena pengine labda zilizungumzia Yesu kusulubiwa msalabani.

Sasa kwa namna hii mna hakika gani na hicho kitabu ambacho mliaminishwa kuwa kimeshushwa kumbe kimeandikwa na watu tu miaka mingi baada ya Mtume kufa?Kitu gani kilitumika kutambua kwamba hizi zina makosa zichomwe na hii haina ibaki kuwa Quran iliyopitishwa?

Na je hii inaweza kuwa ndio sababu ya makosa mengi ya kihistoria na kisayansi ambayo tunayoana kwenye Quran?

Hebu tusaidie mwanazuoni.
 
Kwa hiyo tunakubaliana kuwa hakuna kitabu kilichoshushwa wala nini na pia kwenye uandishi kuna mkono wa binadamu. Kwa sababu hiyo inawezekana kabisa kila kilichoandikwa kimetokana tu mawazo yao tu,wakaongeza wanayojua na kupunguza wanayoyataka na pengine zile Copy zilizochomwa ndo zilikuwa sahihi zaidi. Tena pengine labda zilizungumzia Yesu kusulubiwa msalabani.

Sasa kwa namna hii mna hakika gani na hicho kitabu ambacho mliaminishwa kuwa kimeshushwa kumbe kimeandikwa na watu tu miaka mingi baada ya Mtume kufa?Kitu gani kilitumika kutambua kwamba hizi zina makosa zichomwe na hii haina ibaki kuwa Quran iliyopitishwa?

Na je hii inaweza kuwa ndio sababu ya makosa mengi ya kihistoria na kisayansi ambayo tunayoana kwenye Quran?

Hebu tusaidie mwanazuoni.
Kabla ya kukusanywa na kuandikwa kama msahafu walikuwepo maswahaba wengi tu ambao walihifadhi kitabu chote kutokana na vita vya mara kwa mara watu wengi waliohifadhi kuuwawa na kukatoka rai ikisanywe na kuandika kama kitabu kimoja ili isije kupotea baadae wakifa waliohifadhi wengi zaidi na hakuna hata aya moja ambayo iliyoongezwa wala kutolewa na maswahaba kama ipo weka ushahidi..

Zilizochomwa moto ni Lahaja nyingine za Qu'ran maana Qu'ran ilishuka katika Lahaja tofauti tofauti za lugha ya kiarabu hata Kenya Kiswahili chao "moja"wanaita "moya" lakini hapo maana sasa baada ya muda kupita ikafikia hatua watu kujisifu kuwa Qu'ran yao (yenye Lahaja yao) ni bora hadi kukawa na usomaji tofauti tofauti wa Qu'ran ili kuonda hilo ikatoka rai kuwa ikusanywe katika Lahaja Moja na kopi zipelekwe Ktk miji tofauti tofauti ya Uislamu na hiyo ndio itumike kufundisha na nyingine zikusaywe ziteketezwe ili kuondoa utofauti katika usomaji na kuleta umoja.

Kwa hiyo hakuna aya iliyofutwa na kupotezwa au kuteketezwa bali iliyoteketezwa ni Lahaja mbalimbali za Qu'ran..
 
hapana.
NABII Ibrahim hakuwa myahudi.
Jina la yahudi limetokea kipindi cha nabii MUSA.
yakubu aliitwa ISRAEL.
Ambaye alizaa watoto 12 ambao ndo kabila za wanna Israel.
 
Mkuu nakuomba hebu achana nao , hao wote wapo empty hakuna Mwenye IQ yoyote eti ulinganishe Qur-an na bibilia?, narudia hakuna kitabu cha dini kinacho kinachoelezea mwanadamu ninani ila Qur-an, sasa hao wanao mmfanya binaadamu (yesu) kuwa mungu ndio waliopotea hata hao ma royal wao (wayahudi) hawalikubali hili
Quran haijatoa jibu lolote kuhusu dhambi wala kumjua Mungu. Wewe kama umeamua kuikataa Biblia its your life and its your loss hakuna namna tutakusaidia.

Mungu hawezi kamwe kuwa less God kwa sababu watu fulani wamemkataa. Its your choice but consequences of your choices are not yours do decide.
Kabla ya kukusanywa na kuandikwa kama msahafu walikuwepo maswahaba wengi tu ambao walihifadhi kitabu chote kutokana na vita vya mara kwa mara watu wengi waliohifadhi kuuwawa na kukatoka rai ikisanywe na kuandika kama kitabu kimoja ili isije kupotea baadae wakifa waliohifadhi wengi zaidi na hakuna hata aya moja ambayo iliyoongezwa wala kutolewa na maswahaba kama ipo weka ushahidi..

Zilizochomwa moto ni Lahaja nyingine za Qu'ran maana Qu'ran ilishuka katika Lahaja tofauti tofauti za lugha ya kiarabu hata Kenya Kiswahili chao "moja"wanaita "moya" lakini hapo maana sasa baada ya muda kupita ikafikia hatua watu kujisifu kuwa Qu'ran yao (yenye Lahaja yao) ni bora hadi kukawa na usomaji tofauti tofauti wa Qu'ran ili kuonda hilo ikatoka rai kuwa ikusanywe katika Lahaja Moja na kopi zipelekwe Ktk miji tofauti tofauti ya Uislamu na hiyo ndio itumike kufundisha na nyingine zikusaywe ziteketezwe ili kuondoa utofauti katika usomaji na kuleta umoja.

Kwa hiyo hakuna aya iliyofutwa na kupotezwa au kuteketezwa bali iliyoteketezwa ni Lahaja mbalimbali za Qu'ran..
Kwa hiyo umekubali haikushushwa imeandikwa na watu. Pia Hakuna habari za Lahaja hapo kaka uliposoma wanajaribu tu kuficha ukweli. Kama Mungu aliamua zije kwa lahaja tofuati huyu aliyeamua aziomdoe yeye ni nani na mamlaka hayo katoa kwa Mungu au kajiamulia?

Kiufupi hakuwakuwa na changamoto za lahaja bali utofaauti wa idadi ya Aya na tafisiri ya baadhi ya aya ambazo nyingine zilikuwa zincontradicg mpaka Uislam wenyewe.
 
Anaandika Robert Heriel,

Ukristo na Uislam ni watoto wa baba mmoja aitwaye Uyahudi.
Licha ya kuwa Ukristo ulitangulia kabla ya Uislam lakini Uislam kwenye ishu ya maadili upo makini zaidi kuliko Ukristo, na dini hizo zote mbili baba yao ni dini ya Kiyahudi (Judaism).

Ukisema Ukristo ni mtoto mtundu au mkaidi aliyegundua mavumbuzi mengi hautokuwa unakosea. Labda kwa vile ni mtoto wa kwanza. Uislam ni lastborn wa Uyahudi ambao umeendelea kushika baadhi ya Falsafa na principles za baba yake.

Dini ni maadili ambayo yamejengwa kwa msingi wa imani. Kuamini katika miungu, lakini lengo kuu la dini ni ishu ya maadili.

Ukristo na Uislam hauwezi kusimama wenyewe bila kutegemea Uyahudi, hiyo haiwezekaniki kwani huyo ndiye baba yao. Hata hivyo kama utatazama kwa jicho lisilo la makengeza, unaweza kuona bila ya shaka kuwa Ukristo unahangaika kujitegemea wenyewe pasipo kufuata misingi ya baba yake Uyahudi.

Licha ya kuwa lastborn Uislam anaonekana kuwa alimpinga na hamtaki baba yake Myahudi lakini ukiangalia mtazamo na falsafa zake bado zinajikita kwa baba yake. Wakati huo Ukristo yeye kwa vile ni firstborn ambaye kisheria ndiye mrithi kwa nje anaonekana kumkubali baba yake Myahudi lakini kimatendo na kifalsafa anampinga baba yake.

Baada ya watoto kukua wanahama na kwenda kuanzisha miji yao. Ukristo boma/mji wake aliuita KANISA
Uislam boma/mji wake akauita MSIKITI. Wakazaliwa watoto, Ukristo ukazaa Wakristo wakati Uislam ukazaa watoto Waislam ambaye babu yao ni Uyahudi.

Falsafa chache za baba Uyahudi ukilinganisha na watoto wake wawili:
1. Mungu ni mmoja,
Ukristo hauamini katika Mungu mmoja isipokuwa mmoja katika utatu Mtakatifu. Baba, mwana, na roho mtakatifu.

Uislam unaungana na Baba yake Uyahudi kuwa Mungu ni mmoja na wapekee asiye na mshirika. Yaani hakuna cha utatu wala upili. Katika falsafa hii Ukristo unapingana na baba yake huku Uislam ukiungana na Baba yake.

2. Mungu ni mtakatifu/msafi
Ukristo: Mtoto huyu anasema kwa mdomo jambo hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu wa mwili na mavazi.

Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Ukristo umejijenga zaidi katika kanuni ya kusafisha ndani zaidi kuliko nje. Lakini umesahau kuwa uchafu unatokea nje kwenda ndani.

Ukristo unaruhusu mtu kula jambo lolote kwa imani, siyo ajabu Ukristo mtu kula nguruwe au panya au mbwa kwa sababu ni kwa imani.

Uislam: Mtoto huyu anasema mdomoni na kutekeleza kwa vitendo. Falsafa na kanuni hizi amezitoa kwa baba yake aitwaye Uyahudi. Mungu ni msafi/mtakatifu na anataka watu wake wawe watakatifu/wasafi.

Uislam umeiga tabia ya baba yake kugawa vitu visafi na vichafu. Kipi chafaa kula na kipi hakifai. Uislam hauwezi kula uchafu.

3. Ndoa na mahusiano.
Ukristo: Mtoto huyu amemuasi baba yake dhahiri shahiri. Uyahudi kuna sheria ya talaka lakini Ukristo kaamua kuiweka kapuni. Hii inafanya watu wawe watumwa kwenye mahusiano yasiyo na tija.

Ikiwa siyo lazima kuwa na mahusiano na Mungu iweje iwe lazima ukioa mke au kuolewa na mume muishi maisha yote? Ndoa ni mkataba wa hiyari kwasababu unahusu upendo. Upendo ni hiyari, kama watu watapishana waachane. Uyahudi unaeleza hivyo, Ukristo hautaki.

Ukristo huyu mtoto kapingana na baba yake. Uyahudi haukatazi mtu kuoa wake wengi, unaruhusu ndiyo maana kunasheria zinazohusu mtu atakayetaka kuoa wake wengi.
Ukristo hautaki na umepinga jambo hilo.

Uislam: Mtoto huyu licha ya kuonekana kama muasi kwa babaye lakini bado anatumia kanuni zilezile za baba yake.
Mtoto huyu anaruhusu Talaka kama kuna mambo yanaenda ndivyo alivyo. Pia mtoto huyu anaruhusu wake wengi ingawaje ameweka kikomo kuwa ni wake wanne.

4. Mavazi
Ukristo: Mtoto huyu anatumia u-firstborn wake vibaya. Ukristo unaruhusu mtu avae atakavyo kwani Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo wa mtu.
Siyo ajabu wafuasi wa Ukristo kuwaona wakivaa nguo zisizo na stara.

Hii ni tofauti na baba yake Uyahudi ambaye alikuwa na sheria za mavazi na kusisitiza watu wavae kwa adabu hasa wanawake wajistiri kutokana na maumbile yao kuwa na ushawishi.

Uislam: Mtoto huyu mwenye madeko ambaye yeye kila kitu lazima aone anaonewa, yeye anaungana na baba yake katika hilo. Uislam unazingatia maadili ya mavazi. Wafuasi wa mtoto huyo wamekuwa wastaarabu/waungwana sana katika hilo.

5. Mwanaume ndiye kuhani.
Ukristo: Ukristo kadiri siku zinavyoenda unazidi kuonyesha kupuyanga na kutumia urithi wa u-firstborn vibaya kama alivyofanya Esau. Ukristo unaruhusu mtu yeyote kuwa kuhani hata kama ni mwanamke. Wakati baba yake Uyahudi jambo hilo kwake kamwe lisingewezekana.

Nafasi ya mwanaume kwenye Ukristo huchukuliwa kuwa sawa na mwanaume. Wakati mzee Uyahudi hilo kwake lilikuwa ni ushetani.

Uislam: Ni kufuru kubwa kwa mtoto wa kike kusimama madhabahuni kuwahutubia wanaume. Hilo uislam alilichukua kama lilivyo na analitekeleza. Uislam umempa nafasi kubwa mwanaume kama ilivyo kwa baba yake Uyahudi.

6. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.
Ukristo: Unatanabaisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kupitia kwa Bikra Maria aliyepewa mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Hoja hii ndiyo mzizi wa utatu mtakatifu na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu, ilhali hilo kamwe hata kwa akili ya panzi haliwezekaniki.

Baba yao Uyahudi kama ungesikika ukisema maneno hayo, basi ilikuwa umeamua kutaka kuuawa kwa kupiga mawe kwani ungekuwa umekufuru na kufanya dhambi kubwa mno.

Uislam: Mtoto huyu yeye anabaki na msimamo wa baba yake kuwa Mungu hajazaa wala hajazaliwa. Na Hilo ni kosa kubwa la kukufuru.

7. Neema
Ukristo: Ukristo huu ndiyo msingi namba moja yaani huwezi tenganisha Ukristo na neema.
Kwamba mtu akifanya kosa basi anastahili kupewa nafasi ya pili, neema pasipo kuhukumiwa.
Wakati baba yake Uyahudi yeye kanuni yake ni haki. Kwamba mtu akikosea basi aadhibiwe, na mtu akipatia basi apewe zawadi yake (thawabu).

Uyahudi ulijikita kwenye mwili na roho. Wakati Ukristo unajikita katika roho pekee. Hii ni kumaanisha kinachopewa neema ni roho sio mwili. Yaani mtu akiomba neema ya msamaha, basi roho yake ndio ipewe second chance lakini mwili uadhibiwe.

Lakini wafuasi wa Ukristo wakalazimisha kuwa mwili na roho vyote vipewe neema[emoji23][emoji23]. Huku wakishikilia kanuni isemayo usihukumu usije ukahukumiwa au samehe saba mara sabini. Wakisahau kuwa mwili ndio unafanya makosa wakati huo roho ndiyo hufanya dhambi[emoji23][emoji23]. Mwili huadhibiwa na dunia kwa makosa yake wakati huohuo roho huadhibiwa na Mungu kwa dhambi zake.

Uislam: Mtoto huyo yeye kafuatisha kwa kiasi kikubwa kanuni na sheria na falsafa za baba yake. Mwenye makosa aadhibiwe kulingana na makosa yake na vile sheria zisemavyo.

Zingatia, binadamu hawezi kusamehe dhambi isipokuwa Mungu. Ila anasemehe makosa kwa sababu ya mwili ndiyo hufanya makosa na roho ndiyo itendayo dhambi. Kumaanisha, roho ndiyo inamuasi Mungu halafu mwili unamfanyia makosa binadamu mwenzako au kiumbe au mazingira yanayokuzunguka.

8. Hukumu
Ukristo: Mtoto huyu anajieleza kuwa atakayehukumu ulimwengu ni Kristo/Yesu.
Na Yesu ndiye atakuwa mtawala wa kila kitu. Hii ni tofauti na falsafa ya baba mtu Uyahudi. Yeye anajua Mungu ndiye mtawala na ndiye atakayehukumu viumbe vyake kwa haki. Zingatia neno viumbe inamaanisha vinavyoonekana na visivyoonekana. Hata Yesu pia ni kiumbe.

Uislam: Huyu mtoto anaungana na baba yake Uyahudi kwa kusema, hukumu atakayoitoa ni Mungu. Na kila kiumbe atahukumiwa kulingana na yale aliyoyafanya.

9. Urithi na mirathi
Ukristo: Umejikita zaidi katika mambo ya kiroho na kusahau mambo ya kimwili. Ukristo unajikita katika urithi wa Ufalme wa mbinguni pekee. Ilhali baba yake akijikita kwa yote mawili.
Uyahudi ilitoa utaratibu wa namna ya kurithisha mali kwa haki, na namna ya kutoa mirathi endapo mtu atakufa.

Ukristo jambo hilo limeachwa liamuliwe kidunia, hapohapo dunia kwa mujibu wa Ukristo inaongozwa na shetani[emoji23][emoji23]. Unaona mambo hayo!

Uislam: Mtoto huyu kamuiga baba yake na kuongeza baadhi ya vitu. Kajikita kiroho na kimwili.
Urithi na mirathi kwa uislam imefafanuliwa namna itakavyogawiwa. Uislam haujaliacha jambo hilo liamuliwe na walimwengu kwani shetani ndiye mlimwengu mwenyewe.

Mpaka hapo sina la ziada, siyo kazi yangu kukuambia kipi chakuamini au kipi ni sahihi na kipi sio sahihi. Nilikuwa naeleza habari za watoto hao wawili wenye wafuasi wengi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Uzi umeenda class huu
 
Braza angu alinipa hadithi ya Yacobo na Yusuph nikiwa chalii tukisubiri gemu za Uefa nilimuelewa sana akasema hao ni ndugu na hata hapa unaona wanatofautiana sana ni kwa kuwa wengi hawana uelewa wa hizi dini zetu wamekaririshwa kuchukiana wakati ni ndugu moja...baadae nikafatilia kwenye Biblia nikakuta ni kitu kile kile hata mitume wengi ni wale wale...
Ni walewale sawa ila biblia ewaelezea kwa utofauti ukilinganisha na uislam
 
Roho zidanganyazo zimekupata. Nadhani utakuwa umetembelewa na jibril. Uwe makini maana jibril alimkaba muhammad kule mapangoni hadi akarudi kwa Khadija akiomba afunikwe na mablanketi.

Jibril alikuwa anamlazimisha asome kitabu. Alikuwa hajui kama Muhammad alikuwa illiterate? Hicho kitabu ni kipi hasa wakati quran haikuwepo?

Yesu Kristo ndiye Mungu wa milele, muumba wa mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Makasikiko yameanza hoooo
 
Uislamu imeibuka tu ukiwa na mafundisho yake wenyewe.

Ukristo ni mwendelezo wa dini ya Kiyahudi ndio maana wote wanatumia kitabu cha Biblia na kuamini manabii wake wote.

Baadhi ya mambo mapya ya Uislamu ni pamoja na

1.Kuyashirikisha Majini kwenye dini ya Kiislamua. (hili ni la ajabu zaidi)

2. Kuimba Shahada.

3. Kutufu, yaani ibada ya kulizunguka, kulirushia mawe na kulisujudia Jiwe Jeusi. linaloitwa Aswadi na kuliamini kwamba linasamehe dhambi

4. Kuhiji Maka.

5. Kufunga Ramadhani.

6. Kutawadha kama sehemu ya ibada

7. Kuimba adhana kama sehemu ya Ibada.

8. Mavazi kama sehemu ya ibada.

9. Kuswali, kutwa mara tatu, na aina za kuswali kama kupiga rakaa.

10. Kumswalia mtume Muhammadi

11. Kuswali kugeukia Maka

12. Kuswali kwa Kiarabu tu

13. Ibada ya jengo la Al-Kaaba.

Nk.

Hayo mambo hayakuwepo wakati wa Manabii wa zamani hadi katika Ukristo. Ni mambo yaliyoibuka na Uislamu.

Hakuna ushahidi wa Kihistoria Uyahudi kuzaa Uislamu. Wala Mtoto wa Ibrahim Ishmael kuwa Waarabu.

Watoto wa Ishmaeli waliitwa Waishmaeli na ndio waliomnunua Yusuf toka kwa ndugu zake.

Mwanzo 37:26 Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake?

27 Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali.

Na Waarabu walijuikana kama Waarabu hivyo hivyo, ni makabila mawili tofauti kabisa.

2 Mambo ya Nyakati 26:7
Mungu akamsaidia juu ya Wafilisti, na juu ya Waarabu waliokaa Gur-baali, na juu ya Wameuni.

(Wayahudi na Wakristo walimkataa Muhammadi kutokana na mafundisho yake yasiyolingana na Manabii wao, kama sivyo basi leo hii qurani ingekuwa sehemu ya Biblia kama Injiri)
 
Tuoneshe hayo mafundisho yenu yaliibukia wapi kuabudu Miungu watatu huko nyuma.

Itakuwa haufatilia bali una hadithiwa kanisani. Wayahudi wanatumia agano la kale na tanakh, sio hili agano jipya mnalobadilisha kila siku. Pia wanawalaumu kuwabadilishia tafsiri ya agano la kale, wanaamini huyo mnayemwita Yesu mtoto wa zinaa. Utuambia wayahudi wa wapi wanamkubali Yesu.

Mwenyezi Mungu aumbe majini halafu ayape adhabu wote bila kosa la nani kafanya, huyo Mwenyezi Mungu atakuwa sio msamehevu.
Mbona binadamu kamkosea na nyie mnaamini kamuua mtoto wake? Logic yako ipo wapi?

Kuimba shahada ndiyo nini? Waulizeni kanisani wawatolee ufafanuzi msiwe vituko

Hilo kulisujudia na kusamehe dhambi mmetoa kwenye nukuu gani?
Ibada ya kukata viuno na kucheza hayo mafundisho nyie mlitoa wapi?

Hiyo kawaida imewekwa kwa mwenye uwezo. Hakuna logic ya kuona tatizo ukitaka nenda kazuru Jerusalem

Mbona unaonekana mweupe sana kijana. Ibada ya funga ipo kitambo sana mtume mwenyewe ameikuta.
Usipende kula ovyo ovyo kwani funga ina faida kiafya.

Kijana biblia huwa unasoma kweli? Ukisikia kutawadha unaelewa kitu gani inaelekea hata maana haujui kuna kitu umemezeshwa.

Hiyo kawaida kwenye kuita kwenye sala hakuna mantiki. Haujajiuliza kwenye masuala ya kengele mmetoa wapi?

Mavazi ni muhimu hauwezi kwenda nyumba ya ibada kama unaenda club. Kwa kuvaa vimini au kichupi.

Hata idadi ya kuswali haufahamu. Mara tano kwa siku. Huku hakuna uvivu. Hii sio dini ya kisiasa na uvivu kubadilisha vipengele ili fulani aweze.

Kumswalia ni kitu cha kawaida. We ulitaka wamswalie Yesu. Inaelekea hata maana hauelewi.


We ulitaka kuelekea Jerusalem? Ndiyo utaratibu uliowekwa na Mwenyezi Mungu. Kila kitu kimewekwa sheria zake.

Hiyo ni nzuri kwa sababu inatuunganisha hata nikiwa nchi yoyote. Wewe ukienda china, India au France. Itabidi ukae nyumbani au utafute kanisa linaloongea kingereza.

Ulichokiandika umekielewa?

Tutajie manabii wa zamani unaowajua wewe waliokuwa wanasema kwa jina la baba, mwana na roho mtakatifu.
Waliokuwa wanaimba na kucheza kwenye makanisa, waliokuwa hawasujudu, waliokuwa wanaweka misalaba nyumba za ibada, waliokuwa wanachanganya wanawake na wanaume nyumba ya ibada na kuvaa wanavyotaka wao,
n.j



Kuandika neno injili unashindwa neno ambalo la kawaida. Inaelekea hata sio msomaji bali mtu kuhadithiwa na kunukuu aya kibubusa. Sio ajabu mnadanganywa ovyo ikiwa kuandika neno kama hilo haujui
Nadhani umeelewa vya kutosha.
Hata Ibirisi yaani Shetani nao ni viumbe wa Mungu.
Na ni Muhamadi pekee aliye fanikisha kumsilimisha Ibirisi yaani Shetani Lucifer na wenzake na kuwa Muislamu kama waislamu Watu na Majini.

Kwakuwa wote ni viumbe wa Mwenyezi Mungu.
 
Shetani ni sifa. Kama kwenye biblia Yesu alimwita Petro Shetani. Ukifanya mambo ya ovyo maana yake ni shetani.
Tunarudi tena kwenye biblia utueleze majini sifa yake.
Kwa nini wakifanya makosa wasisamehewe wakati binadamu walifanya makosa na kutolewa mtu atundikwe ili msamehewe?
Hilo swali ni rahisi. Unipe majibu kwa maandiko sio porojo.
Neno Shetani linatokana na neno Satan kwa Kiingereza.
Hebu google "Satan" halafu uje unipe mrejesho.
Mtaongopewa hadi akili iwakae sawa.

Kwahiyo unataka kuniambia Muhammadi ndio alimsilimisha huyo unaye mwita Ibirisi na kwa sasa ni Muislamu safi kabisa.
Kwakuwa naye ni kiumbe wa Mungu sio
 
Church fathers wamekudanganya hadi huruma. Shetani limetokana na neno la kiarabu.
Ukitamkiwa kiarabu na kingereza neno gani linafanana ndiyo utajua.
Muwe mnasoma vijana kuliko kuleta ushabiki haitokusaidia.
Kila kitu usigoogle ovyo bila kutumia akili. Kuna vyanzo vingine utaambiwa ulikuwa nyani na kukubali bila akili.
Kila kitu mnawaza kiarabu tu.

Mimi namtambua Shetani huyu hapa kwenye Biblia, ambaye anaitwa Satan kwa kiingereza.
Wewe baki na hiyo sifa ya Kiarabu

Ayubu 2:7 Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.

Mathayo 4:10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
 
Hakuna kitabu chochote unachojua wewe kimempinga shetani kuliko Qur'an. Aya za namna hiyo zipo nyingi kuliko unavyofikiria
Hizi verse hauwezi kuzijua kwa sababu unagoogle kwa wapotoshaji wenzako.

Enyi watu! Kuleni vilivyomo katika ardhi, halali na vizuri, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye ni adui yenu aliye dhaahiri.
(Qur'an 2:168)
Sahih al-Bukhari 3271

Narrated Ibn `Abbas:

The Prophet (ﷺ) said, "If anyone of you, when having sexual relation with his wife, say: 'In the name of Allah. O Allah! Protect us from Satan and prevent Satan from approaching our offspring you are going to give us,' and if he begets a child (as a result of that relation) Satan will not harm it."



Sahih Muslim 2366 b

This hadith has been narrated on the authority of Zuhri with the same chain of transmitters (and the words are):

" The newborn child is touched by the satan (when he comes in the world) and he starts crying because of the touch of satan." In the hadith transmitted on the authority of Shu'aib there is a slight variation of wording.
 
Upande ulipokaa nimepaona kaka!!..La msingi Acha ku-act uko neutral sifu na pongeza upande wako...
 
Sahih al-Bukhari 3271

Narrated Ibn `Abbas:

The Prophet (ﷺ) said, "If anyone of you, when having sexual relation with his wife, say: 'In the name of Allah. O Allah! Protect us from Satan and prevent Satan from approaching our offspring you are going to give us,' and if he begets a child (as a result of that relation) Satan will not harm it."



Sahih Muslim 2366 b

This hadith has been narrated on the authority of Zuhri with the same chain of transmitters (and the words are):

" The newborn child is touched by the satan (when he comes in the world) and he starts crying because of the touch of satan." In the hadith transmitted on the authority of Shu'aib there is a slight variation of wording.
Baeleze baeleze baelewe
 
Uzi wako ni WA akili ndogo ila nitazungumzia jambo Moja TU la talaka hasa talaka yenu waislam talaka ya tatu,,, kwamba ukimpa mwanamke talaka ya tatu inatakiwa aolewe na mwanaume mwengine aachwe Tena ndio umrudie,,hiki ni kioja na mtu asieelewa maana ya huo uchafu ndie anaweza kusema kwamba ukristo na uislam Zina msingi wa wayahudi,,,kitu Cha kukusaidia ni kwamba uislam una msingi kwa wakureish na pia waliokuwepo wakiabudu kwa taratibu za kiislam kabla yenu mmewaita majahilia / wajinga lakini mmecopy na kupesti taratibu zao zote za ibada,,usidanganye watu dada Robert heriel
 
Uyahudi umezaa Judaism/uyahudi kama dini na Ukristo,,ukiona unahangaika na vijitopic vya kipuuzi kama Yesu sio Mungu,,Mungu hazai,,Paulo alikuwa shoga,,issa,,nguruwe ngamia nk nk nk una tatizo la paradox huelewi kwako ni wapi (where you belong) na kibaya zaidi mmeshindwa kuijua misingi ya dini yenu hasa kutokana na kwamba imeandikwa kwa kiarabu
 
Labda itabidi tufike mahali tuanza kuwapa wenzetu Hawa maana ya sura/chapter zao za Quran kama surat Al baqara=Sura ya Ng'ombe,,,
surat Al nisaa = sura ya wanawake,,surat Al jinn = Sura ya majini,,Sural Al namli = Sura ya mchwa/sisimizi nk nyengine zitafuata
 
Labda itabidi tufike mahali tuanza kuwapa wenzetu Hawa maana ya sura/chapter zao za Quran kama surat Al baqara=Sura ya Ng'ombe,,,
surat Al nisaa = sura ya wanawake,,surat Al jinn = Sura ya majini,,Sural Al namli = Sura ya mchwa/sisimizi nk nyengine zitafuata.

Meanings of 114 Surahs of Quran

List of 114 Surahs of Quran with meaning.
Fatehah-The Opening
Baqarah-The Cow
Al-Imran-The Family of Imran
NisaaThe -Women
MaidahThe -Table spread with Al-Anaam-The Cattle
Al-AraafT-he wall with Elevations
Al-Anfaal-The Spoils of War
Tawbah-The Repentance
Yunus-The Prophet [Jonah]
Hud-The Prophet Hood
Yusouf-The Prophet [Joseph]
Al-Ra’ad-The Thunder
Ibrahim-The Prophet [Abraham]
Hijr-The Rocky Tract
Nahl-The Bee
Israa-The Journey by Night
Al-Kahf-The Cave
Maryam- Mary (Mother of Issa)
Taha- One of the Names of Prophet Muhammad
Al-Anbiya-The Prophets
Al-Hajj-The Pilgrimage
Al-Muminun-The Believers
Al-Nur-The Light
Al-Farqan-The Criterion
Ash-Shu’ara-The Poets
Al-Naml-The Ant
Al-Qasas-The Narration
Al-Ankabut-The Spider
Al-Rum-The Romans
LuqmanLuqman (A wise Man)
As-Sajdah-The Prostration
Al-Ahzab-The Confederates
Al-SabaSheba- (The Queen)
Al-Fatir-The Originator of Creation
Ya’sin- One of the Names of Prophet Muhammad
As-Saffat-Those Ranged in Ranks
SuadArabicAlphabet
Az-Zamar-The Groups
Al-Mumin-The Forgiver/The Believer
Hamim SajdahIn Detail
Ash-Shura-The Consultations
Al-Aukhruf-The Gold Adornment
Al-Dukhan-The Smoke
Al-Jathiyah-The Kneeling
Al-Ahqaf-The Curved-Sand Hills
Muhammad-The Prophet Muhammad
Al-Fath-The Victory
Al-Hujurat-The Dwellings Q’afArabic Alphabet
Al-Dhariyat-The wind that Scatters
Al-Tur- The Name of Mountain
Al-Najm-The Star
Al-Qamr-The Moon
Ar-Rahman-The Most Gracious
Al-Waqiah-The Event
Al-HadidIron
Al-Mujadila-The Disputation
Al-Hashr-The Gathering
Al-MumtahanaThe Woman to be Examined
As-Saff-The Row or The Rank
Al-JumahFriday
Al-Munafiqun-The Hypocrites
Al-Taghabun-Mutual Loss or Gain
Al-Talaq-The Divorce
Al-Tahrim-The Prohibition
Al-Mulk-Dominion
Al-Qalam-The Pen
Al-Haqqah-The Inevitable
Al-Maarij-The Way of Ascent
Noah-The Prophet Noah
Al-J’nn- The Genie, Demons
Al-Muzammil-The One wrapped in Garment
Al-Mudashir-The One Enveloped
Al-Qiyamah-The Resurrection
Al-Dahr-The Man
Al-Mursalat-Those Sent Forth
Al-Naba-The Great News
Al-Naziat-Those Who Pull Out
Al-Abasa-The Frowned
Al-Takwir-Wound Round and Lost its Light
Al-Infitar-The Cleaving
Al-Mutaffafin-Those Who Deal in Fraud
Al-Inshiqaq-The Splitting Asunder
Al-Bhruj-The Big Stars
Al-Tariq-The Night-Comer
Al-A’la-The Most High
Al-Ghashiya-The Overwhelming
Al-Fajr-The Break of the Day/The Dawn
Al-Balad-The City
Ash- Shams-The Sun
Al-Lail-The Night
Al-Duha-The Forenoon after Sunrise
Al-Inshira-The Opening Forth
Al-T’in-The Fig
Al-Alaq-The Clot
Al-Qadr-The Night of Decree (A blessed night)
Al-Beyinnah-The Clear Evidence
Al-Zilzal-The Earthquake
Al-Aadiyat-Those Who Runs
Al-Qariah-The Striking Hour
Al-Takatur-The Pilling up of Emulous Desire
Al-Asr-The Time
Al-Humazah-The Slanderer
Al-Fil-The Elephant
Al-Qureysh- The Famous Arab Tribe
Alma’un-The Small Kindnesses
Kauthar-A River in Paradise
Al-Kafirun-The Disbelievers
Al-Nasr-The Help
Al-Lahab-The Palm Rope
Al-Ikhlas-The Purity
Al-Falaq-The Day Break
Al-Nas-The People

Islamic Info

Back to top
 
Back
Top Bottom