Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Nachojua, El alikua mungu wa caanan, Abraham amekuja caanan ndipo akaanza kuabudu mungu wa caanan,, Abraham siyo myahudi wala hajawahi kuabudu dini ya kiyahudi, dini ya kiyahudi imeanza baada ya waisrael kurudishwa toka utumwani babel na mfalme wa persia, cyrus,, ambae ndie aliwajengea hekalu na kutuma waalimu kuwafundisha dini,
Moses siyo mwanzilishi wa dini ya kiyahudi,, dini ya kiyahudi inaabudu mungu tofauti na El,, wao wanaabudi yahwew,,
Moses alupikimbilia jeddah baada ya kumuua mtumishi wa farao,, alikwenda akajiunga na dini iliyokua ikiabudiwa na wa medianite aliejulikana kama yahwew,,
Hawa wa median ni uzao wa mke wa tatu wa Abraham aliekua akiitwa , Kedari,
Baba mkwe wa moses ndiyo aliembatiza moses kufuata imani ya wa median,
Uyahudi ni dini iliyoibuka kwa kuchanganya imani mbalimbali za kijadi za mesopotamia
Elungata unaweza kunipa maandiko kibibloa yakimtaja Ibrahimu kumwabudu El?
Niko hapa ninasubiri
 
Anzia hapa.
Kuna mahali uko sahihi na kuna mahali umechanya

Post yako inazua mjadala mpya.
Je tunajua maana ya NABII NA MTUME?

tukijibu hili tutajua Yesu ndiye?

Yesu akawaambia, “kila mtu humheshimu nabii isipokuwa watu wa mji wa kwao mwenyewe, jamaa zake mwenyewe na wale wa nyumbani mwake mwenyewe.” Marko 6:4

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.
Mathayo 10.40-41

Yeye mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni Nabii. Je, nini mawazo ya wale wafwasi wake waliomuamini na wakamwona na wakaishi naye? Injili zinatwambia:

Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
Yohana 6.14

Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
Mathayo 21.46

Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

Mathayo 21.10-11

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, ni Maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda mbele za Mungu na watu wote.
Luka 24.13-19

Injili kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.

"Hakika huyu ni nabii", anasema Yohana.

"waliwona kuwa nabii", anasema Mathayo.

"Huyu ni yule nabii, Yesu", anasema tena Mathayo.

"Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii", anasema Luka.
 
Nachojua, El alikua mungu wa caanan, Abraham amekuja caanan ndipo akaanza kuabudu mungu wa caanan,, Abraham siyo myahudi wala hajawahi kuabudu dini ya kiyahudi, dini ya kiyahudi imeanza baada ya waisrael kurudishwa toka utumwani babel na mfalme wa persia, cyrus,, ambae ndie aliwajengea hekalu na kutuma waalimu kuwafundisha dini,
Moses siyo mwanzilishi wa dini ya kiyahudi,, dini ya kiyahudi inaabudu mungu tofauti na El,, wao wanaabudi yahwew,,
Moses alupikimbilia jeddah baada ya kumuua mtumishi wa farao,, alikwenda akajiunga na dini iliyokua ikiabudiwa na wa medianite aliejulikana kama yahwew,,
Hawa wa median ni uzao wa mke wa tatu wa Abraham aliekua akiitwa , Kedari,
Baba mkwe wa moses ndiyo aliembatiza moses kufuata imani ya wa median,
Uyahudi ni dini iliyoibuka kwa kuchanganya imani mbalimbali za kijadi za mesopotamia
Je? Ibrahim alienda kaanani mwenyewe au aliitwa? Kama alienda mwenyewe kwa nini kizazi chake hakikumfuata huyo Mungu wa kusadikika wa kanani?

Kama aliitwa na akaambiwa atoke nchi yake ya Iraq aende caanani ni kwa nini afike caanani aache kumfuata Mungu aliemuita afuate kijimungu Cha kaanani??

Narudia kukuomba,,,nataka unionyeshe jina la Yehova,,Yahwe,,shadai,, Adonai katika miongoni mwa majina 99 ya Allah Subhana Wataalah.
 
Yesu akawaambia, “kila mtu humheshimu nabii isipokuwa watu wa mji wa kwao mwenyewe, jamaa zake mwenyewe na wale wa nyumbani mwake mwenyewe.” Marko 6:4

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.
Mathayo 10.40-41

Yeye mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni Nabii. Je, nini mawazo ya wale wafwasi wake waliomuamini na wakamwona na wakaishi naye? Injili zinatwambia:

Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
Yohana 6.14

Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
Mathayo 21.46

Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

Mathayo 21.10-11

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, ni Maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda mbele za Mungu na watu wote.
Luka 24.13-19

Injili kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.

"Hakika huyu ni nabii", anasema Yohana.

"waliwona kuwa nabii", anasema Mathayo.

"Huyu ni yule nabii, Yesu", anasema tena Mathayo.

"Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii", anasema Luka.
Usiwe unakurupuka kujibu.
Una copy na ku paste hapa...
Tunachambua hoja hayo mengine tunayajua
 
Usiwe unakurupuka kujibu.
Una copy na ku paste hapa...
Tunachambua hoja hayo mengine tunayajua

Mimi nimekuwekea aya zinazosema yesu ni nabii ; na mtume , ulitaka nitowe maneno yangu ??
 
Elungata unaweza kunipa maandiko kibibloa yakimtaja Ibrahimu kumwabudu El?
Niko hapa ninasubiri
Soma kisa cha Abraham wanapokutana na mtawala wa wafilist na mkuu wa mji wa jerusalem,, Melkizedeki,,
Melkizedeki ndio aliemu introduce Abraham kwa mungu mkuu wa Canaan El,,
Ndio maana hata mtoto wake wa kwanza akamwita Ishmael, ambalo lina maana moja na ismail.. 🤷🏼‍♂️,
Anyway ntakutafutia andiko la mkutano wa abraham na melkizedeki,
 
Mimi nimekuwekea aya zinazosema yesu ni nabii ; na mtume , ulitaka nitowe maneno yangu ??
Mimi nilitaka tujadili neno nabii na mtume.
Wengi hawajui maana yake ndio maana wanapinga unabii na utume wa Yesu
 
Anaandika Robert Heriel,

Ukristo na Uislam ni watoto wa baba mmoja aitwaye Uyahudi.
Licha ya kuwa Ukristo ulitangulia kabla ya Uislam lakini Uislam kwenye ishu ya maadili upo makini zaidi kuliko Ukristo, na dini hizo zote mbili baba yao ni dini ya Kiyahudi (Judaism).

Ukisema Ukristo ni mtoto mtundu au mkaidi aliyegundua mavumbuzi mengi hautokuwa unakosea. Labda kwa vile ni mtoto wa kwanza. Uislam ni lastborn wa Uyahudi ambao umeendelea kushika baadhi ya Falsafa na principles za baba yake.

Dini ni maadili ambayo yamejengwa kwa msingi wa imani. Kuamini katika miungu, lakini lengo kuu la dini ni ishu ya maadili.

Ukristo na Uislam hauwezi kusimama wenyewe bila kutegemea Uyahudi, hiyo haiwezekaniki kwani huyo ndiye baba yao. Hata hivyo kama utatazama kwa jicho lisilo la makengeza, unaweza kuona bila ya shaka kuwa Ukristo unahangaika kujitegemea wenyewe pasipo kufuata misingi ya baba yake Uyahudi.

Licha ya kuwa lastborn Uislam anaonekana kuwa alimpinga na hamtaki baba yake Myahudi lakini ukiangalia mtazamo na falsafa zake bado zinajikita kwa baba yake. Wakati huo Ukristo yeye kwa vile ni firstborn ambaye kisheria ndiye mrithi kwa nje anaonekana kumkubali baba yake Myahudi lakini kimatendo na kifalsafa anampinga baba yake.

Baada ya watoto kukua wanahama na kwenda kuanzisha miji yao. Ukristo boma/mji wake aliuita KANISA
Uislam boma/mji wake akauita MSIKITI. Wakazaliwa watoto, Ukristo ukazaa Wakristo wakati Uislam ukazaa watoto Waislam ambaye babu yao ni Uyahudi.

Falsafa chache za baba Uyahudi ukilinganisha na watoto wake wawili:
1. Mungu ni mmoja,
Ukristo hauamini katika Mungu mmoja isipokuwa mmoja katika utatu Mtakatifu. Baba, mwana, na roho mtakatifu.

Uislam unaungana na Baba yake Uyahudi kuwa Mungu ni mmoja na wapekee asiye na mshirika. Yaani hakuna cha utatu wala upili. Katika falsafa hii Ukristo unapingana na baba yake huku Uislam ukiungana na Baba yake.

2. Mungu ni mtakatifu/msafi
Ukristo: Mtoto huyu anasema kwa mdomo jambo hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu wa mwili na mavazi.

Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Ukristo umejijenga zaidi katika kanuni ya kusafisha ndani zaidi kuliko nje. Lakini umesahau kuwa uchafu unatokea nje kwenda ndani.

Ukristo unaruhusu mtu kula jambo lolote kwa imani, siyo ajabu Ukristo mtu kula nguruwe au panya au mbwa kwa sababu ni kwa imani.

Uislam: Mtoto huyu anasema mdomoni na kutekeleza kwa vitendo. Falsafa na kanuni hizi amezitoa kwa baba yake aitwaye Uyahudi. Mungu ni msafi/mtakatifu na anataka watu wake wawe watakatifu/wasafi.

Uislam umeiga tabia ya baba yake kugawa vitu visafi na vichafu. Kipi chafaa kula na kipi hakifai. Uislam hauwezi kula uchafu.

3. Ndoa na mahusiano.
Ukristo: Mtoto huyu amemuasi baba yake dhahiri shahiri. Uyahudi kuna sheria ya talaka lakini Ukristo kaamua kuiweka kapuni. Hii inafanya watu wawe watumwa kwenye mahusiano yasiyo na tija.

Ikiwa siyo lazima kuwa na mahusiano na Mungu iweje iwe lazima ukioa mke au kuolewa na mume muishi maisha yote? Ndoa ni mkataba wa hiyari kwasababu unahusu upendo. Upendo ni hiyari, kama watu watapishana waachane. Uyahudi unaeleza hivyo, Ukristo hautaki.

Ukristo huyu mtoto kapingana na baba yake. Uyahudi haukatazi mtu kuoa wake wengi, unaruhusu ndiyo maana kunasheria zinazohusu mtu atakayetaka kuoa wake wengi.
Ukristo hautaki na umepinga jambo hilo.

Uislam: Mtoto huyu licha ya kuonekana kama muasi kwa babaye lakini bado anatumia kanuni zilezile za baba yake.
Mtoto huyu anaruhusu Talaka kama kuna mambo yanaenda ndivyo alivyo. Pia mtoto huyu anaruhusu wake wengi ingawaje ameweka kikomo kuwa ni wake wanne.

4. Mavazi
Ukristo: Mtoto huyu anatumia u-firstborn wake vibaya. Ukristo unaruhusu mtu avae atakavyo kwani Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo wa mtu.
Siyo ajabu wafuasi wa Ukristo kuwaona wakivaa nguo zisizo na stara.

Hii ni tofauti na baba yake Uyahudi ambaye alikuwa na sheria za mavazi na kusisitiza watu wavae kwa adabu hasa wanawake wajistiri kutokana na maumbile yao kuwa na ushawishi.

Uislam: Mtoto huyu mwenye madeko ambaye yeye kila kitu lazima aone anaonewa, yeye anaungana na baba yake katika hilo. Uislam unazingatia maadili ya mavazi. Wafuasi wa mtoto huyo wamekuwa wastaarabu/waungwana sana katika hilo.

5. Mwanaume ndiye kuhani.
Ukristo: Ukristo kadiri siku zinavyoenda unazidi kuonyesha kupuyanga na kutumia urithi wa u-firstborn vibaya kama alivyofanya Esau. Ukristo unaruhusu mtu yeyote kuwa kuhani hata kama ni mwanamke. Wakati baba yake Uyahudi jambo hilo kwake kamwe lisingewezekana.

Nafasi ya mwanaume kwenye Ukristo huchukuliwa kuwa sawa na mwanaume. Wakati mzee Uyahudi hilo kwake lilikuwa ni ushetani.

Uislam: Ni kufuru kubwa kwa mtoto wa kike kusimama madhabahuni kuwahutubia wanaume. Hilo uislam alilichukua kama lilivyo na analitekeleza. Uislam umempa nafasi kubwa mwanaume kama ilivyo kwa baba yake Uyahudi.

6. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.
Ukristo: Unatanabaisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kupitia kwa Bikra Maria aliyepewa mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Hoja hii ndiyo mzizi wa utatu mtakatifu na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu, ilhali hilo kamwe hata kwa akili ya panzi haliwezekaniki.

Baba yao Uyahudi kama ungesikika ukisema maneno hayo, basi ilikuwa umeamua kutaka kuuawa kwa kupiga mawe kwani ungekuwa umekufuru na kufanya dhambi kubwa mno.

Uislam: Mtoto huyu yeye anabaki na msimamo wa baba yake kuwa Mungu hajazaa wala hajazaliwa. Na Hilo ni kosa kubwa la kukufuru.

7. Neema
Ukristo: Ukristo huu ndiyo msingi namba moja yaani huwezi tenganisha Ukristo na neema.
Kwamba mtu akifanya kosa basi anastahili kupewa nafasi ya pili, neema pasipo kuhukumiwa.
Wakati baba yake Uyahudi yeye kanuni yake ni haki. Kwamba mtu akikosea basi aadhibiwe, na mtu akipatia basi apewe zawadi yake (thawabu).

Uyahudi ulijikita kwenye mwili na roho. Wakati Ukristo unajikita katika roho pekee. Hii ni kumaanisha kinachopewa neema ni roho sio mwili. Yaani mtu akiomba neema ya msamaha, basi roho yake ndio ipewe second chance lakini mwili uadhibiwe.

Lakini wafuasi wa Ukristo wakalazimisha kuwa mwili na roho vyote vipewe neema😂😂. Huku wakishikilia kanuni isemayo usihukumu usije ukahukumiwa au samehe saba mara sabini. Wakisahau kuwa mwili ndio unafanya makosa wakati huo roho ndiyo hufanya dhambi😂😂. Mwili huadhibiwa na dunia kwa makosa yake wakati huohuo roho huadhibiwa na Mungu kwa dhambi zake.

Uislam: Mtoto huyo yeye kafuatisha kwa kiasi kikubwa kanuni na sheria na falsafa za baba yake. Mwenye makosa aadhibiwe kulingana na makosa yake na vile sheria zisemavyo.

Zingatia, binadamu hawezi kusamehe dhambi isipokuwa Mungu. Ila anasemehe makosa kwa sababu ya mwili ndiyo hufanya makosa na roho ndiyo itendayo dhambi. Kumaanisha, roho ndiyo inamuasi Mungu halafu mwili unamfanyia makosa binadamu mwenzako au kiumbe au mazingira yanayokuzunguka.

8. Hukumu
Ukristo: Mtoto huyu anajieleza kuwa atakayehukumu ulimwengu ni Kristo/Yesu.
Na Yesu ndiye atakuwa mtawala wa kila kitu. Hii ni tofauti na falsafa ya baba mtu Uyahudi. Yeye anajua Mungu ndiye mtawala na ndiye atakayehukumu viumbe vyake kwa haki. Zingatia neno viumbe inamaanisha vinavyoonekana na visivyoonekana. Hata Yesu pia ni kiumbe.

Uislam: Huyu mtoto anaungana na baba yake Uyahudi kwa kusema, hukumu atakayoitoa ni Mungu. Na kila kiumbe atahukumiwa kulingana na yale aliyoyafanya.

9. Urithi na mirathi
Ukristo: Umejikita zaidi katika mambo ya kiroho na kusahau mambo ya kimwili. Ukristo unajikita katika urithi wa Ufalme wa mbinguni pekee. Ilhali baba yake akijikita kwa yote mawili.
Uyahudi ilitoa utaratibu wa namna ya kurithisha mali kwa haki, na namna ya kutoa mirathi endapo mtu atakufa.

Ukristo jambo hilo limeachwa liamuliwe kidunia, hapohapo dunia kwa mujibu wa Ukristo inaongozwa na shetani😂😂. Unaona mambo hayo!

Uislam: Mtoto huyu kamuiga baba yake na kuongeza baadhi ya vitu. Kajikita kiroho na kimwili.
Urithi na mirathi kwa uislam imefafanuliwa namna itakavyogawiwa. Uislam haujaliacha jambo hilo liamuliwe na walimwengu kwani shetani ndiye mlimwengu mwenyewe.

Mpaka hapo sina la ziada, siyo kazi yangu kukuambia kipi chakuamini au kipi ni sahihi na kipi sio sahihi. Nilikuwa naeleza habari za watoto hao wawili wenye wafuasi wengi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Kwanza nikupe hongera kwa kuongea kile unachokijua.
You are what U learn.

Hata hivyo kumbuka ktk dunia tulionayo kuna vita kubwa sana inayoendelea.

Information warfare.

Ktk vita hii kuna misinformation na disinformation. Ktk makala yako pamoja na kusimama roho yako ikiwa huru hata hivyo umeathiriwa na vita kwa kiasi Fulani.

Nachotaka kusema ni kwamba dini zetu na imani zetu zimeshambuliwa kwa siasi kikubwa tokea iliposimama dola ya kale warumi.

Sasa kwa ufupi Uislam au kwa kiswahili unyenyekevu ni dini ya asili tokea kwa Adam. Ni kutokana na disinformation ndio watu wamekatirishwa kuwa uislam ulianzishwa na Muhammad.

Uislam unasema watu wote huzaliwa wakiwa waislam lkn wazazi wao huwabadili dini watoto (kuwabatiza) na kuwa waabudu masanamu au waabudu moto.

Ni warumi na wayahudi walioaso kama Paulo ndio waanzilishi wa ukristo wakosema "jamani kwa mambo aliyoyafanya huyu yesu.... Mmmm sio MTU huyu ni mungu. Na kuanza kuwauwa walioamini yesu ni mtume.

Kwa ufupi mavazi ya kale ya wayahudi na yesu wenyewe sawa na mama maria bint imran ni sawa na waislam wa sasa.

Kristo kwa mujibu wa wayahudi mpakwa mafuta.

Lkn professa Paulo akadisinform akasema INA maana ya mungu.

Hata hivyo shukran kwa madini yako. Uko ktk hatua chache kuuona ukweli kama utapata taarifa sahihi.
 
Je? Ibrahim alienda kaanani mwenyewe au aliitwa? Kama alienda mwenyewe kwa nini kizazi chake hakikumfuata huyo Mungu wa kusadikika wa kanani?

Kama aliitwa na akaambiwa atoke nchi yake ya Iraq aende caanani ni kwa nini afike caanani aache kumfuata Mungu aliemuita afuate kijimungu Cha kaanani??

Narudia kukuomba,,,nataka unionyeshe jina la Yehova,,Yahwe,,shadai,, Adonai katika miongoni mwa majina 99 ya Allah Subhana Wataalah.
Zamani watu walikua wakitanga tanga sana,, hasa hawa waliokua na mifugo,, story ya abraham siyo ya kuamini sana,, kipindi chake, timeline inakataa kwamba tayari ngamia alikua kishakua domesticated,,
Timeline ya abraham history inaangukiw kwenye Bronze age,,
Wakati moses timeline inaangukia kwenye iron age,,
Hivyo usiamini bila kufanya research,, in bronze age ina maana wanaadamu hawajagundua hata chuma ili wakitumie kuleta civilisation, na mifugo ilikua bado haijawa domesticated 😆😆
 
Je? Ibrahim alienda kaanani mwenyewe au aliitwa? Kama alienda mwenyewe kwa nini kizazi chake hakikumfuata huyo Mungu wa kusadikika wa kanani?

Kama aliitwa na akaambiwa atoke nchi yake ya Iraq aende caanani ni kwa nini afike caanani aache kumfuata Mungu aliemuita afuate kijimungu Cha kaanani??

Narudia kukuomba,,,nataka unionyeshe jina la Yehova,,Yahwe,,shadai,, Adonai katika miongoni mwa majina 99 ya Allah Subhana Wataalah.

Biblia ya Kiebrania haina neno “Yehova” ndani yake hata kidogo.

Neno linalotumika ni tetragramatoni kwa kutumia, 'Y' 'H' 'W' 'H'.

Mtu anawezaje kutamka YHWH kuwa Yehova? Hakuna njia inayowezekana. Kama vile Kiarabu, Kiebrania hakina vokali. Kuongeza vokali kunaweza kufanya neno kuwa "YEHOWA" lakini hiyo inamaanisha nini?

Neno hili si neno la Kiebrania, wala halina maana yoyote katika Kiarabu (lugha dada ya Kiebrania). Njia sahihi ya kulitamka ni "YAHUAH" ambalo pia lipo katika Kiarabu na kusomeka kama "YA HUWA" maana yake "O! HE" au "O! YEYE ni" na inaweza pia kuchukuliwa katika wakati ujao.

Catholic Encyclopedia inatoa maana ya Yahweh kama "Yeye Aliyeko" na pia inaendelea kutoa tafsiri yake isiyo sahihi kwamba ni jina la Mungu.

Huenda hoja hiyo ikasikika kuwa ya kudanganya lakini ikisomwa kulingana na muktadha na kutoka katika Biblia, inaonekana kuwa yenye mantiki na sahihi. Katika Biblia, wakati wowote maneno Ya Huwa yanapotumiwa, kuna neno la ufuatiliaji ambalo linamaanisha Mungu.

Kwa mfano:

JEHOVAH SHAMMAH

Ezekieli 48:35

YEHOVA RAFA

Kutoka 15

JEHOVAH-TSIDKENU

Yeremia 23:6

JEHOVAH-JIREH

Mwanzo 22:14

JEHOVAH-MELEK

Isaya 33:22

JEHOVAH-NISSI

Kutoka 17:8-16

JEHOVAH-SHALOM

Waamuzi 6:24

YEHOVA-SABATO

1 Samweli 1:3

YEHOVA-MEKADESHI

Mambo ya Walawi 21:8

Hizi ni sehemu chache tu ambazo majina haya yametajwa. Wametajwa mara nyingi.

Hata kama tunachukulia neno Yehova kuwa halimaanishi "O! Yeye yuko", bado haileti maana kile ambacho Biblia inasema.

Kwa njia hii, Yehova Elohim ingemaanisha “Mungu Mungu”.

Kwa hakika Yehova haimaanishi Mungu.

Biblia nyingi hutafsiri kama Bwana ambayo ina maana zaidi, "Bwana Mungu".

The dictionary defines Lord as:

1. a person who has authority, control, or power over others; a master, chief, or ruler.

2. a person who exercises authority from property rights; an owner of land, houses, etc.

3. a person who is a leader or has great influence in a chosen profession: the great lords of banking.

4. a feudal superior; the proprietor of a manor.

5. a titled nobleman or peer; a person whose ordinary appellation contains by courtesy the title Lord or some higher title.

6. Lords, the Lords Spiritual and Lords Temporal comprising the House of Lords.

7. (initial capital letter) (in Britain) a. the title of certain high officials (used with some other title, name, or the like): Lord Mayor of London.

b. the formally polite title of a bishop: Lord Bishop of Durham.

c. the title informally substituted for marquis, earl, viscount, etc., as in the use of Lord Kitchener for Earl Kitchener.

8. (initial capital letter) the Supreme Being; God; Jehovah.

9. (initial capital letter) the Savior, Jesus Christ.

10. Astrology. a planet having dominating influence.

Lord does not mean God.

Kwa Kiarabu ,YaHuwa ,maana yake ni "O! YEYE ni" na kwa Kiebrania ina maana "Aliyeko".

Maana hizi mbili zinafanana sana. Limetumika kimakosa kama jina la Mungu.

, katika Kiebrania ,Ya Huwa (Yehova/Yahweh) si jina la Mungu bali larejezewa kuwa hilo kwa sababu ya heshima.
 
Soma kisa cha Abraham wanapokutana na mtawala wa wafilist na mkuu wa mji wa jerusalem,, Melkizedeki,,
Melkizedeki ndio aliemu introduce Abraham kwa mungu mkuu wa Canaan El,,
Ndio maana hata mtoto wake wa kwanza akamwita Ishmael, ambalo lina maana moja na ismail.. 🤷🏼‍♂️,
Anyway ntakutafutia andiko la mkutano wa abraham na melkizedeki,

Soma pamoja nami.
hapo Mungu gani anatajwa?
Ibrahimu hajawahi kuabudu miungu bali Mungu muumba mbingu na nchi...Mungu mwenyezi.

Mimi ni msomi mzuri wa biblia na vitabu wa thilojia huwezi kuniletea blaablaa kamwa.

Nimesoma pia dini za ulimwengu na Uislam wako naujua vilivyo...nimecheza misikirini udogoni so unapoleta hoja jizatiti
Screenshot_20230225-192412_Biblia Takatifu.jpg
 
Soma pamoja nami.
hapo Mungu gani anatajwa?
Ibrahimu hajawahi kuabudu miungu bali Mungu muumba mbingu na nchi...Mungu mwenyezi.

Mimi ni msomi mzuri wa biblia na vitabu wa thilojia huwezi kuniletea blaablaa kamwa.

Nimesoma pia dini za ulimwengu na Uislam wako naujua vilivyo...nimecheza misikirini udogoni so unapoleta hoja jizatiti
View attachment 2529818
Inabidi uwe unafanya research,, mungu the most high,, yaani alie juu wa eneo hilo aliitwa El,,
Alie juu wao walikua wanatafsiri , juu kwa maana mkubwa kuliko wote na anaepatikana juu,
Ndio maana hata moses alipotaka kuongea na huyo mungu alipanda mlimani,, hata yesu pia alikua akipanda mlimani,,
Ilikua ni marufuku kujenga majengo marefu, kwani ilitafsiriwa kwamba ni kutaka kujiweka juu kama huyo mungu,
Ndio maana kuna story ya watu eti walitaka kujenga wamfikie mungu,, mungu akawachanganya(story ya BabEl),
Melkizedeki sio jina la mtu, ni cheo.
Melk=malki=mmiliki=KING.
Zedeki=Mtukufu,
Melkizedeki=MFALME MTUKUFU,
so melkizedeki alikua mfalme wa citystate called, Saleam,
Alikua king na pia kiongozi wa kiroho kama alivyo Ayotollah tu ,, 😄🤷🏽‍♂️,
Mungu aliekuwa akimuabudu ni caananite deity, called El,,
Ambae ukitaja mungu mkuu yaani The most high,, unasema El Elyon,
So melkizedeki alikua king na pia kuhani mkuu wa El Elyon yaani God the most high,
Abraham alitoa fungu la kumi, according to tradition kwa Melkizedeki,,
Sasa jiulize, kwanini jina halisi la melkizedeki limefichwa, kwanini story inataja title ya huyo, Mfalme mtukufu na siyo jina halisi?
 
Kwanza nikupe hongera kwa kuongea kile unachokijua.
You are what U learn.

Hata hivyo kumbuka ktk dunia tulionayo kuna vita kubwa sana inayoendelea.

Information warfare.

Ktk vita hii kuna misinformation na disinformation. Ktk makala yako pamoja na kusimama roho yako ikiwa huru hata hivyo umeathiriwa na vita kwa kiasi Fulani.

Nachotaka kusema ni kwamba dini zetu na imani zetu zimeshambuliwa kwa siasi kikubwa tokea iliposimama dola ya kale warumi.

Sasa kwa ufupi Uislam au kwa kiswahili unyenyekevu ni dini ya asili tokea kwa Adam. Ni kutokana na disinformation ndio watu wamekatirishwa kuwa uislam ulianzishwa na Muhammad.

Uislam unasema watu wote huzaliwa wakiwa waislam lkn wazazi wao huwabadili dini watoto (kuwabatiza) na kuwa waabudu masanamu au waabudu moto.

Ni warumi na wayahudi walioaso kama Paulo ndio waanzilishi wa ukristo wakosema "jamani kwa mambo aliyoyafanya huyu yesu.... Mmmm sio MTU huyu ni mungu. Na kuanza kuwauwa walioamini yesu ni mtume.

Kwa ufupi mavazi ya kale ya wayahudi na yesu wenyewe sawa na mama maria bint imran ni sawa na waislam wa sasa.

Kristo kwa mujibu wa wayahudi mpakwa mafuta.

Lkn professa Paulo akadisinform akasema INA maana ya mungu.

Hata hivyo shukran kwa madini yako. Uko ktk hatua chache kuuona ukweli kama utapata taarifa sahihi.
Kama ndio hivyo basi quraan ni kitabu cha uongo. Quraan yenyewe inasema muhamad ndio muislam wa kwanza alafu hapa unakuja na Adam.
 
Inabidi uwe unafanya research,, mungu the most high,, yaani alie juu wa eneo hilo aliitwa El,,
Alie juu wao walikua wanatafsiri , juu kwa maana mkubwa kuliko wote na anaepatikana juu,
Ndio maana hata moses alipotaka kuongea na huyo mungu alipanda mlimani,, hata yesu pia alikua akipanda mlimani,,
Ilikua ni marufuku kujenga majengo marefu, kwani ilitafsiriwa kwamba ni kutaka kujiweka juu kama huyo mungu,
Ndio maana kuna story ya watu eti walitaka kujenga wamfikie mungu,, mungu akawachanganya(story ya BabEl),
Melkizedeki sio jina la mtu, ni cheo.
Melk=malki=mmiliki=KING.
Zedeki=Mtukufu,
Melkizedeki=MFALME MTUKUFU,
so melkizedeki alikua mfalme wa citystate called, Saleam,
Alikua king na pia kiongozi wa kiroho kama alivyo Ayotollah tu ,, 😄🤷🏽‍♂️,
Mungu aliekuwa akimuabudu ni caananite deity, called El,,
Ambae ukitaja mungu mkuu yaani The most high,, unasema El Elyon,
So melkizedeki alikua king na pia kuhani mkuu wa El Elyon yaani God the most high,
Abraham alitoa fungu la kumi, according to tradition kwa Melkizedeki,,
Sasa jiulize, kwanini jina halisi la melkizedeki limefichwa, kwanini story inataja title ya huyo, Mfalme mtukufu na siyo jina halisi?
Hii ni tafsi yako binafsi ndio maana unaandika mungu na sio Mungu
 
Umeshindwa kuthibitisha kimaandiko huyo mungu El wa Kanaan.
 
Hii ni tafsi yako binafsi ndio maana unaandika mungu na sio Mungu
Mie najadili hii mada with open mind,, wewe uko kimahubiri zaidi,, 😆,huwezi ukanielewa,, wewe uko brainwashed, huwezi kumwelewa mtu ana discuss with open mind,,
Ndo maana unaona hata kuandika mungu kwa herufi ndogo eti ni dhambi😂,
Uko so deep brainwashed na dini za kigeni, wazungu wenyewe waliozileta wanajadili hizi ishu with open mind,,
Leo sasa ngozi nyeusi ndo utashangaa, 🤷🏾‍♂️
Jews claim themselves to be a race – but are they?
The earliest reference yet found to this singular people is on a statue from the Syrian city of Alalakh, dated to about 1550 BC. The inscription refers to hapiru warriors in the land of Kin’anu – a presence confirmed by clay tablets from Akhenaten’s capital of Amarna, referring to marauders in the hill country of Palestine. The famous stele of Pharaoh Merneptah dated to 1207 BC records 'Israel is laid waste, his seed is not’. 'Israel' here is a reference to a people, not a territory.

The weight of evidence suggests these original ‘Hebrews’ coalesced during the bronze age from successive migrations, some from the periphery of the Nile delta (in Egyptian, ‘Peru or apiru meant a labourer) but most from across the Jordan and Euphrates rivers. In their own semitic tongue, habiru meant ‘beyond’, suggesting an origin elsewhere. In Babylonian script khabiru referred to a class of slaves. As a people, therefore, the Hebrews combined Mesopotamian and Egyptian stock, almost certainly drawn from the lowest social order, conceivably including runaway slaves. One migration, at least, brought with it a mountain/sky god – Yahweh – destined for higher things.

Settlement in Canaan

As barbarous newcomers to what was the land of Canaan, these semites (speakers of a tongue common to Syrians, Arabs and Mesopotamians) took up migratory occupation of the less fertile hill-country of the interior. Neither their limited sub-culture – an illiterate donkey nomadism; nor their social organisation – patriarchal and authoritarian – distinguished them from other tent-dwelling pastoralists. These early, polytheistic, Hebrews scratched an existence in an unpromising land on the fringes of the major civilisations, occasionally moving with their animals into the Nile delta in times of draught.

It seems as if they were joined, over time,by outcasts or refugees from the more sophisticated Canaanite (Phoenician) coastal cities. ‘Israel emerged peacefully and gradually from within Canaanite society ‘ concluded Karen Armstrong, the noted religious scholar. (A History of Jerusalem, p23]

Ethnic cleansing – by God's order
"And the Lord said to Moses in the plains of Moab by the Jordan at Jericho,
"Say to the people of Israel, When you pass over the Jordan into the land of Canaan, then you shall drive out all the inhabitants of the land from before you, and destroy all their figured stones, and destroy all their molten images, and demolish all their high places; and you shall take possession of the land and settle in it, for I have given the land to you to possess it ...
But if you do not drive out the inhabitants of the land from before you, then those of them whom you let remain shall be as pricks in your eyes and thorns in your sides, and they shall trouble you in the land where you dwell.
And I will do to you as I thought to do to them
."
Numbers 33.50-56
The Canaanite migrants brought with them cultic practices and images of their traditional gods. A major Canaanite god was El, and the phrase ‘El has conquered’ gives us the word Isra’el. The Canaanite god El had a ghostly presence in a host of Jewish heroes: Dan-i-El; Ezek-i-El; Sam-u-El, Ish-ma-El, El-i-jah, El-o-him, etc.

God-inspired names were common throughout the west-Semitic language region. Other Canaanite gods included Baal (a storm god) – also honoured in a host of Hebrew names, Asherah (a fertility goddess, consort of El), Shalem (a Syrian sun god – later to be honoured in the name Jeru’salem ), Milcom, Chemosh, etc. Ru’shalimum is mentioned in records of the Pharaoh Sesostris III (1872 - 1847 BC) – the settlement actually pre-existent long before the tribe of Hebrews made it their own. The site then appears to have been unoccupied for three hundred years until the Jebusites (otherwise known as Kereti or Peleti – Cretans or Philistines) arrived.
 
Mimi nilitaka tujadili neno nabii na mtume.
Wengi hawajui maana yake ndio maana wanapinga unabii na utume wa Yesu

Sasa nimekuelewa , nitakuja tena baadaye nikijaaliwa
 
Back
Top Bottom