Uchambuzi wa Kiufundi naunga mkono nchi yetu kununua umeme kutoka inje nchi kuliko kusafilisha hadi kaskazini

Uchambuzi wa Kiufundi naunga mkono nchi yetu kununua umeme kutoka inje nchi kuliko kusafilisha hadi kaskazini

Sasa kama tulikuwa na hiyo access toka Mwanzo, hayo matrilioni tuliyoenda kuchoma hapo Rufiji ni ya kazi gani...

Kagera, Geita, Mwanza-Uganda
Mbeya, Ruvuma, Katavi-Zambia
Mara-Kenya
Kili, Arusha, Manyara-Ethiopia.

Mtwara, Lindi- Mozambique

Tayari nusu ya nchi ina access ya Umeme nje ya nchi, zile MG kwamba tuzalishe ili tujitegemee zilikuwa za nini?

CBA haikufanyika?

Au National sovereignty came into play?

Au kuna Miscalculation kubwa ambayo pengine hatuji au hatuambiwi.
Me nilisema watakuja na utetezi wa ujinga lengo la kujenga bwana kubwa ni sisi tu run solo kama ishue ilikuwa hivyo kwanini tusinge kujua tu tungesave hela mingi
 
Hoja za mleta mada hazina mashiko hata kidogo.

Kulikuwa na haja gani kujenga HPP kubwa kama uwezo na gharama za kusambaza hatuziwezi?

Kama Station kubwa ipo Chalinze, kuna umbali gani kutoka hapo hadi Tanga, Same nk hadi tuone its cheaper kununua huko Ethiopia/Kenya kuliko kuweka lines zetu na kutumia umeme wetu?

Kwanini Pangani na Nyumba ya Mungu yaliyopo kaskazini yasiboreshwe ili kuleta stability ya umeme ukanda huo?

What was the point kujenga HPP kubwa kama mikoa yote ya mipakani wanategemea kununua umeme nje ya nchi? Hii surplus iliyopo itamnufaisha nani?

Nini maana ya kusema TUTAUZA UMEME KWA MAJIRANI wakati hata capacity ya kujenga transmission lines hatuna?

Bado hoja hazina mashiko, upigaji tu wa ccm na watu wake.
 
Nitakujibu hapa hapa.

1. Unazungumzia Kaskazini yenye mabwawa ya umeme ya Nyumba ya Mungu, Hale na Pangani yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha mikoa ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga. Kwanini uende nje ya nchi kununua umeme?

2. Umeme unaosema kunakwenda kuuchukua Kenya ni umeme unaozalishwa kwenye mabwawa kule Ethiopia na kusafirishwa kupitia Kenya na baadaye ndio uingie Tanzania. Kama unasema Rufiji ni mbali basi tuambie ni vipi Ethiopia patakuwa karibu. Hupaswi kuupima umbali kutoka hapo Kenya umeme unapopitishwa bali kule kule unapozalishwa yaani Ethiopia.

3. Katika mazingira ambayo tunazalisha umeme mwingi kupitiliza, na tunaupata bure kutoka Rufiji, ni vipi unataka tuumie huo upotevu unapotokea wakati tukiusafirisha kuuleta mikoa ya kaskazini kiasi tuamue tutoe pesa zetu kwenda kuununua umeme kutoka nje ya nchi?
Hale 21MW, Nyumba ya Mungu 8MW hio ndio capacity ya hayo mabwawa. Nchi nzima tunazalisha umeme kama 3600MW hivi, so huo ni kama asilimia 1 ya umeme wote nchi hii, je asilimia 1 ya umeme unatosha kuhudumia Kaskazini nzima?

Mleta mada kakuambia miundombinu ipo Kenya, tayari ipo it's not like serikali ya Tanzania inanunua nguzo na kuzisambaza hadi Ethiopia.

Na uwezekano upo wa kutoa umeme Rufiji hadi Same ila haimaanishi tayari miundombinu 100% ipo, je upo tayari wenzako wakae bila umeme wa uhakika ama uchukue shortcut

Kama Hufahamu Tanzania inauza pia umeme kwa Nchi jirani, Around Bilioni 30 zinapatikana kwa kuuza umeme nje, haimaanishi hizo nchi tunazoziuzia hazina umeme la hasha, bali na wao wana strategic area ambazo kwao ni rahisi kununua kwetu kuliko kusambaza wenyewe.
 
Serikali haifanyi biashara bali inatoa huduma kwa wananchi wake....hata ikisafirisha kilomita afutatu ni sawa kulikuwa kununua nje ,je ikitokea migogoro ya kidiplomasia si tutalala giz huku kaskazini?
Halafu nyie nyie munakuja kulalamika kampuni za Serikali zikifanya vibaya.
 
1741562191671.png

kwenye umeme, ukichanganya tu kati ya KVAR na KVA, inatosha kuvuruga kila kitu.......
 
Kwahiyo uzalishaji wa umeme umefikia lengo?kwanza tuanzie hapo
Lengo limefikiwa, wali-target about 3.4GW kufikia 2025, na 5GW kufikia 2044.

Grid ipo mpaka Nyqmongo, Mara, upande ule kutokea Chalinze mpaka Same, Moshi...Tanga ndani!

Magharibi mwa nchi ndo hawana grid, sasa hiyo kaskazini ni ipi isiyo na umeme kwasababu ya transmission line?

Ukumbuke, huo wa kuchukulia Kenya, tutaunga kwenye 33kV sawa na unaotoka kwenye substation kama za Kipawa na the like.

Wakati Kilwa Energy ina harakati za kuanza, plan si ilikuwa kuuza Kenya? Transmission line gani ingetumika?

Mtoa mada ni chawa na si vinginevyo!
 
Hale 21MW, Nyumba ya Mungu 8MW hio ndio capacity ya hayo mabwawa. Nchi nzima tunazalisha umeme kama 3600MW hivi, so huo ni kama asilimia 1 ya umeme wote nchi hii, je asilimia 1 ya umeme unatosha kuhudumia Kaskazini nzima?

Mleta mada kakuambia miundombinu ipo Kenya, tayari ipo it's not like serikali ya Tanzania inanunua nguzo na kuzisambaza hadi Ethiopia.

Na uwezekano upo wa kutoa umeme Rufiji hadi Same ila haimaanishi tayari miundombinu 100% ipo, je upo tayari wenzako wakae bila umeme wa uhakika ama uchukue shortcut

Kama Hufahamu Tanzania inauza pia umeme kwa Nchi jirani, Around Bilioni 30 zinapatikana kwa kuuza umeme nje, haimaanishi hizo nchi tunazoziuzia hazina umeme la hasha, bali na wao wana strategic area ambazo kwao ni rahisi kununua kwetu kuliko kusambaza wenyewe.
Hale 21MW. Nyumba ya Mungu 8MW, Pangani Falls 68MW.
 
Kuna ufisadi utafanyika hapo. Hela za kununulia umeme zitatiwa mfukoni na Kaskazini watapata umeme wa humu humu ndani.
 
Kuna wakati Makamba Jr alisema serikali inanunua software itakayotumiwa na Tanesco kwa around 60B(?).

Huu ni mwendelezo wa ufisadi ndani ya nchi, hakuna sehemu nzuri kupiga pesa kama kwenye construction na tender kubwa kama hizi. Utayafahamu yote in the next 10yrs, not now!
 
Kama miaka yote hatuna umeme huko kaskazini, hiyo haraka ya kununua umeme kutoka nje ya nini au kuna nini hasa mpaka muone leo kuna haja ya kununua umeme kutoka nje ya nchi?

Kama kujenga miundo mbinu kuusambaza umeme itachukua miaka 5 hadi 10, kwanini tusifanye hivyo kwa kutumia hizo pesa za kutaka kuagiza umeme kutoka nje?

Sisi wadanganyika hatuna haraka, tumeishi maisha haya ya bila umeme na maji miaka yote na tupo, kwanini leo nyie watu wachache mjifungie huko mtoke na majibu rahisi kama haya, kwamba tununue umeme kutoka nje kwa sababu gharama za kusambaza umeme wetu ni ghali sana.

Kwani gharama za kujenga hilo bwawa Rufiji ni ndogo?

Mbona tuliamua kulijenga?

Malengo ilikuwa ni tujitosheleze sisi kwanza, kwa nishati humu ndani, kisha ziada ndio tuuze nje.

Mimi sijali wewe ni Engineer au Fundi mchundo, mimi sioni kama hiki unachokisema kiko sawa.

Hakuna mradi rahisi, hata SGR siyo rahisi lakini tulijenga na tunaendelea kujenga, kuna mradi wa UDART sio rahisi lakini bado tunaujenga.

Aliyekwambia sisi hatujui kujenga miundombinu kuusambaza huo umeme ni ghali ni nani?

Kama umeme umeshazalishwa wa kutosha na hauna pa kwenda, tusifunge mashine zote au tusimamishe uzalishaji tuanze kutengeneza miundo mbinu ya kuusambaza humu nchini kwanza.

Sidhani kama Magufuli alitaka kujenga bwawa lile ili tufanye biashara, alichoka na vilio vya shirika letu la umeme Tanesco, kusema umeme hautoshi, mara bwawa la Mtera limekauka, mara IPTL mafuta, na upuuzi kama huo, na ndio maana walikuwa wanatupa nishati hiyo kwa mgao.

Kwanini leo muanze kutupanga na kutufundisha biashara badala ya kutafuta njia za kutusambazia umeme?

Kule Kagera, kuna kampuni ya ABB walijenga zile nguzo kutoka uganda sidhani hata kama miaka sita ilifika. Tuwaite hawa watujengee miundombinu ya kuusambaza.

Miaka ile IPTL inaanzishwa tuliambiwa hadith kama hizi, kwamba IPTL itazalisha umeme wa kutosha na utakuwa ni muarobaini kwa tatizo letu la umeme nchini, kumbe ilikuwa miradi ya wezi wachache. Kila siku hesabu zinabadirika.

Wakaja wajanja wengine Richmond, SONGAS yale yale.

Kuna Mbunge mmoja anajiita Dr. Kasheku Musukuma, anasema kuna wapigaji nchi hii, wakitaka kupiga wanakunja na gia za usomi. Wana kuja na maelezo meeengi, kutafuta namna ya kujustfy upigaji wao, kisha wanatokomea gizani.

Kuhitimisha hoja yangu, Sisi hatuna haraka, kama kujenga miundo mbinu ni miaka 5 au 10, jengeni tutasubiri umeme wetu wenyewe.

Huo mnaotaka kuuleta wenyewe auhitaji miundo mbinu ya kuuingiza nchini?

Ikiwa huo nao utahitaji miundombinu, basi nashauri tujenge miundombinu yetu, iwe ya juu au aridhini lakini tuwe na mfumo wetu, tutumie umeme wetu, hatuna haraka.
Bila shaka Pana upigaji umeandaliwa hapo ! Wajanja macho kumchuziii !
 
Unataka kuniambia wewe unaakili kuliko wizara waliotathimini wakaona wakachukulie kenya!
Wakati mwingine Vijana tunahoji vitu vingine havina hata msingi!

Nimekutolea mfano ungekuwa wewe ungesafilisha maji kutoka Dar upeleke dodoma wakati Dom kuna mtu anatafta wateja kwa gharama nafuu?
Safirisha...
 
Nayazungumza haya nikiwa kama fundi mzoefu katika sekita ya umeme!

Nimeona mijadala watu wakilalamika kwanini nchi inataka kununua umeme kutoka inje kwa mikoa ya kaskazini wakati ina umeme wa kutosha?

Ni kweli nchi ina umeme wa kutosha lakini haina maana kwasababu umeme upo wa kutosha basi unaweza kuupeleka popote pasipo kufanya tathmini!

Iko hivi umeme kutoka vyanzo vikuu vya umeme wa uhakika Rufiji na mikoa mingine ukitaka kuusafirisha kwenda mikoa ya kaskazini unakuwa unazungumzia mradi wa wastani wa 800km ~900Km

Gharama za kusafirisha umeme kwa umbali huo ni kubwa mno ukilinganisha na kuuchukulia hapo kenya .
Wanaposema umeme wa Ethiopia haina maana uko huko Ethiopia! Ni uko hapo jilani kenya wastani wa km 250km~300km tu

Hivyo ukichukulia gharama za kuusafirisha umeme kwa wastani 50mil kwa kila span moja ( nguzo moja hadi nyingine) hapa tutazungumzia wastani wa span elf 8000 hadi 9000 endapo utaamua kuutoa Rufiji

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Mbali na gharama hizo mradi mkubwa kama huo unahitaji kulipa watu fidia na kuchepusha miundombinu itayoingiliana hapo katikati ya mradi!

Miradi ya mabomba ya mafuta yaliyopita ardhini yatalazimisha kubadilisha span badala ya kupitisha umeme juu ya bomba ushushwe chini (underground) ili kuepusha muingiliano wa frequency za umeme na zile za bomba la mafuta! Yote hayo yanapaisha gharama za mradi!

Muda wa kuujenga mradi mkubwa kama huo unaweza kuchukua miaka siyo chini ya mitano!

Upotevu wa umeme hapo katikati (power losses) kwa umbali huo ni Mkubwa ukilinganisha na faida utayovuna ukiuufikisha mikoa husika ya kaskazini!

Yote tisa hata kama umeme upo lakini kama jilani ana bei rahisi kuliko za nchi yetu kwanini kujichosha ilihali kwa jilani anao umeme karibu na ni bei nafuu zaidi?

Ambao hawajaelewa naomba kutoa mfano huu!

Mfano una nyumba yako dar salaam na umechimba kisima na unayo maji ya kutosha hata kusamabaza! Ukajenga nyumba nyingine Dodoma ambako huko kuna mtu ana kisima cha maji ya bei rahisi zaidi kuliko hata wewe unavyowauzia maji dar!

Je utalaza mabomba ya maji uunganishe maji yako kutoka Dar upeleke hadi Dodoma kisa una maji ya kutosha hapo DAR?

Kama mtu hajaelewa na anaswali kwanini serikali inampango wa kununua umeme kutoka jilani niko tayali kumwelewesha zaidi kiufundi ;
mimi naitwa fundi samico, napatikana kwa namba 0711756341 na huko Instagram Samico Tanzania
Nimeishia pale nilipoona unasema wewe fundi mzoefu kwenye SEKITA ya umeme. Mimi sijui mambo yanayohusu SEKITA ya umeme.
 
Back
Top Bottom