Uchambuzi wangu kuhusu hoja za Tundu Antipass Lissu kwenye suala la Bandari

Natamani angetoka mwanasheria mkuu wa serekali akaeleza mbivu na mbichi za mkataba huu
Mkuu unategemea mwanasheria mkuu wa serikali atatoa kilicho nje ya matakwa ya serikali?
 
Natamani angetoka mwanasheria mkuu wa serekali akaeleza mbivu na mbichi za mkataba huu
Sidhani kama kuna haja hiyo? Kinachofanyika ni utoto na siasa za upotoshaji sasa atajibu mangapi? atawajibu wangapi? Si kila siku atakuwa anaitisha press conference!!
 
Sehemu pekee unayoweza mjibu Lissu Kwa utulivu ni nyuma ya keyboard tu.

Zaidi ya hapo, Lumumba hawana mtu wa kumjibu Lissu.
Lissu nimemjibu mara nyingi sana alivyoenda ndivyo sivyo na nimewahi muunga mkono sehemu nyingi sana alizoenda sahihi.

Humu Jf nimeshawahi itwa mke wa Tundu Lissu, wengine wamewahi niita Tundu Lissu kipindi nilivyosimama na Lissu mwaka 2017- 2020 sasa sijui kama una lingine?
 
Watanganyika tuhamuke, kyaro chaghenda
 
Nadhani umeanza kunifahamu juzi wewe!! Mimi niwe na njaa leo?? Wakati nipo upande wa Lissu namtetea humu 2017- 2020 nilikuwa nimeshiba sio? Nilikuwa nahongwa na Lissu sio?
 
Wewe ndio hujaelewa au unapotosha! Huu mkataba uliopitishwa bungeni ndio mkataba mama na kupitishwa kwake bungeni unaenda kuwa juu ya katiba kama alivyosema Lissu.

Hizo HGA msingi wake ni huo mkataba na lazima isipingane. Kama mkataba mkuu hauna ukomo kwanini tuamini HGA zitakuwa na ukomo? Tunawajua CCM, mnaweza kuja kutuingiza matatizoni zaidi.

Kuhusu kodi pia huku muelewa Lissu, mkataba mkuu umeshasema maswala ya kodi kwenye uwekezaji sheria ipi ifuatwe! Hiyo sheria imejaa exemptions kibao na pia imeelekeza watalipa kodi kwenye faida. Mkataba wenyewe hauelezi uwekezaji ni kiasi gani, mgawanyo wa faida utakuwaje! Hizo HGA zitafanya nini hapo?

Mkataba umetoa hadi maeneo mengine ya kiuchumi kwa huyo huyo mwekezaji kwa masharti hayo hayo. Ni hatari.
 
Sawa huu ndo mkataba mama! Niambie basi kwa mujibu wa huu Mkataba Mama DP World kapewa bandari zipi?
 
Kumbuka kuwa hata mahakama hupishana kwenye hukumu ya kosa moja, huo si upotoshaji kwenye kesi hisika, maamuzi ya jaji mkuu yanaweza kupingwa na jaji wa chini yake, huo si ushujaa, unaweza kuwa sahihi lakini lugha uliyoitumia haitufanyi watu wote tuamini wewe pekee uko sahihi.
 
Ni sawa ila nimeeleza kihoja kwa nini anapotosha
 
Wewe pandikizi la mabeberu! Sisi tumemwelewa vizuri Tundu lisu
 
Lord denning nisaidie kitu kimoja tu, yaan huu mkataba unachukua mda gani labda miaka 20, 45 au ngp🤔
Masuala ya muda yatawekwa kwenye Host Government Agreements au other agreements ambazo kwa mujibu wa Article 1 (2) ndo zitaingiwa kuhusu uwekezaji kwenye maeneo husika na kutoa wajibu pamoj na kuweka masharti kwa pande husika
 
Popote utakapomuona GUSSIE na Lord denning ujue Kuna umatemate

Huwezi wakosa hao mapacha kwenye dili zenye na mpunga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…