Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli 🙏Upuuzi mtupu. Hakuna uchunguzi wowote wala kitu cha maana, ni siasa tu za umiliki wa mali za kanisa kati ya Mke wa TB Joshua na Baraza la Wazamini wa Kanisa kwani mama aliwashinda waliokuwa wanategemea kujichotea manoti ya kanisa baada ya jamaa kufa. Sasa wanapambana kuona namna gani wataliyumbisha kanisa mbele ya jamii.
Hapa hakuna uchunguzi wa maana na huo uchunguzi ni aibu kwa BBC. Uchunguzi ungetakiwa usiwe wa maneno tu bali uwe na ushahidi tosha kama:
1. Taarifa za kidaktati zinazoonesha namna hao waathirika waliathiriwa na Nabii.
2. Case zilizofunguliwa Mahakamani na mashtaka yaliyopelekwa polisi.
3. Namna Balozi za UK,NAMIBIA na nchi nyingine zilipokea malalamiko na kurespond kuhusu malalamiko ya waathiriwa.
4. Picha na vielelezo toka kwa waathirika.
Simtetei TB Joshua kwani naye ni Bunadamu na alikuwa na mapungufu ila hiki walicholeta BBC ni blah blah na hadithi tu, kwanini wasingechunguza na kuja na hizo blah blah muhusika akiwa hai?
Blah blah hizi zinahusu mtu aliyekufa direct asiyejitetea na hazihusu taasisi. Wajunga wasiojitambua wala wenye uwezo wa kufikiria kizazi cha 1990's to 2000's ndio mtashadadia ila kwa mtu mwenye utulivu wa kiakili, hakuna kitu cha maana hapa.
Watajitokeza wengi, wa Tanzania bado wapo kimya sijui wanaona aibu?
Kanisa litawalipa fidia.
Ukute na huku kwetu yapo hivyo hivyo ila watu wanajikaza tu.
Nini huwa kinawasukuma BBC kutayarisha documentaries nyingine mbalimbali?Nini kiliwasukuma BBC kutayarisha documentary hiyo?
KwambaWatu sijui wanaangalia vipi mambo, vile ambavyo hawaamini kwamba aliyejiita nabii Joshua anaweza kubaka au kufanya mambo machafu hayo ndivyo pia waliobakwa walikuwa wanaogopa kutoka hadharani na kusema wakihofia kutoaminika na kutukanwa na waaminifu wake Joshua.
Hawa watu wakubwa wanaoaminika kwenye jamii wana matendo ya kishenzi ukiambia huwezi kuamini!
Mtu ana bakwa hadi ana abort mimba 5 mwingine 3 ?? Ume waona hao wana wake BBC lakini ? as a man sijaona cha kuni shawishi kubebeahq mimba mala 5 ata mmoja paleeWatu walibakwa seminary
wamekuja kusema uzeeni.....
We vipi mkuu. Mambo hayo yamechanganyika na woga wa kiimani.
Hata kuandika hujui [emoji23][emoji23]Baki njia kuu CATHOLIC CHARCH FINISHED
Achana na imani...KwambaMtu ana bakwa hadi ana abort mimba 5 mwingine 3 ?? Ume waona hao wana wake BBC lakini ? as a man sijaona cha kuni shawishi kubebeahq mimba mala 5 ata mmoja palee
Tunacho sema sisi ni hii trend ya wanawake wa ulaya kufungua case za claim za miaka ilio pita kuchafua watu
Huu sio uchunguzi. Huu ni sawa na ubuyu wa Nifah tu. Wangemuomba hata cocastic Awafanyie uchunguzi kuliko huu ujinga waliouleta mbele za watu.KwambaMtu ana bakwa hadi ana abort mimba 5 mwingine 3 ?? Ume waona hao wana wake BBC lakini ? as a man sijaona cha kuni shawishi kubebeahq mimba mala 5 ata mmoja palee
Tunacho sema sisi ni hii trend ya wanawake wa ulaya kufungua case za claim za miaka ilio pita kuchafua watu
Umenishawiahi kuanza kuamini kuwa kuna kitu cha kutazama behind the altar1. Wanaoshuhudia madhila na utapeli ni walioukuwa watumishi na wanafunzi wa TB Joshua mwenyewe na kanisa lake, sio watu baki. Mmojwapo ni watu waliokuwa karibu kabisa naye kama mtu namba mbili baada ya TB Joshua.
2. Kwenye baadhi ya sehemu za clips zilizorekodiwa na kanisa hilo na ambazo ni public zilizotumiwa na BBC TB Joshua anaonyeshwa akifanya mambo ya ajabu mbele ya hadhara kama kupiga watu makofi kama sehemu ya huduma!
3. TB Joshua alikuwa akiishi kwenye jumba mfano wa gereza na kundi kubwa la wanaoitwa "disciples" wanafunzi wake, wengi wakiwa wanawake vijana na vigori, walivyokuwa wanapatikana anajua yeye mwenyewe ila mmoja wa wahojiwa anasema alipewa na kazi na TB Joshua ya kuleta wanafunzi wa kike mabikira. Watu kuzuiliwa kama wako kifungoni na viongozi wa cults sio jambo jipya, mifano ni mingi sana kuanzia kwa jirani zetu hapa Kenya katika kisa cha Shakahola, huko kwingine duniani wamewahi kuwepo kina Jim Jones wa people's temple, David Koresh wa Waco n.k
4. Hakuna mgogoro wowote ndani ya kanisa la SCOAN unaohusishwa na waathirika hawa walioamua kusema yaliyokiwa yanatendeka nyuma ya pazia, hivyo huwezi kusema hata ni watu wenye nia ovu ya kulimega hilo kanisa na kuanzisha lao.
5. BBC wanasema waandishi wao walirushiwa risasi na walinzi wa kanisa hilo walipokuwa wanachukua video. Kanisa lolote linaloweza kufikia kiwango hichi cha kujificha kutoka waandishi wa habari ni taa nyekundu.
6.Ni kweli jengo la kanisa la TB Joshua liliwahi kuanguka na kuua mamia ya watu kwa sababu ya kutofuata taratibu sahihi za ujenzi na TB Joshua akasema kulikuwa na ndege ndogo iliyokuwa ikizunguka katika jengo hilo iliyopelekea kuporomoka na kwamba pia lilikuwa na jaribio la mauaji dhidi yake. Hata hivyo Ushahidi wa wazi ni kwamba taratibu nyingi za ujenzi wa jengo hilo zilikiukwa lakini kwa sababu matapeli wa kidini kama yeye wamekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana katika serikali za Africa hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa.
7. BBC wamefanya uandishi wa kiuchunguzi "investigative journalism" sio utafiti "research" au forensic investigation ambayo sasa inapaswa kufanywa na polisi kuthibitisha zaidi yaliyoletewa hadharani na BBC. Yani kazi kubwa iliyofanywa na BBC ni kuwasikiliza waathirika takribani 30 kutoka sehemu mbalimbali, kuhakikisha hawajapanga "conspire" kusema walichosema, kuoanisha wanachosema"corroboration" na kisha kuwapa fursa kanisa la SCOAN la TB Joshua kuzungumzia tuhuma hizo ambapo walikataa kuwapa ushirikiano wowote.
Kazi ya ushahidi mwingine unaodaiwa na baadhi ya member hapa jukwaani kama ushahidi wa video wa watu wakibakwa ni suala la forensic investigation na mahakamani kama polisi wa Nigeria wataamua kufuatilia kesi hiyo. BBC wamefanya kazi yao uandishi wa kiuchunguzi kwa weledi mkubwa na wamemaliza.
Kwetu si ndio kina Mwamposa hao na wenginewanaojinadi kufufua watu.Watajitokeza wengi, wa Tanzania bado wapo kimya sijui wanaona aibu?
Kanisa litawalipa fidia.
Ukute na huku kwetu yapo hivyo hivyo ila watu wanajikaza tu.
Kuna raia wa Uingereza walikuwa brainwashed na TB Joshua. Ukiangalia documentary utaona.Nini kiliwasukuma BBC kutayarisha documentary hiyo?
Waziri wa kibuyu chetu cha asali alikwenda huko, sijui yeye alishuhudia nini3. TB Joshua alikuwa akiishi kwenye jumba mfano wa gereza na kundi kubwa la wanaoitwa "disciples" wanafunzi wake, wengi wakiwa wanawake vijana na vigori, walivyokuwa wanapatikana anajua yeye mwenyewe ila mmoja wa wahojiwa anasema alipewa na kazi na TB Joshua ya kuleta wanafunzi wa kike mabikira. Watu kuzuiliwa kama wako kifungoni na viongozi wa cults sio jambo jipya, mifano ni mingi sana kuanzia kwa jirani zetu hapa Kenya katika kisa cha Shakahola, huko kwingine duniani wamewahi kuwepo kina Jim Jones wa people's temple, David Koresh wa Waco n.k
Hawa BBC ndo waliibua yale madudu ya Kenya. Mwanzoni watu waliwadhihaki hivihivi baadaye serikqli ikachukulia issue serious na kugundua mambo mazito. Kama Hawa mashahidi wote wamefanya kazi kwa TB Joshua Tena kama mitume kwenye inner circle yake basi kuna jambo. Ukiangalia zile documentary wote wanaonekana wakihudumu. Huyu mwingira si alishitakiwa kuzaa na mke wa muumini alipotakiwa kwenda kupima DNA ya mtoto si aligoma why?Achana na imani...
Juzi Kenya wamezikwa watu wakiwa hai kwa hiari yao!! Itakuwa kubakwa, au huna habari za kesi ya Kenya.
hapa ndo siri ilipo!Nini kiliwasukuma BBC kutayarisha documentary hiyo?
KwambaMtu ana bakwa hadi ana abort mimba 5 mwingine 3 ?? Ume waona hao wana wake BBC lakini ? as a man sijaona cha kuni shawishi kubebeahq mimba mala 5 ata mmoja palee
Tunacho sema sisi ni hii trend ya wanawake wa ulaya kufungua case za claim za miaka ilio pita kuchafua watu
Part 1Mkuu hii umeiandika mwenyewe au una source? Nataka kuitumia sehemu kuelewesha.