Uchunguzi: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
Hatukubali tafiti za kipuuzi dhidi ya waafrika maarufu
Wakajifanyie na wao huko kwao
Unajua kubisha humu jf haisaidii kanisa wala mtu..
Ni kuposti BBC na kukanusha hata kwenye website zao, radio zao nk
 
Utafiti wao wa Uebert Angel uliishia wapi?

Wafanye tafiti watoe na mrejesho sio kupoteana tena
Kwanza sio utafiti, ni uchunguzi,
Pili, wewe ulitaka wafanuaje baada ya kutoa ripoti yao kama waandishi wa habari?
 
Ni kweli haya makanisa yanayoibuka kila siku na watu kujiita manabii na mitume, kuna mengi nyuma ya pazia
Na wewe usiwe kama BBC, ungoje mtu afe useme alikuwa mbakaji. Sema sasa hivi ni mtume na nabii gani ameficha mengi nyuma ya pazia.
Mtaje na utaje aliyoficha ili vyombo vya sheria viokoe mapema.
 
Mbona kama ushahidi hauna nguvu, mtu yoyote anaweza kuzungumza.

N.B MIMI SI MFUASI WA TB JOSHUA
Hata mi naona kama ulivyoona wewe...tena wazungu ndio wanatoa ushahid huo!.. yan mzungu kabisaa ukam lock up for 20 years mtu mweusi,seriously???
 
Na wewe usiwe kama BBC, ungoje mtu afe useme alikuwa mbakaji. Sema sasa hivi ni mtume na nabii gani ameficha mengi nyuma ya pazia.
Mtaje na utaje aliyoficha ili vyombo vya sheria viokoe mapema.
Kabisaaa walikua wapi hawa..? Mbona hawakum expose b4 wasubir mpaka afe??? Au kuna maslah wamedhurumiana???
 
Na wewe usiwe kama BBC, ungoje mtu afe useme alikuwa mbakaji. Sema sasa hivi ni mtume na nabii gani ameficha mengi nyuma ya pazia.
Mtaje na utaje aliyoficha ili vyombo vya sheria viokoe mapema.
Inahitaji uchunguzi kufikia hitimisho ndo maana nimetia shaka hayo mazungumzo yaloletwa na BBC.

Nasema kuna mengi nyuma ya pazia kulingana na ibada zenyewe zinavyoendeshwa, kuyajua yahitaji uchunguzi wa kina
 
Ushahidi wa unyanyasaji ulionea na mateso kutoka kwa mwanzilishi wa mojawapo ya makanisa makubwa ya kiinjili ya Kikristo duniani umefichuliwa na BBC.

Makumi ya waumini wa zamani wa Kanisa la Synagogue Church of all Nations - watano Waingereza - wanadai ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na utoaji mimba kwa lazima, uliofanywa na marehemu TB Joshua wa Nigeria.

Madai ya unyanyasaji katika eneo la siri la Lagos yamedumu kwa takriban miaka 20.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations halikujibu madai hayo lakini lilisema madai ya hapo awali hayana msingi.

TB Joshua, aliyefariki mwaka wa 2021, alikuwa mhubiri na mwinjilisti mwenye mvuto mkubwa na mwenye mafanikio makubwa ambaye alikuwa na wafuasi wengi duniani.

Matokeo ya BBC katika uchunguzi wa miaka miwili ni pamoja na:
  • Masimulizi mengi ya watu waliojionea matukio ya ukatili wa kimwili au mateso yaliyofanywa na Joshua, ikiwa ni pamoja na matukio ya unyanyasaji wa watoto na watu kuchapwa viboko na kufungwa minyororo.
  • Wanawake wengi wanaosema walinajisiwa na Joshua, huku baadhi wakidai kuwa walibakwa mara kwa mara kwa miaka mingi ndani ya boma hilo.
  • Tuhuma nyingi za kutoa mimba kwa lazima ndani ya kanisa kufuatia tuhuma za ubakaji na Joshua, akiwemo mwanamke mmoja ambaye anasema alitolewa mimba mara tano.
  • Simulizi nyingi za moja kwa moja zinazoelezea jinsi Joshua alivyodanganya kuhusu "uponyaji wake wa miujiza", ambao ulitangazwa kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Mmoja wa waathiriwa, mwanamke wa Uingereza, anayeitwa Rae, alikuwa na umri wa miaka 21 alipoacha shahada yake katika Chuo Kikuu cha Brighton mnamo 2002 na kuandikishwa katika kanisa. Alitumia miaka 12 iliyofuata kama mmoja wa wale wanaoitwa "wanafunzi" wa Yoshua ndani ya boma lake la kifahari huko Lagos.

"Sote tulidhani tuko mbinguni, lakini tulikuwa katika hali inayofanana na ya kuzimu, na huko kunatokea mambo mabaya," aliiambia BBC.

Rae anasema alinajisiwa na Joshua na kuwekewa aina ya kifungo cha upweke kwa miaka miwili. Dhuluma hiyo ilikuwa kali sana, anasema alijaribu kujiua mara nyingi ndani ya boma hilo.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations [Scoan] lina wafuasi wa kimataifa, wanaoendesha chaneli ya TV ya Kikristo iitwayo Emmanuel TV na mitandao ya kijamii yenye mamilioni ya watazamaji. Katika miaka yote ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, makumi ya maelfu ya mahujaji kutoka Ulaya, Amerika, Kusini Mashariki mwa Asia na Afrika walisafiri hadi kanisani humo nchini Nigeria kumshuhudia Joshua akifanya "miujiza ya uponyaji".

Takriban wageni 150 waliishi naye kama wanafunzi ndani ya boma lake huko Lagos, wakati mwingine kwa miongo kadhaa.

Rae in a BBC studio interview, wearing glasses and black top

Maelezo ya picha: Rae alisalia kwa miaka 12 katika boma la Joshua

Zaidi ya "wanafunzi" 25 wa zamani walizungumza na BBC - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - wakitoa ushuhuda wenye nguvu wa kuthibitisha waliopitia ndani ya kanisa, pamoja na matukio ya hivi majuzi zaidi katika mwaka wa 2019. Waathiriwa wengi walikuwa katika ujana wao walipojiunga mara ya kwanza. Katika baadhi ya kesi za Uingereza, usafiri wao hadi Lagos ulilipwa na Joshua, kwa ushirikiano na makanisa mengine ya Uingereza.

Rae na waliohojiwa wengine wengi walilinganisha masaibu yao na kuwa katika dhehebu la itikadi kali .
Jessica Kaimu, kutoka Namibia, anasema masaibu yake yalidumu kwa zaidi ya miaka mitano. Anasema alikuwa na umri wa miaka 17 wakati Joshua alipombaka kwa mara ya kwanza, na kwamba matukio ya baadaye ya kubakwa na TB Joshua yalisababisha atoe mimba mara tano akiwa huko.

"Haya yalifanyika kisiri... matibabu tuliyokuwa tukifanyiwa... yangeweza kutuua," aliiambia BBC.
Wengine waliohojiwa wanasema walivuliwa nguo na kupigwa kwa nyaya za umeme na mijeledi ya farasi, na mara kwa mara walikoseshwa usingizi.
Katika kifo chake mnamo Juni 2021, TB Joshua alisifiwa kama mmoja wa wachungaji wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Afrika.

Akiinuka kutoka kwa umaskini, alijenga himaya ya kiinjilisti ambayo ilijivunia makumi ya viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri na wanasoka wa kimataifa kati ya washirika wake.

Hata hivyo, alizua utata wakati wa uhai wake wakati nyumba ya wageni ya mahujaji wa kanisa ilipoporomoka mwaka wa 2014, na kuua watu wasiopungua 116.Uchunguzi wa BBC, ambao ulifanywa na jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari vya Open Democracy, ni mara ya kwanza watu wengi wa zamani wa makanisa kujitokeza kuzungumza juu ya rekodi hiyo. Wanasema wametumia miaka mingi kujaribu kupaza sauti lakini wamenyamazishwa kwa ufanisi.

Baadhi ya mashahidi wetu nchini Nigeria wanadai walishambuliwa kimwili, na katika kisa kimoja walipigwa risasi, baada ya awali kujitokeza kupinga unyanyasaji huo na kuchapisha video zenye madai kwenye YouTube.

Wafanyakazi wa BBC ambao walijaribu kurekodi picha za boma la kanisa hilo Lagos kutoka mtaa wa umma mnamo Machi 2022 pia walipigwa risasi na usalama wa kanisa hilo, na walizuiliwa kwa saa kadhaa.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi wetu. Haikuwajibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.
"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," iliandika.

Raia wanne wa Uingereza waliozungumza na BBC wanasema waliripoti unyanyasaji huo kwa mamlaka ya Uingereza baada ya kutoroka kanisani. Wanasema hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa.

Anneka pictured in BBC studio interview, wearing white jumper

Maelezo ya picha: Anneka anasema anaamini kuna waathiriwa wengi ambao bado hawajazungumza

Zaidi ya hayo, mwanamume Muingereza na mkewe walituma barua pepe kwa mashahidi waliojionea ushahidi wao wa mateso na video - ikiwa ni pamoja na rekodi za kushikiliwa kwa mtutu wa bunduki na wanaume wanaojiita polisi ambao pia ni wanachama wa Scoan - kwa Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria mnamo Machi 2010 baada ya kukimbia kanisa hilo. Katika barua pepe yake, mwanamume huyo alisema mke wake alishambuliwa kingono mara kwa mara na Joshua. Aliionya ubalozi huo kuwa raia wengine wa Uingereza bado wako ndani ya boma hilo wakikabiliwa na ukatili.

Pia anasema hakuna hatua zilizochukuliwa. Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza haikujibu madai haya, lakini iliambia BBC kwamba inachukulia ripoti zote za uhalifu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya raia wa Uingereza nje ya nchi, kwa uzito mkubwa.

Scoan inaendelea kustawi leo, chini ya uongozi wa mjane wa Joshua, Evelyn. Mnamo Julai 2023, aliongoza ziara ya kwenda Uhispania.

Anneka, ambaye aliondoka Derby nchini Uingereza na kujiunga na Scoan akiwa na umri wa miaka 17, aliambia BBC kuwa anaamini kuna waathiriwa wengine wengi ambao bado hawajazungumza. Anatumai hatua zaidi zitachukuliwa kufichua vitendo vya Joshua.

"Ninaamini Kanisa la Synagogue Church of All Nations linahitaji uchunguzi wa kina ili kujua ni kwa nini mtu huyu aliweza kufanya kazi kwa muda mrefu kama alivyofanya," alisema.

Ripoti ya ziada ya Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward
Kwa usaidizi na taarifa kuhusu unyanyasaji wa kingono, tafadhali wasiliana na Mtandao huu wa BBC Actionline nchini Uingereza. Na kwa habari zaidi juu ya madhehebu, tafadhali tazama The Family Survival Trust

BBC
Pia soma: BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua


Kwanini wasichunguze hawa manabii ambao hawajafa badala ya mtu ambaye hawezi kujitetea
 
1. Wanaoshuhudia madhila na utapeli ni walioukuwa watumishi na wanafunzi wa TB Joshua mwenyewe na kanisa lake, sio watu baki. Mmojwapo ni watu waliokuwa karibu kabisa naye kama mtu namba mbili baada ya TB Joshua.

2. Kwenye baadhi ya sehemu za clips zilizorekodiwa na kanisa hilo na ambazo ni public zilizotumiwa na BBC TB Joshua anaonyeshwa akifanya mambo ya ajabu mbele ya hadhara kama kupiga watu makofi kama sehemu ya huduma!

3. TB Joshua alikuwa akiishi kwenye jumba mfano wa gereza na kundi kubwa la wanaoitwa "disciples" wanafunzi wake, wengi wakiwa wanawake vijana na vigori, walivyokuwa wanapatikana anajua yeye mwenyewe ila mmoja wa wahojiwa anasema alipewa na kazi na TB Joshua ya kuleta wanafunzi wa kike mabikira. Watu kuzuiliwa kama wako kifungoni na viongozi wa cults sio jambo jipya, mifano ni mingi sana kuanzia kwa jirani zetu hapa Kenya katika kisa cha Shakahola, huko kwingine duniani wamewahi kuwepo kina Jim Jones wa people's temple, David Koresh wa Waco n.k

4. Hakuna mgogoro wowote ndani ya kanisa la SCOAN unaohusishwa na waathirika hawa walioamua kusema yaliyokiwa yanatendeka nyuma ya pazia, hivyo huwezi kusema hata ni watu wenye nia ovu ya kulimega hilo kanisa na kuanzisha lao.

5. BBC wanasema waandishi wao walirushiwa risasi na walinzi wa kanisa hilo walipokuwa wanachukua video. Kanisa lolote linaloweza kufikia kiwango hichi cha kujificha kutoka waandishi wa habari ni taa nyekundu.

6.Ni kweli jengo la kanisa la TB Joshua liliwahi kuanguka na kuua mamia ya watu kwa sababu ya kutofuata taratibu sahihi za ujenzi na TB Joshua akasema kulikuwa na ndege ndogo iliyokuwa ikizunguka katika jengo hilo iliyopelekea kuporomoka na kwamba pia lilikuwa na jaribio la mauaji dhidi yake. Hata hivyo Ushahidi wa wazi ni kwamba taratibu nyingi za ujenzi wa jengo hilo zilikiukwa lakini kwa sababu matapeli wa kidini kama yeye wamekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana katika serikali za Africa hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa.

7. BBC wamefanya uandishi wa kiuchunguzi "investigative journalism" sio utafiti "research" au forensic investigation ambayo sasa inapaswa kufanywa na polisi kuthibitisha zaidi yaliyoletewa hadharani na BBC. Yani kazi kubwa iliyofanywa na BBC ni kuwasikiliza waathirika takribani 30 kutoka sehemu mbalimbali, kuhakikisha hawajapanga "conspire" kusema walichosema, kuoanisha wanachosema"corroboration" na kisha kuwapa fursa kanisa la SCOAN la TB Joshua kuzungumzia tuhuma hizo ambapo walikataa kuwapa ushirikiano wowote.

Kazi ya ushahidi mwingine unaodaiwa na baadhi ya member hapa jukwaani kama ushahidi wa video wa watu wakibakwa ni suala la forensic investigation na mahakamani kama polisi wa Nigeria wataamua kufuatilia kesi hiyo. BBC wamefanya kazi yao uandishi wa kiuchunguzi kwa weledi mkubwa na wamemaliza.
 
Back
Top Bottom