Duh! Umeamua kuanzisha uzi baada ya kukusoma kwenye ule uzi ukijitenga na dini. Ngoja nikusome nione umeandika nini nijibu.
 
Kweli 🙏
 
Watajitokeza wengi, wa Tanzania bado wapo kimya sijui wanaona aibu?

Kanisa litawalipa fidia.

Ukute na huku kwetu yapo hivyo hivyo ila watu wanajikaza tu.
Waamini wanawatazama hawa manabii mambo leo kama miungu watu, na hao manabii wamewapumbaza akili kiasi hata wakisema lolote kwa waumini wao, wanaamini Mungu ndio amesema. Katika mazingira kama hayo ni rahisi sana nabii mambo leo kutumia udhaifu huo kuwafanyia matendo kama hayo anayotuhumiwa nayo Joshua.

Unaweza kujiuliza ni kwanini hawajitokezi hao waathirika? Fikiria mtu anaaminika na kuabudiwa na Rais, viongozi wakubwa wa serikali na wale wa vyombo vya usalama wanakimbilia kwake kutaka baraka zake, unafikiri binti masikini ukitupa tuhuma kama hizo na hata ushahidi huna unaweza kubaki salama?

Hawa manabii mamboleo wamezijenga 'biashara zao' kwa gharama kubwa sana na wanakula na wakubwa kwenye nchi zao, hawajakaa kitoto!
 
Nini kiliwasukuma BBC kutayarisha documentary hiyo?
Nini huwa kinawasukuma BBC kutayarisha documentaries nyingine mbalimbali?
Unachopaswa kuelewa ni kwamba chombo chochote cha habari huwa kina vigezo/checklist/threshold ili jambo fulani liwe habari , hii documentary ya TB Joshua ni habari ya kiuchunguzi tu iliyowekwa katika mtindo wa documentary.
 
Kwamba
Watu walibakwa seminary
wamekuja kusema uzeeni.....
We vipi mkuu. Mambo hayo yamechanganyika na woga wa kiimani.
Mtu ana bakwa hadi ana abort mimba 5 mwingine 3 ?? Ume waona hao wana wake BBC lakini ? as a man sijaona cha kuni shawishi kubebeahq mimba mala 5 ata mmoja palee

Tunacho sema sisi ni hii trend ya wanawake wa ulaya kufungua case za claim za miaka ilio pita kuchafua watu
 
Achana na imani...
Juzi Kenya wamezikwa watu wakiwa hai kwa hiari yao!! Itakuwa kubakwa, au huna habari za kesi ya Kenya.
 
Huu sio uchunguzi. Huu ni sawa na ubuyu wa Nifah tu. Wangemuomba hata cocastic Awafanyie uchunguzi kuliko huu ujinga waliouleta mbele za watu.
 
Umenishawiahi kuanza kuamini kuwa kuna kitu cha kutazama behind the altar

Ahsante mkuu
 
Nini kiliwasukuma BBC kutayarisha documentary hiyo?
Kuna raia wa Uingereza walikuwa brainwashed na TB Joshua. Ukiangalia documentary utaona.

BBC ina wajibu wa kuelimisha walipa kodi wa Uingereza wasiweze kutekwa mawazo katika cults hizi.

Lakini pia, BBC kama chombo cha habari wana wajibu wa kumulika uongo na kutupa habari zitakazofunua ukweli.

Nafikiri badala ya kuangalia motives za BBC - kimsingi kupanda mbegu za conspiracy theory dhidi ya BBC- ni bora tukahakiki kama habari zilizosemwa ninkweli au si kweli.

Na hatua yavkwanza ni kuangalia hizo episodes tatu ili kuelewa zaidi.
 
Waziri wa kibuyu chetu cha asali alikwenda huko, sijui yeye alishuhudia nini
 
Achana na imani...
Juzi Kenya wamezikwa watu wakiwa hai kwa hiari yao!! Itakuwa kubakwa, au huna habari za kesi ya Kenya.
Hawa BBC ndo waliibua yale madudu ya Kenya. Mwanzoni watu waliwadhihaki hivihivi baadaye serikqli ikachukulia issue serious na kugundua mambo mazito. Kama Hawa mashahidi wote wamefanya kazi kwa TB Joshua Tena kama mitume kwenye inner circle yake basi kuna jambo. Ukiangalia zile documentary wote wanaonekana wakihudumu. Huyu mwingira si alishitakiwa kuzaa na mke wa muumini alipotakiwa kwenda kupima DNA ya mtoto si aligoma why?
 
Wewe ndio hujaona cha kukushawishi pengine yeye Joshua aliona? Wewe unadhani wale vichaa unaona huko barabarani huwa wanabebeshwa mimba na vichaa wenzao?

Kila mtu anafanya mambo yake ana sababu zake, kama ni mambo ya matambiko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…