Sawa,ngoja tuone Sasa na hii kesi upande upi utashinda ndo tujue ukweli

Wanakuwaga na kesi lakini wanashinda which means wanawasingizia tu kama yule padre wa moshi mpaka dada mwenyewe alikiri kuwa alimsingizia
 
Nimekwambia nchi za dunia ya kwanza ikiwamo uingereza zinajali sana maslahi ya raia wao.
Ni ngumu kwao kutochukua hatua maslahi ya raia wao yanapoguswa.
Wewe unanipa mfano wa waarabu na watumwa wao blacks.
Asante na kwaheri!
Dunia ya kwanza kwenyewe haya mambo yanatokea sana tu na kesi nyingine huibuliwa hata miaka 20 baadaye, itakuwa Nigeria ambapo kuna ubalozi tu na polisi wao wanaonuka rushwa.
 
Hivi kwann siku zote mzungu ndio anajua sana matatizo ya mwafrika kuliko hata mwafrika mwenyewe na akija huwa anashambulia mwanaume mwenye nguvu na mamlaka?

Hawa wazungu mimi siwaamini hata kidogo.
Ni kwasababu mwafrika ni mjinga na mzembe, mtu mwenye kupuuzia mambo ya msingi.

Labda nikuulize, ni nani walimshambulia Tundu Lissu aliyekuwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni? Tena katika eneo linalolindwa muda wote?

Kama hujui, jiulize ni miaka mingapi imepita na kama ni sahihi kiongozi mkubwa kama huyo kushambuliwa kwa risasi na hadi leo wewe kama mwananchi hujajua alishambuliwa na kina nani na kwasababu gani.

Ni rahisi sana mtu mwenye pesa afrika kufanya uchafu wa kutisha, kuua, kubaka na hata kulawiti na wala asifanywe lolote. Ni kwanini? Serikali zetu ni serikali za 'kitu kidogo' yaani, RUSHWA tupu!
 
Hivi kwann siku zote mzungu ndio anajua sana matatizo ya mwafrika kuliko hata mwafrika mwenyewe na akija huwa anashambulia mwanaume mwenye nguvu na mamlaka?

Hawa wazungu mimi siwaamini hata kidogo.
Kwa sababu media nyingi za kiAfrica ni kama idara tu za mawasiliano za serikali, watu maarufu na matajiri, pia uchawa umekithiri sana kwa waandishi wa habari wa Africa.
 
Tunapaswa kuwa wafuasi wa Yesu Kristo, si wanadamu na dini zao, ziwe za kikristo au vinginevyo. Kamwe tusiwe wafuasi wao hata kama wana majina makubwa mno ya kidini. Yesu pekee ndiye Mchungaji Mwema!
 
Ni nani anafadhiri hi project ya kumchafua mwamba?
 
Umeongea vizuri sana mkuu, ila hapo mwisho nimeshindwa kukuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu akifa ndo unaropoka huo ni uongo watoe video tuone wanavyonyanyaswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…