Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Tatizo nyumba moja ina vyumba 7+vibanda vya uani 5,choo kimoja hapo unategemea nini?
Je mtu akishikwa na tumbo

Ova
Hizi nyumba za “you face me I face you” zilitakiwa kuwa na Indian Toilets tatu na shower rooms tatu au nne. Yake maisha ni zaidi ya maisha ya hostel.
 
Tatizo kubwa ni upatikanaji wa maji tiririka ndiyo kunafanya wengi wasijenge nyumba self contained.
Asante kwa kusema 'contained' wengi wetu humu wamelemaa sana wanasema 'container'. Kinge kinatutesa Watanzania wengi.
 
Hizi nyumba za “you face me I face you” zilitakiwa kuwa na Indian Toilets tatu na shower rooms tatu au nne. Yake maisha ni zaidi ya maisha ya hostel.
Walipojenga zamani idadi ya watu haikuwa kubwa,sasa sahv familia nzima inalala kwenye chumba kimoja

Ova
 
Kijijini kwetu tangu nikiwa mdogo,kila kitanda kina kibeseni chini kwa hiyo usiku ni kukojoa kwenye hicho kibeseni na kila asubuhi ni kumwaga kojo huko nje na kusafisha beseni na kuirudisha uvunguni mpaka wa leo kwetuhamna mtu anaendaga usiku nje labda anaumwa tumbo la kuhara ndo asindikizwe chooni,wanasema usiku una mambo mengi
Asa juzi nimeenda kibeseni kipo kama kawa nimeshindwa kukojoa sema sikubanwa ningekojoa zangu asubuhi nkaenda kumwaga kojo kama kawa
 
kwema Wakuu!

Tuachane na mambo ya Ukraine na Urusi.
Leo sitaki kupotezea muda watu.

Moja ya mambo yaliyonishangaza tangu nilipotoka nyumbani miaka 10 iliyopita ni kuona wakazi wengi kuwa na tabia ya kukojolea kwenye makopo au ndoo nyakati za usiku.

Hivi inakuwaje mtu alale na Mikojo wakati haumwi?
Ni uvivu wa kutoka nje usiku au ni Woga?

Kinachoshangaza zaidi ni kuona tabia hii ipo mpaka Kwa wanaume. Hivi mwanaume mzima unakojolea kwenye kopo au ndoo kweli badala ya kutoka nje na kujisaidia chooni.

Unakuta mtu kaoa kabisa alafu yeye na Mke wake wanakojolea kwenye ndoo au kopo. Kwa kweli hili sio uungwana Kabisa.

Halafu ndoo hiyo hiyo ati mtu anaogea au kufulia😀😀 hii kuna uchafu zaidi ya huu? Ukimuuliza atakwambia ati ndoo ameiosha, upuuzi mtupu.

Uchunguzi huu unawahusu zaidi Wale wenye nyumba za kupanga ambazo sio Self-container, isipokuwa Choo kipo Kwa nje kimejitenga.

Pia baadhi ya wenye nyumba ambao vyoo vyao vipo Kwa nje.

Ushauri wangu, unapoenda ugenini kusalimia uwe Makini sana, unaweza ukadhani unaoga kumbe unajipaka mikojo ya watu japokuwa watakuambia wanaisafisha hiyo ndoo.

Mikojo na mavi no uchafu, ni najisi, watu lazima muwe wasafi bhana sio muwe Kama majini.

Wito: wenye tabia hii nawasihi mubadilike, acheni kukojolea kwenye makopo au ndoo, alafu ndoo hizohizo mnaogea na kufulia nguo. Huo ni UCHAFU.

Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Buza, Dar es salaam
We jamaa nimekumaindi ya leo kali kunguru kanyea ugali😅
 
Huo ni moja ya magonjwa ya akili,mtu aliyetimamu hawezi kukojoa kwenye kopo au ndoo,halafu akae na huo uchafu mpaka asubuhi aende kuumwaga,kuwa na ugonjwa wa akili siyo kuokota vitu jalalani tu au kukimbia ovyo barabarani bila nguo,

La hasha,yapo matatizo mengine yanaweza yakamkuta mtu yanayosababishwa na akili kuwa ngonjwa,moja wapo ni hili la kujisaidia kwenye makopo na ndoo.
Kama kukaa na haja ni ugonjwa wa akili basi wote tu wagonjwa wa akili! We mbona unatembea na Mah.Vee full time umeyabebebelea kwenye utumbo mkuu😅😅😅 af unajiona una akili sana?
 
Tatizo nyumba moja ina vyumba 7+vibanda vya uani 5,choo kimoja hapo unategemea nini?

Je mtu akishikwa na tumbo

Ova
Hahahahahah ni noma yani! Matundu mawili ya choo wapangaji 12😂 af vyoo vya kupangiana zamu kuosha!
 
Kama kukaa na haja ni ugonjwa wa akili basi wote tu wagonjwa wa akili! We mbona unatembea na Mah.Vee full time umeyabebebelea kwenye utumbo mkuu😅😅😅 af unajiona una akili sana?
kasahau kwamba bladder ya mkojo anatembea nayo imejaa ammonia
colon nzima limejaa 'nya' na anatembea nayo
 
Kama Huna self amka usiku kakojoe choo cha nje, uvivu wa kulala na mikojo ndani unatia aibu.
Tatizo kubwa ni upatikanaji wa maji tiririka ndiyo kunafanya wengi wasijenge nyumba self contained.
 
Hizi nyumba za “you face me I face you” zilitakiwa kuwa na Indian Toilets tatu na shower rooms tatu au nne. Yake maisha ni zaidi ya maisha ya hostel.
Long time enzi za ubeach boy nlipanga chumba moja national housing zile mara nying kujisaidia kuoga nlikuwa nakwenda nyumba za jirani
Maana asubuhi bafuni foleni

Ova
 
Alafu sasa cha ajabu ni kwamba sio kwamba choo kilipo labda ni nje kabisa kwamba mtu anaogopa,, yaan unakuta nyumba imezungushiwa ukuta choo kipo uwani tu mtu anakojoa ndani alafu ni mwanume!!

Hii tabia ni ya kijinga mno
Ni kweli, ni ujinga sana.
 
Acha watu waishi mbona wazungu wanauza chupa special kabisa la kulimwaga...
74346001-1948321171~2.jpg
 
Back
Top Bottom