Ufisadi unavyopangwa na Wizara wakati wa bajeti. Hii BYD nani dealer hapa nchini??

View attachment 3489221
Kanchi kenu kalichelewa kuadpot EVs, kama kawaida kila siku mko nyuma
Sahihi mkuu, wasichoelewa ni kuwa kwa kuwa sisi tuko ndani ya EAC, negotiations nyingi zina mirror Nchi zote wanachama. Imagine Kenya awe na 0% import duty kwenye EV halafu sisi tuna stay kwa 35% kama nchi tutakuwa tunapata faida gani against Kenya??? Wakati sisi tunakuja kuadopt Kenya anakuwa tayari ashatumia magari, yamezoeleka na pengine ashaatract assembling ya EVs nchini kwake, na kwa kuwa zinazalisshwa ndani ya EAC zikiingia Tanzania zinakuwa na dity ya 0%.

Wabongo baaana;
 
Kuna upigaji mkubwa sana kwenye procurement.
Misamaha ya Kodi za kibiashara za nje imekuwa sana.

Kila kiti ni kununua TU, hakuna kutengeneza kitu hapa nyumbani TZ,
 
IMF imedai serikali imetumia vema fedha katika miradi yake

IMF na WB ni wafanyabiashara kama kausha damu vile
Cha msingi wao wapate faida
Na watatoa takwimu za kubumba ili tukope tena

Vp mabasi ya mwendo Kasi BRT
Ingekuwa ni pesa ya mtu kutoka kwake binafsi mradi ungeshakufa kitambo na tungebaki na Ile miundo mbinu ya barabara kama kumbukumbu ya mradi
 
Elimu ya vyeti na akili ni vitu viwili tofauti.
Inakuwa bora zaidi kama vyote vinaenda sambamba (akili, elimu na vyeti).

Wasomi wenyewe ndio kama Hawa

Tulia akxon
Kabudi aka Mzee wa tokea jalalani
Mkumbo
Mpango

Hapo hakuna jipya
Wanajali matumbo yao na teuz zao na watoto wao tokea ikulu
 

Wewe unajua Mkataba wa AGOA
Rwanda nguo za mitumba wamepiga marufuku kitambo
Tz na KNY na Ug ni wafuqta upepo

Kutumia tu gesi ya Mtwara ktk mqgri imekuwa shida sembuse hayo magari ya kuchaji
Hiyo ni mirqdi ya watu
 

Wanaondoa kodi kwenye hayo magari ya umeme wakati wanaongeza TOZO kwa Mnyonge!
 
Wewe unajua Mkataba wa AGOA
Rwanda nguo za mitumba wamepiga marufuku kitambo
Tz na KNY na Ug ni wafuqta upepo

Kutumia tu gesi ya Mtwara ktk mqgri imekuwa shida sembuse hayo magari ya kuchaji
Hiyo ni mirqdi ya watu
Kwani mkataba wa AGOA ni wa nguo za mtumba mkuu?? Daau

Tufuatilieni vitu aisee!

hivi ni vitu vya kitaalamu - sio siasa. Hata kikiingia chama kingine utaalamu utabaki uleule, kama ni kodi zitachapwa tu ama kuondolewa. Refer, Kenya - hata baada ya Ruto kuingia bado kodi zinatozwa sana na mpya zimenzishwa na zingine zimetolewa (hadi wananchi wakaandamana kisa finance bill). Ukielewa haya hata hausumbuki.

Hiyo unayosema gesi ya Mtwara imekuwa shida - sasa unaongea hadithi. Adoption ya gesi inazidi kuongezeka hauwezi kilimganisha na miaka 7 iliyopita. Dangote anatumia gesi kwenye magari yake yote; vituo vimeongezeka hadi kigamboni kuna kituo cha gesi (nadhani wameshaanza)

Wewe kama hauoni umuhimu wa sera hii, enjoy sera zingine.. mbona kuna misamaha kibao tu? Yaani huu mmjoa wa mgari ambayo wewe hutumii uwe nongwa? Shida ya ujamaa unaamini kwenye heri tukose wote (loose loose).

Hao Rwanda unaowasifia - kuna bidhaa za viwandani nyingi tu wananunua kwetu ikiwemo cement, Vioo, tiles, soft drinks nk. Wabongo hatujikubali kabisa.. hata Kenya kwa sasa kitu cha msingi sana anachotuuzia kwa wingi ni sabuni za jama, sausage na blueband.. wakati sisi tunamuuzia bidhaa kana vioo, transformer za umeme, tiles nk hapo hujasema kuhusu vyakula
 
Mafuta ya kula mbona bei bado ni zilezile tu za kabla ya bajeti hasa alizeti.
 
"Bajaji nyingi" Nyingi maana yake ni nini?
Hizo ni lugha za kizembe tu! Yaani bajaji unazitolea mfano, halafu hujui ni ngapi, wewe umeona ni nyingi. Nyingi!

Nakurudisha kwenye gari ya umeme. NIi gharama kubwa kwa nchi kuliko kuendesha gari ya mafuta. Hii ni nchi ambao hata waya wa umeme unaagizwa nje. Usiangalie hadithi za gharama za kuagiza mafuta. Kwani zinaibiwa ngapi kutoka hazina? Kwani hao wajali kiasi hicho?
 
View attachment 3489221
Kanchi kenu kalichelewa kuadpot EVs, kama kawaida kila siku mko nyuma
Kuna mtu hapa JF anasema Miafrika ndo tulivyo.
Kwa hiyo unaona ni jambo la kuwahiana. Yaani wengine walianza zamani kuondoa kodi, eti?
Mtindo huo ndo uliotumika kuondoa kodi kwenye mafuta ya kula yasiyosafishwa, eti Kenya na Uganda walishaondoa. Kumbe mwenye biashara aliwafuata mmoja mmoja.

Spika naye akaongeza mishahara ya wabunge kwa kisingizio kwamba wenzetu nchi jilani wana mishahara mikubwa. Rubbish!

Usiendesha nchi kwa kuiga wakati unajua walioko Ikulu wanatofautiana maono na ubora.
 
Kwa hiyo BYD alipita Afrika, Latin America, Ulaya, Asia na Australia akiwashawishi waondoe kodi? Maana huko kote BYD wanauza EVs
 
Huwa sipendi sana watu wanao- argu bila kuzingatia context. Inafanya kukosa mantiki. Hili sio professional group kwamba kila kitu kitakuja na actual data.. lakini kwa context public transport dunian ina run cost effectively kwa kutumia nishati mbadala tofauti na mafuta. Na tumeona Tanzania Bajaji na Bolt nyingi zinatumia gesi na hii utaona kwenye ongezeko la vituo vya gesi DSM.

wakati unasema kurun gari ya umeme ni costful lakini umeshindwa kuquantify ni cost kias gani halafu unanilaumu mimi kwa kusema 'bajaji nyingi' - very poor.
 
Tatizo la Tanzania wenye maamuzi wengi wanawaza ufisadi tu, ndo maana mafisadi yanapewa viti vya mbele kwenye mifumo ya utawala. Tanzania misamaha ya kodi haileti unafuu wowote kwa wananchi wa kawaida. Niambie ni kitu gani nchi hii kimesamehewa kodi wananchi wana-enjoy unafuu wake. Bidhaa zinazotozwa kodi na zile zisizotozwa kodi kwa nchi yetu vyote viko sawa, wanaonufaika na misamaha ya kodi ni mafisadi lakini sio wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…