UFISADI: Waziri Mkuu amsimamisha Mhazini wa TPA na wengine. CAG aagizwa kufanya ukaguzi haraka

UFISADI: Waziri Mkuu amsimamisha Mhazini wa TPA na wengine. CAG aagizwa kufanya ukaguzi haraka

Selikali ya MATUKIO ikiendeleza Maigizo.

Mane mane tekeli.

#TUMEWACHOKA.
Kazi ya Usalama wa Taifa bongo ni kuwashitaki wezi kwa waziri mkuu.
Kazi za mashirika na taasisi za kiusalama nchi nyingine ni kudhibiti mianya yote ya uhalifu, na uhalifu ukitokea basi wahalifu hufikishwa mahakamani mara moja na mashirika hayo hubadili mfumo wa kudhibiti mapato na kuachana na ule wa zamani.
Bongo tuko nyuma sana, we are not proactive at all
 
Waziri mkuu kasimu majaliwa leo 27/12/2020 amewasimamisha kazi mkuu wa kitengo cha fedha wa bandari ya TPA dar es salaam na maafsa wengine na kuitaka ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika bandari za tanga,mtwara ,,kyela,mwanza na Dar as salaam haraka.

Waziri mkuu amekagua mapato na matumizi na kubaini dosari hizo leo alipoitembelea bandari ya dar es salaam na kukuta madaudu

My take :tukutane mahakami

USSR
Hivi mtu akitumbuliwa si anabaki na mshahara wake ule ule.
Serikali itaingia gharama sana maana wengi wametumbuliwa hadi sasa
 
Waziri mkuu kasimu majaliwa leo 27/12/2020 amewasimamisha kazi mkuu wa kitengo cha fedha wa bandari ya TPA dar es salaam na maafsa wengine na kuitaka ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika bandari za tanga,mtwara ,,kyela,mwanza na Dar as salaam haraka.

Waziri mkuu amekagua mapato na matumizi na kubaini dosari hizo leo alipoitembelea bandari ya dar es salaam na kukuta madaudu

My take :tukutane mahakami

USSR

Hali ya kifedha ya nchi ni mbaya sana inabidi wote waanze kwenda kukagua vibubu!!! Tafadhalini ziachieni benki zifanye biashara ya forex without interference ; let them negotiate applicable exchange rates in the transactions na wateja wao!! In no time mtaona improvement kwenye forex reserves zenu!!!! Over regulation has always been counter productive.
 
Cha ajabu Kakoko ndio kapewa kazi ya kuunda tume ichunguze upotevu wa hela za bandari hahahaa!
Wakati mwingine nikimsikiliza waziri mkuu nabaki kuwaza mambo mengi sana.
Hela imepotea kwenye ofisi yangu halafu mimi mwenye ofisi niunde tume ichunguze.
Uchawi upo
Yule mkurugenzi wa Bandari kakoko kamuacha hahahah kakoko hoyee!!
 
Hali ya kifedha ya nchi ni mbaya sana inabidi wote waanze kwenda kukagua vibubu!!! Tafadhalini ziachieni benki zifanye biashara ya forex without interference ; let them negotiate applicable exchange rates in the transactions na wateja wao!! In no time mtaona improvement kwenye forex reserves zenu!!!! Over regulation has always been counter productive.
Wi a ini ze raiti traka. MPJ 2018.
 
Cha ajabu Kakoko ndio kapewa kazi ya kuunda tume ichunguze upotevu wa hela za bandari hahahaa!
Wakati mwingine nikimsikiliza waziri mkuu nabaki kuwaza mambo mengi sana.
Hela imepotea kwenye ofisi yangu halafu mimi mwenye ofisi niunde tume ichunguze.
Uchawi upo
Watakuambia Kakoko ni mbobezi kumbe geresha tupu! Toka akiwa Tanroad.
 
hii kweli inatisha, inamaana kuna baadhi ya watumishi wa TPA DSM bado sio waadilifu hadi leo hii?! aisee hao ni watu wasio faa wala kuonewa huruma.
Hongera mhe waziri mkuu kwa kuchukua hatua, sasa cheche za Mhe. Majaliwa zinaonekana. safi sana
 
Huyu ni viti maalumu hizo ni sinema za ccm ,kikwete aliwahi kwenda kariakoo kufanya Sanaa kama hizi
 
ufisadi, ufisadi, ufisadi ndio kansa ya taifa letu....japo imebaki kwa kiwango kidogo lkn madhara yake ni makubwa sana hivyo dawa ya kansa na mionzi au "kukata" eneo lenye kansa
 
Leo tarehe 27/12/2020 Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa amefika katika bandari ya Dar es Salaam

More to follow

=====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalum katika bandari za Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara, Tanga na Kyela kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Pia Waziri Mkuu amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bibi Nuru Mhando pamoja na Meneja wa Matumizi ya Fedha wa TPA, Bibi Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada kupokea ripoti ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na CAG katika hesabu ya Bandari ya Kigoma kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019. Lengo la ukaguzi huo lilikuwa kujiridhisha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 27, 2020) katika kikao chake na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kilichofanyika katika ofisi za TPA jijini Dar es Salaam. Amesema taasisi hiyo imebeba taswira ya uchumi wa Taifa, lazima kazi ifanyike vizuri.

Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Bodi ya Bandari Tanzania ihakikishe kwamba mamlaka hiyo inafanyakazi kwa weledi na isisite kuchukua hatua kwa mtumishi atakayebainika kutenda makosa na isimbebe kwa namna yoyote.
It does not make sense kuwasimamisha mameneja na kumuacha Mkurugenzi Mkuu
 
Back
Top Bottom