UFISADI: Waziri Mkuu amsimamisha Mhazini wa TPA na wengine. CAG aagizwa kufanya ukaguzi haraka

Waziri mkuu kasimu majaliwa leo 27/12/2020 amewasimamisha kazi mkuu wa kitengo cha fedha wa bandari ya TPA dar es salaam na maafsa wengine na kuitaka ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika bandari za tanga,mtwara ,,kyela,mwanza na Dar as salaam haraka.

Waziri mkuu amekagua mapato na matumizi na kubaini dosari hizo leo alipoitembelea bandari ya dar es salaam na kukuta madaudu

My take :tukutane mahakami

USSR
Duuuuuh jamaa yangu toka Kijiji kimoja Robert Madaraka nilivyomfahamu kwa uadilifu ni nn kimemsibu Genius huyu
 
Kitu Kama ufisadi umekwisha hivi!!!Bado upo?.Why???
ufisadi sio kuiba pesa za umma tu. hata kutumia vibaya Kodi na rasilimali za umma ni ufisadi, kwa akili ndogo tu unaweza kujenga vipo ikulu nyingine ya bilioni 500 na ushehe huku wanafunzi wanakosa vyoo na madarasa? Hali we ni mpitaji ukifika mda wako unaondoka anakuja mwingine madaraka ni sawa na siti ya daladala.
 
Leo tarehe 27/12/2020 Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa amefika katika bandari ya Dar es Salaam

More to follow

=====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalum katika bandari za Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara, Tanga na Kyela kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Pia Waziri Mkuu amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bibi Nuru Mhando pamoja na Meneja wa Matumizi ya Fedha wa TPA, Bibi Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada kupokea ripoti ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na CAG katika hesabu ya Bandari ya Kigoma kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019. Lengo la ukaguzi huo lilikuwa kujiridhisha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 27, 2020) katika kikao chake na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kilichofanyika katika ofisi za TPA jijini Dar es Salaam. Amesema taasisi hiyo imebeba taswira ya uchumi wa Taifa, lazima kazi ifanyike vizuri.

Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Bodi ya Bandari Tanzania ihakikishe kwamba mamlaka hiyo inafanyakazi kwa weledi na isisite kuchukua hatua kwa mtumishi atakayebainika kutenda makosa na isimbebe kwa namna yoyote.
Turudi hapa tena
 
Hapa kulikuwa na namna namna ya kulindana hasa Kakoko alikuwa analindwa na Hayati, Ila mama kanifurahisha sana kala kichwa mwenyewe.
 
Takukuru wamemaliza na Rais amefanya maamuzi

Tanzania iko imara sana

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote 😍🇹🇿🔥
 
Hapa kulikuwa na namna namna ya kulindana hasa Kakoko alikuwa analindwa na Hayati, Ila mama kanifurahisha sana kala kichwa mwenyewe.

Kama makonda eee🙄🙄🙄
Kwa taarifa tuu Serikali haina urafiki.
Uchunguzi ulitakiwa kufanyika na umekamilika, sasa serikali imetekeleza
Safi Madame President Samia Suluhu Hassan
 
hapo Bandarini panahitaji Fagio la chuma,
Hakuna msafi hata mmoja wote wananuka ufisadi hapo.
hao ndio wanao tafuna nchi yetu
 
Hayawi hayawi yamekuwa. Yule aliyeseama ni untouhable yuko mikono salama
 
Back
Top Bottom