UFISADI: Waziri Mkuu amsimamisha Mhazini wa TPA na wengine. CAG aagizwa kufanya ukaguzi haraka

UFISADI: Waziri Mkuu amsimamisha Mhazini wa TPA na wengine. CAG aagizwa kufanya ukaguzi haraka

Kakoko ajichunguze mwenyewe upotevu wa pesa yeye akiwa bado ofisini ......haya mapya.....ila tulisema huyu atamuweza kakoko ?? Sijui labda ......
Ni kweli hawa Wahasibu ni watekelezaji tu, hili soo ni la Deus Kakoko tu
 
Ushawahi kuwa Supervisor na mmoja wa unao wa supervise ni Mtoto wa Bosi?

Status ya PM inatia shaka sana. Lilipobomoka daraja huko Dodoma, PM alihangaika na site engineer bila kuwagusa waziri mhusika, Katibu Mkuu na CEO wa TANROADS waliokuwa wamemzunguka. Hata amri yake ya kumhamisha site engineer ikapuuzwa.

Hapa sasa anafokea wakurugenzi wa idara za TPA huku viongozi wa wizara husika na CEO wa TPA wakimkodolea macho tu. Interesting!
 
Ushawahi kuwa Supervisor na mmoja wa unao wa supervise ni Mtoto wa Bosi?

Sawa mkuu. Anyway, kwa sisi tunaofanya kazi kwenye mifumo inayofanya kazi tukiona tukio la aina hiyo katika nchi yetu tunapata maumivu kweli. Unajiuliza, kuna ulazima wa mtu kama PM kwenda public namna hiyo? For what?

Ni rahisi wapuuzi kukuita si mzalendo; unashabikia upinzani; n.k. But you really feel the pain of embarrassment. Sijui uliona ile posture ya kiburi ya CEO alivyomjibu PM kwa nini site engineer hakuondolewa na hawezi kuondolewa? Hakumwambia chochote wakati anatoa agizo hadi alipokuja kushangaa one week later. He had just ignored the PM!
 
Pale Kwa Mkemia Mkuu kaulizie kuhusu yule Mtoto aliongoza kura za maoni za Kawe jinsi alivyo na nguvu zisizo mithilika
Sawa mkuu. Anyway, kwa sisi tunaofanya kazi kwenye mifumo inayofanya kazi tukiona tukio la aina hiyo katika nchi yetu tunapata maumivu kweli. Unajiuliza, kuna ulazima wa mtu kama PM kwenda public namna hiyo? For what?

Ni rahisi wapuuzi kukuita si mzalendo; unashabikia upinzani; n.k. But you really feel the pain of embarrassment. Sijui uliona ile posture ya kiburi ya CEO alivyomjibu PM kwa nini site engineer hakuondolewa na hawezi kuondolewa? Hakumwambia chochote wakati anatoa agizo hadi alipokuja kushangaa one week later. He had just ignored the PM!
 
Hii Awamu ya 5 ndiyo pesa inapigwa kuliko kawaida. Imagine CAG Prof Assad kwa miaka 3 aligundua ufisadi wa Tsh 2.4 Trillion. Alipohoji akafukuzwa kazi
Acha kupotosha mkuu. Unaweza kueleweka bila kuweka uongo. Mkataba ukiisha akateuliwa mwingine ni ujinga kusema kafukuzwa kazi.
 
Acha kupotosha mkuu. Unaweza kueleweka bila kuweka uongo. Mkataba ukiisha akateuliwa mwingine ni ujinga kusema kafukuzwa kazi.
Nenda ukapimwe akili zako pengine unatumia za panzi. Kwa Mtanzania mwelewa hawezi kubisha hoja ya Prof Assad
 
CAG wa sasa hivi anakumbushwa majukumu yake, inamaana hakuna ukaguzi wowote anaoufanya wanasubiri wapike data
Kwanza uwezo wake ni mdogo sana. Ma Internal Auditors na External watakuwa wanamchemsha tu. Kosa kubwa sana walipomtoa Assad msema kweli na anayeifahamu Auditing. Yaani kila siku najiuliza ni kosa gani alilotenda Assad? Daah kwenye miti hakuna wajenzi. Au ni jungu lilipikwa maana mijizi ilikuwa inaumbuliwa? Maana maFisadi jua wana nguvu kubwa sana pia.
 
Nenda ukapimwe akili zako pengine unatumia za panzi. Kwa Mtanzania mwelewa hawezi kubisha hoja ya Prof Assad
Teh teh teh. Sasa hapa panzi nani! Au basi weye utakua nzige kabisa. Mimi sijazungumzia hiyo hoja ya Assad. Mimi nimekushauri uache kupotoshwa kuwa alifukuzwa kazi ilhali unajua kuwa mkataba wake ulifika kikomo na mteuzi halazimiki kumteua tena. Sasa hapo unataka kusema panzi siyo wewe kweli.

Nyumbu buana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hao Nuru Mhando na Witness Mahela subordinate wake ni kondoo wa sadaka tu. Nuru Mhando hawezi kufanya chochote bila maagizo ya Deus Kakoko. Deus Kkoko ni Mkurugenzi Mkuu, na amewekwa hapo na Meko mwenyewe kwa kuwa wanafahamiana naye kuanzia Meko akiwa Waziri wa Ujenzi na Deus Kakoko akiwa Meneja Mkoa TANROADS. Kuna uzi unamhusu kakoko, ngoja tuulete
Tafadhali naomba mni-tag mkileta huo Uzi.
 
Leo tarehe 27/12/2020 Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa amefika katika bandari ya Dar es Salaam

More to follow

=====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalum katika bandari za Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara, Tanga na Kyela kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Pia Waziri Mkuu amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bibi Nuru Mhando pamoja na Meneja wa Matumizi ya Fedha wa TPA, Bibi Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada kupokea ripoti ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na CAG katika hesabu ya Bandari ya Kigoma kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019. Lengo la ukaguzi huo lilikuwa kujiridhisha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 27, 2020) katika kikao chake na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kilichofanyika katika ofisi za TPA jijini Dar es Salaam. Amesema taasisi hiyo imebeba taswira ya uchumi wa Taifa, lazima kazi ifanyike vizuri.

Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Bodi ya Bandari Tanzania ihakikishe kwamba mamlaka hiyo inafanyakazi kwa weledi na isisite kuchukua hatua kwa mtumishi atakayebainika kutenda makosa na isimbebe kwa namna yoyote.
Kitu Kama ufisadi umekwisha hivi!!!Bado upo?.Why???
 
Akitoka hapo aanze ziara za nchi nzima kuzindua viwanda 100@mkoa, vilivyojengwa kwenye awamu hii ya Tanzania ya viwanda. Hii itasaidia wale watanzania 12.5m wa kura za kwenye mabeg wawe na uhakika wa ajira.
mmmmmmmmmmmmm!
 
tena namuomba Mhe. waziri Mkuu asipunguze kasi anayo enda nayo kwa sasa, huu ndio mwendo sikuzote nilikuwa natamani, kamwe asikubali kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa, ukali ni muhimu sana ktk mambo ya msingi ya taifa hakuna kuchekeana wala kulindana. hii ndio awamu ya lala salama.
tena mafisadi wote wafilisiwe mali zao wakipatikana na hatia.
 
Back
Top Bottom