Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Nikisoma Uzi kama huu nashangaa sana kwamba wizara ya kilimo na taasisi zinazohusika na mambo haya ya mifugo wanafanya Nini? Kwa Nini pasiwepo mkakati WA makusudi kuboresha mbegu za kienyeji ili kuongeza tija?
Unalolisema ni kweli kabisa lakini shida inakuja hao Serekali wana tambua ufugaji ni nini? kuna saa tunapata shida mpaka unafika mahala huamini unachokutana nacho pindi unakwenda kwenye hizo ofisi husika kwaajili ya kuomba msaada wa kitaalamu kwaajili ya kupata msaada wa kinacho kukabili.
 
Hongereni wakuu kwa kufuga,ukiachana na uzoefu, ushauri wangu kwenu ni kuwatumia wataamu wa mifugo (vets) kama sehemu ya input ktk biashara zenu
Tunaupokea ushauri wako na tunaufanyia kazi Ubarikiwe.
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.
Habari kaka, Nimependezwa sana na ujumbe wako ila ningependa sana kupata mawasiliano yako. Natamani kujifunza sana kutoka kwako
 
Mbuzi wangu ana miezi 10 tangu azae uzao wake wa mwisho,.. Ajabu ni kwamba ana mimba kubwa na ni wiki ya 3 sasa anaonyesha dalili za kuzaa lkn hazai na dalili zinapotea na kuanza tena,.. Nini kifanyike
 
Samahani kulitatua hilo ningalikushauri umshirikishe vet aweze kumkagua vyema maana naona inawezekana ikawa shida inayohitaji uchunguzi wa kina na kitaalamu zaidi.
 
Kweli kabisa unacho kisema lakini mtihani unakuja pindi unapo ingia ktk huo mradi na umeshakopa pesa umewekeza hapo halafu mara wanaanza kudondoka kisa mafua, mara hawa zai vyema kumbe kijana hawachungi vyema wanakosa malisho bora. Mara Mimba zinatoka sababu haojulikani lazima utafiti ufanyike. Ndio maana nasisitiza kila mara kwanza ni kutembelea wafugaji wenzako kupata ABC za ufugaji ndipo uanze sasa ufugaji. Nawapongeza sana wale wote ambao wananitafuta nawapa kile nilicho nacho ktk tasnia hii, sio kwamba mimi ni mjuzi sana ila namimi bado najifunza ktk hilo. Tujifunze pamoja tufuge pamoja. Mbarikiwe sana
 
..ukimsikiliza huyu mfugaji wa mbuzi na wewe utatamani kufuga.

View: https://www.youtube.com/watch?v=rFSqNDDfQbY

cc MUBENDE, Malila

Naam,

Hili game nililifanya Mkuranga hadi raha, wizi ulinifanya nibadili gear angani, kuna ndugu mmoja amenitafutia mbegu bora kabisa ya mbuzi inaitwa Isiolo, nimeshapata shamba salama la kufugia. Mbuzi watamu sana kuwafuga kibiashara, kila mara wateja wako hewani. Kipindi cha uchaguzi mbuzi nilikuwa napiga hadi laki na nusu pale Mkuranga, looh
 
Isiolo anakuuzia kwa bei gani?
 
Mungu akubariki sana ktk ufugaji wako, uwe mfano bora kwa wafugaji wachanga.
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu bado nawasisitiza sana ktk kututembelea wafugaji wenzenu ili muweze kupata ABC za ufugaji, nawashukuru sana wale wote walio kuja kwangu kwaajili tujifunze pamoja ktk ufugaji huu. Ktk ufugaji changamoto ni nyingi nilazima uzikubali ili uweze kufikia malengo yako kwahiyo kujifunza hakuishi daima. Mungu awabariki sana na kuwjaalia kila yaliyo Mema ktk mashamba yenu.
 
Hapo sw ngoja n mm nijipange. Niweke isiolo majike n dume moja tu
 
Kobe na nyoka sidhani kama utapata watu mkuu.
Monduli Arusha kulikuwa na zoo sijui Bado IPO ila walikuwa na aina 3 ya utalii. Mamba kadhaa,Ngamia wawili (kumpanda na kupigia picha Kwa malipo)Nyoka .
Hapo kwenye Nyoka ndio 80% ya zoo lote ,kulikuwa na Nyoka zaidi 20.Chatu, blackmamba,nk
Kumbeba na kupigia picha baadhi ya Nyoka rafiki.
Sema gharama za kuwalisha(wanakula mbuzi na panya) na mabanda ya vioo na wataalamu wawepo.
Restaurant Kwa pembeni.
Mtaji wake sio wa kitoto sema ukisha set kila kitu basi wewe ni kuvuna dollar kama utaitega sehemu sahihi.
 
USHAURI WENU WAKUU
Nataka nikafanye hii project mkoa wa Tabora wilaya X .
Nataka niinvest kimillion changu kimoja.
 
Back
Top Bottom