Uganda imekubali kuwapa raia wa Afghanistani hifadhi ya ukimbizi

Wasijali watakula sosho.
 
Naomba nisaidie kuna kitu kinanitatiza. Taliban wamechukua nchi ila tofauti na vikundi vingine vya ukombozi vinapopigania ukombozi huwa wanaungwa mkono na wananchi ila Taliban ni tofauti nini tatizo?
Mkuu nadhani hawaungwi mkono na Wananch wengi kwasababu ya Sheria tofauti kali za kiislam Sharia (form of sharia Islamic law based on fundamentalism and militant Islamism) ambayo imechanganyikana na mila na Desturi za kabila la Pashtun kwasababu asilimia 98 ya Wataliban ni Pashtun. Wako kivyao.
 
Nashukuru kwa kunielewesha mkuu, ngoja tuone vuta nikuvute yao itakuwaje.
 
Umeona mkutano wa uongozi wa Taliban na waandishi wa habari leo? Wamesema watasamehe kila kitu na hakuna kulipa kisasi. Sana sana naona wakikaa Uganda kwa muda halafu hali ya Afghanistani ikionekana ni nzuri warudishwe.
 
Naomba nisaidie kuna kitu kinanitatiza. Taliban wamechukua nchi ila tofauti na vikundi vingine vya ukombozi vinapopigania ukombozi huwa wanaungwa mkono na wananchi ila Taliban ni tofauti nini tatizo?
Ujue kuwa Taliban ni wa kabila moja, Pashtun, wanafuqtq siasa kali za sheria za Kiislamu. Zamani walisaidiwa na watu wa mataifa mengine kama Al Qaeda. Wanakubatia Uislamu kuendesha nchi. Sharia kali. Wale wenzao pamoja na kuwa pia ni waislamu hawakubatii Sharia. Hivyo Taliban hawapendeki nchini kwao.

Tatizo la suala la sasa ni kuwa wanajeshi wa serikali wenyewe walikuwa hawapendi Wamarekani hivyo wakaona heri zimwi likujualo. Ambalo ni Taleban.
Wamarekani walipooondoka majeshi ya serikali yalikuwa yanasalimu amri bila mapigano yoyote. Ndio maana ikawa rahisi Taliban kuteka nchi.
 
M7 amelipwa pesa nyingi kuwapokea, sio hivi hivi tu
 
Hhhhhh
Hatari sana
 
Na ukifuatilia hili swala,hofu kubwa inakuja kwenye uvunjifu wa haki haswa kwa wanawake na watoto. Maana wananchi wengi wanaijua shughuli ya hawa jamaa, japo jamaa kwa wakati huu ni kama wamekuja kwa mrengo tofauti na wanatafuta kuungwa mkono na jamii ya kimataifa


Sasa kwa wanayosema leo na kuyaahidi kuwa watayasimamia, hamna mwenye uhakika kama ndiyo yatatokea, ndio maana wengi wana hofu.
 
Naamini hapa kuna kitu kilikuwa kinaendelea. Maana jana Biden amefanya press conference na alisema kwamba Marekani ilitoa mafunzo yote ya kijeshi kwa wanajeshi wa jeshi la Afghanistan ikiwepo hadi jeshi la anga. Tafsiri yake ni kuwa serikiali na jeshi walikuwa wana silaha nzito na za kisasa ukilinganisha na Taliban.

Akasema Marekani haiwezi kuendelea kupigana vita ya kufa na kupona ilhali wanajeshi wa nchi husika hawako tayari kupigania nchi yao.

Ila pia inasemekanika kuwa pamekuwa na rushwa sana ndani ya serikali na kupelekea polisi na wanajeshi kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu. Hii imepelekea hawa watu kuona hamna faida ya kundelea kujiweka rehani maisha yao ilhali hamna wanachopata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…