Pole mkuu. Huo muwasho unaweza kuwa dalili ya minyoo aina ya entrobius vermicularis ambayo huwa sehemu ya mwisho inayoitwa anus wakati wa kutaga mayai, na hasa muwasho unakuwa muda wa asubuhi. Vile vile kuna aina nyingine ya mnyoo uitwao trichuris trichiura ambao huwa katika sehemu ya mwisho ya utumbo mpana, ingawa inatokea hasa kwa watoto, huweza kusababisha sehemu fulani ya utumbo kama kinyama kutokeza nje ya anus, kwa kitaalamu huitwa rectal prolapse. Lakini rectal prolapse pia huweza tokea sababu ya constipation kama ulivyosema, udhaifu wa kamba zinazoshikiza utumbo katika ukuta n.k. USHAURI: nenda hospitali wakakupime choo kuangalia mayai ya hiyo minyoo maana inatibika. Na pia wanaweza kukufanyia operation kama ni kwa sababu ya udhaifu wa mishipa inayoshikiza utumbo ukutani. Wakati ukijipanga jitahidi kufuata ushauri wa mchangiaji hapo juu, unaweza hata kujitosa ukatengeneza mchanganyiko wa matunda yanayopatikana sehemu ulipo, sahani moja inatosha kulainisha choo. Zaidi unaweza kuniprime kwenye inbox yangu.