Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Wahi hospital aisee maana kama sio constipation yawezekana kuna shida nyingine kama
Hemorrhoids
Rectal cancer
Colon cancer
Ushauri : kwa sababu unapoteza damu kila haja kubwa nenda hospital ili uondoe wasiwasi wa magonjwa makubwa hapo juu ili ubaki na sababu ndogo utibiwe kwa amani

Pole lakini
 

BAWASILI: TIBA NA TAHADHARI

Maradhi haya yapo ya aina kumi na tano (15). Maradhi haya hushambulia njia ya haja kubwa. Hujitokeza kwa sura tofauti na hali tofauti. Kwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla, aina tatu za maradhi haya ni maarufu sana na yamekuwa yakiwaumiza watu wengi. Katika makala hii nitazitaja aina hizi tatu:

i) Kutoka kinyama katika njia ya haja kubwa
Kuna vinyama vya aina mbili. Cha kwanza ni kirefu hutoka ndani ya njia ya haja kubwa baada ya haja kubwa au mtu anapochutama. Kwa lugha ya kitaalam huitwa skin tab. Cha pili ni kinyama kinachoota pembezoni mwa mzunguko wa njia ya haja kubwa. Kwa kitaalam hiki huitwa external hemorroid . Hizi ni aina mbili za vinyama vinvyoota njia ya haja kubwa.

ii) Mpasuko katika njia ya haja kubwa
Walio wengi hupata maradhi haya. Njia ya haja kubwa hufanya mchaniko pembeni (anal fissure). Mchaniko huu husababisha maumivu makali sana hata mtu hushindwa kukaa. Mara kwa mara hutoa damu hasa mtu anapojisaidi haja kubwa. Maumivu makali hupatina.

iii) Kushuka nyama kubwa njia ya haja kubwa
Baadhi ya walio wengi hushukwa na nyama katika njia ya haja kubwa. Baadhi ya watu wa pwani hasa visiwani huliita nyama hili ni futuru. Hii ni moja ya aina ya maaradhi ya bawasili, mgolo, mjiko.

Kwa kuwa hizi ni aina muhimu zinasosumbua sana hapa ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki naomba tuishie hapo. Mungu akipenda siku nyingine utaangalia maradhi mengine.

4) Matibabu
Kuna matibabu ya aina nyingi kwa njia za kihospitali. Ila ni kwamba maradhi haya yanatibika kwa dawa za MITI SHAMBA. Zipo dawa za kunywa na kujipaka. Dawa ya Mega dose, Tumbo tonic na Hemorrhoid oil ni mjarabu na zinatibu vyema hasa iwapo tatizo utaliwahi mapema

5) Tahadhari
- Unapoona dalili hizo hapo juu MUONE DAKTARI au mtabibu anayeaminika. Usijaribu kujikata au kumpa mtu akukate bila utaalam ni HATARI.
- Usikipasue kinyama kilichoota kwani huo ni mshipa wa damu. Damu itamwagika nyingi sana.

- Jiepushe na yote yaliyotajwa hapo juu yanayosababisha maradhi haya
- Ukiona dalili hizo acha kula nyama za wanyama wa miguu minne (red meat)
- Usile pilipili.
- Ukigundua una tatizo hili usile pia sheli sheli, mboga ya muhogo (kisamvu)
- Iwapo imefikia hatua ya kutoka damu basi usile nafaka za maganda mfano maharage, kunde, chooko, mbaazi, fiwi n.k

6) Ushauri kwa wenye tatizo hili
- pendela kula mboga na matunda
- pendelea kula ndizi mbichi za kupikwa
- kunywa juice mchanganyiko ya ndizi mbichi
- acha yote yanayosababisha maradhi haya
- usimchukie mumeo au mkeo
- mwanamke ukiona mumeo amapoteza hamu ya tendo la ndoa au anamaliza haraka, usichukie, juwa hilo ni tatizo. Tuone tukusaidie, lakini kwanza mfanyie juice ya ndizi mchanganyiko anywe na herbal digestive tea
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa...

Damu fresh isiyo na mabonge inapotoka pamoja na haja kubwa shida ni nini na tiba yake ni nini? Tumbo haliumi na hakuna dalili na maumivu yoyo hata kwenye njia ya haja kubwa.
 
Inaweza kuwa bawasiri au tatizo lingine dogo. Lakini pia inaweza kuwa kansa.
Cha muhimu inabidi uonwe na mtaalam wa njia ya haja kubwa (proctologist ) au surgeon yeyote akufanyie uchunguzi.

The sooner the better...
 
Inaweza kuwa bawasiri au tatizo lingine dogo. Lakini pia inaweza kuwa kansa.
Cha muhimu inabidi uonwe na mtaalam wa njia ya haja kubwa (proctologist ) au surgeon yeyote akufanyie uchunguzi.

The sooner the better...
Kwa Dar hospitali gani ukiachia Muhimbili?
 
Oohhh nitakuwa na Bawasiri nini? Coz ni kama week sasa nahisi maumivu fulani japo kwa mbali wakati wa haja kubwa, Pamoja vi muwasho Fulani ambavyo sio vya kawaida. Nikaanza kuhisi labda ni minyoo. Ila haya maelezo yako yamenitisha
 
na mimi nilikua na tatizo hilo ila nilikutana na mtu akanisaidia..tuwasilane nikudokeze 0754586624
 
Mkuu nimeelewa sana ushaur wako, i thnk nianze kutendea kaz kwa upande wa kitunguu saumu kwa kwel maana hili tatizo linanitesa sana almost three yrz nw
 
Mkuu nimeelewa sana ushaur wako, i thnk nianze kutendea kaz kwa upande wa kitunguu saumu kwa kwel maana hili tatizo linanitesa sana almost three yrz nw
Jaribu hii nilielekezwa na mtu ambaye alitumia na akapona kabisa.Tumia Olive oil iliyombewa,huyu jamaa yangu alinunua pale kwenye kanisa la Mch.Mwingira Lugalo akawa anapaka kutwa mara mibili ndani ya wiki moja kikawa kimekwisha kabisa.
 
Jaribu hii nilielekezwa na mtu ambaye alitumia na akapona kabisa.Tumia Olive oil iliyombewa,huyu jamaa yangu alinunua pale kwenye kanisa la Mch.Mwingira Lugalo akawa anapaka kutwa mara mibili ndani ya wiki moja kikawa kimekwisha kabisa.
Duu niko mbal na dar tatizo, bt naweza pata kwenye maduka ya aina gan..n kwa kiswahil ndo mafuta ya zaituni au?
 
Duu niko mbal na dar tatizo, bt naweza pata kwenye maduka ya aina gan..n kwa kiswahil ndo mafuta ya zaituni au?
Uko sahihi mkuu ni mafuta ya Zaituni,kuna baadhi ya maduka ya dawa yanauza.
 
FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba.

JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI?

Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.
Tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30-50.
AINA ZA BAWASIRI
Kuna Aina mbili za bawasiri

(A) BAWASIRI YA NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa wana tatizo hili.
Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa .

Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika.

(2)DARAJA LA PILI ~Hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia.

(3)DARAJA LA TATU :Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenyewe.

(4)DARAJA LA NNE :Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

(B)BAWASIRI YA NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu hilo.Pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS.
CHANZO CHA TATIZO
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni

KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
KUHARISHA KWA MUDA MREFU
TATIZO LA KUTOPATA CHOO
MATATIZO YA UMRI
KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
UZITO KUPITA KIASI
MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU

DALILI ZA BAWASIRI

1. Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
2. Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
3. Kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
4. Kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
5. Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
Matibabu ya bawasiri hutegemea na aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia.

Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia

Kula mbogamboga za majani, matunda, na nafaka ziszokobolewa.

Kunywa maji mengi angalau grass 6/12 kwa siku.

Epuka kukaa chooni kwa muda mrefu.

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI

Kupata upungufu wa damu (anemia)

Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo

Hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
Kuathirika kisaikolojia
Kukosa morali ya kufanya kazi kutokana na maumivu makali
 
Ndg, Asante kwa Taarifa Hii
Mimi kama Mtanzania mara nipatapo Mtu mwenye BAWASIRI Mwa- Africa Nitatafuta Thread Hii kwa Ushauri na Matibabu.
 
Uwo ugonjwa ni mwepesi sana dozi moja tu ya hospital unatibika....ila sijui kwanini watu wanaukuza sana
 
dawa gani inayoweza kutibu ugonjwa wa aina hiyo hapo ulioolelezea mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…