Hii nazungumzia External Hemorrhoids au Bawasili inayotokea upande wa nnje, nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakipoteza Garama kubwa kuhangaika nayo kwa kuifanyia upasuaji na Baadhi wamekuwa wakisema baada ya upasuaji ugonjwa huu huwa unajirudia tena
Pia mkumbuke kuwa swala la (Surgey) upasuaji huwa lina matokeo mawili either liende vizuri au likatae na kuleta madhara zaidi au kuzalisha ugonjwa mengine kama cancer n.k na ndio maana kabla ya kufanyiwa upasuaji wowote ni lazima usign kuwa umekubali.
*Nini cha kufanya unapopatwa na Ugonjwa huu ?
Wengi wanaopata ugonjwa huu huwa ni waoga na wengi hudhani kuwa njia ya upasuaji ndio njia pekee ya kulimaliza tatizo hili kwa haraka lakini sio kweli, kama hautadhibiti mambo ambayo yalikupelekea kuupata ugonjwa huu basi jua huu ugonjwa hata ukifanyiwa upasuaji utajirudis tu.
So unapota huu ugonjwa kitu cha kwanza unatakiwa uchunguze ni kitu gani kilichokupelekea uupate kama kupata choo kigumu, kutumia baadhi ya sabuni za kuogea ambazo sio nzuri, kutumia vinywaji vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa, chai na Soda, kutokunywa maji kwa wingi, ujauzito kwa wanawake, kunyanyua vitu vizito n. K
Hivyo ugonjwa huu unauwezo wakuondoka wenyewe bila kufanyiwa upasuaji kwa kubadili mfumo wa vyakula ambao ndio hupelekea mara nyingi watu kuupata ugonjwa huu, so unapoupata unatakiwa kufanya mambo haya mara moja na utaondoka wenyewe bila ya kufanyiwa upasuaji
~Hakikisha unakunywa maji kwa wingi ili kupata choo laini
~Epuka ulaji wa vyakula vya ngano kama mikate, chapati, maandazi n. K
~Epuka kusimama kwa mda mrefu
~Usitumie vinywaji kama Kahawa, Soda, maziwa fresh ambayo kitaalam yanasemekana kuwa hupelekea kuzalisha gesi tumboni ambayo hupelekea kuzidisha maumivu na vimbe
~Usitumie pilipili, Chumvi nyingi kwenye chakula, usile vyakula vilivyokobolewa kama ugali wa sembe, ngano, mchele,pia usitumie kwa wingi nyama nyekundu machungwa pia usitumie
~Kunywa maji kwa wingi pia tumia vyakula visivyokobolewa kama ugali wa dona, kula matunda kwa wingi hasa mapapai na ovacado (parachichi)
~Kula mboga za majani kwa wingi hasa spinach na mchina, ni mboga ambazo kitaalam zina fiber nyingi ambayo itapelekea kuondoa hizo vimbe automatically.
~Pia angalia sabuni unazotumia kuogea baadhi ya sabuni hupelekea hilo tatizo
Sent using Jamii Forums mobile app