Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Mkuu mimi niko mwanza, nimetoka hospital sasa hivi nimeambiwa ni bawasiri, kuna dawa Dr kanishauri nikazitafute zitanisaidia zaidi kuliko hizo za bima, kuna gel moja inauzwa 18k nimeshaipata na vidonge vinauzwa 38k ndio nahangaika kuvitafuta hapa bado sijavipata....ila mwanzoni nilidhani ni jipu na wife aliniwekea kitunguu saumu eti liive, hapa nilipo nikishika nalisikia kama ni laini laini mno, natamani ata litobolewe niweze kukaa au kutembea vizuri.
 
Sasa umeenda hospitali tayari na umepewa tiba/ushauri wa kitaalamu huku unatafuta ushauri gani tena kama sio masihara na utani...!!!
Ushauri nimeomba kabla ya kwenda, pili ata kama nimeshaenda hospital hiyo hainizuii kutafuta ushauri zaidi kwasababu madaktari wanazidiana uwezo na uzoefu,tatu kama huna cha kuchangia ni vyema ukajikalia kimya au ukaenda kule chit chat.
 
Nyumba unayokaa au ofisini unatumia choo cha aina gani? Naamanisha cha kukaa au cha kuchuchumaa?
 
Wife alikueekea kitunguu maeneo hayo?
 
wewe acha kukaa kwenye vyoo vya kukaa muda mrefu, unaminya mishipa ya damu, unapojisahidia!
 
pia dawa za kuweka kunako zipo nyingi tuu! chanzo ni vyoo vya kukaa maranyingi!
 
Pole sana bro.
 
Sasa mkuu kijipu kikutoke makalioni kwako sisi tutajuaje? kwani upo mkoa gani tuone ili nikukague na niweze kukushauri.
 
pole sana ndugu. kuna mdau hapo juu ameshauri ule vyakula vya nyuzi nyuzi ni kweli na cha kuongezea usisahau kunywa maji ya kutosha kila siku.
 
Hilo ni jipu linalosababishwa na bacteria. Na hii husababishwa sana na uchafu hasa kutokusafisha vizuri maeneo hayo au kuvaa chupi au boxer chafu kwa muda mrefu.

Onana na docta yeyote akuandikie dawa au tumia anti bayotic dozi.
 
hiyo ni bawasiri mkuu

madokta wanasema hakuna sababu ya moja kwa moja kupelekea ugonjwa huo, ila huchangiwa na..
-kujikamua wakati wa haja kubwa
-kuchuchuma/kukaa kwa muda mrefu
-kupata choo kigumu
-kujihusisha mapenzi kinyume na maumbile......sababu nyingine nimesahau mkuu

tumia hizo dawa kama hazitasaidia nitafute

mimi sio dokta at your own risk
 
Hiyo ni fistula. Wahi hospitali ukamuone Daktari akupasue...
 
Kiongoz,inaelekea mboga za majan hutumii kabsa na matunda.

Fululiza mboga za majan kwa wing na papai...na hzo dawa ulizopewa hospital itapona.

Usipozingatia haya ukiendelea pata huu ugonjwa mara kwa mara,utapata kansa
 
Hakika ni bawasiri inauma na zaidi inafadhaisha nimewahi kutokewa mara mbili na ikapotea yenyewe ila ilipokuja kutoka Mara ya tatu hali haikuwa nzuri nilitumia alovera kwa kupaka ute wake kuzunguka uvimbe pia kunywa juisi yake kiasi cha nusu Lita asubuhi kabla ya chochote na jioni wakati wa kulala kuhusu maumivu nilikuwa nikitumia flamar mix
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…