Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

kuna ndugu yangu alikua anasumbuliwa na huo ugonjwa ukimwangalia alivyokua anateseka utamuonea huruma
 
Pole na hongera kwa kupona na asante kwa taarifa tosherezi, dawa za kienyeji nazo zinaubaguzi sana, wewe inaweza kukuponya kabisa na mwingine ikagoma,
 
Wakuu kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na hizi vimbe za sehemu ya haja kubwa ambazo zimekuwa zikiniletea maumivu makali kwa kipindi cha miaka mitatu.

Nilijaribu dawa mbali mbali zikiwemo anusol ya cream na suppositories lakini hazikuwahi kunisaidia hadi ikafikia kipindi nikashauriwa kufanyiwa upasuaji lakini nilikataa kutokana na wengi wanaofanyiwa upasuaji huu ugonjwa umekuwa ukiwarudia baada ya miaka kadhaa

Nilijaribu na baadhi ya dawa za mitishamba lakini bado hazikufua dafu bali vimbe ziliendelea kunitesa hadi ikafika kipindi nikakata tamaa

Lakini mwezi uliopita nililetewa na shangazi yangu dawa iliyo kwenye kichupa kidogo iliyo katika mfano wa maji maji

Nilipouliza nikaambiwa ni maji ya mgomba yalioandaliwa kwa kuchanganywa na mafuta ya mnyonyo kiasi.

Wakuu nimetumia ndani ya wiki vimbe zote zimepotea kabisaa.

Kama kwenu kuna migomba usikate aisee huwezi jua kesho yako

Nawasilisha
Tueleze vizuri huu mgomba una sehem nyingi kuna magome na majani yake...kipi unachosema wewe majani au majimaji ya mgome ya mgomba?
 
Mnyonyo ni kitu gani?

image.jpg
image.jpg

Mbugu zake zikikomaa
image.jpg
 
Hii issue ni serious case.
Kuna ndugu yangu hawezi kukaa kwa zaidi ya dakika tatu,miezi kadhaa sasa. Analalamika kuna uvimbe mkubwa sana so akikaa unapasuka na kutoa damu. Hizo enusol zote kamaliza, aloevera nayo katumia sana.

Naomba mtoa mada atoe ufafanuzi vizuri jinsi ya kutengeneza hii dawa.
Mimi mwenyewe naona dalili kama kauvimbe kanaanza anza hivi.
 
aende hospital....wajue..ni.nin.kwanza...haya maswala ya kutulia na uvimbe mda mrefu sio dili.....ushauri...tu... Coz wagonjwa weng wanakuja hospital baada ya miti shamba kugoma
 
Wakuu kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na hizi vimbe za sehemu ya haja kubwa ambazo zimekuwa zikiniletea maumivu makali kwa kipindi cha miaka mitatu.

Nilijaribu dawa mbali mbali zikiwemo anusol ya cream na suppositories lakini hazikuwahi kunisaidia hadi ikafikia kipindi nikashauriwa kufanyiwa upasuaji lakini nilikataa kutokana na wengi wanaofanyiwa upasuaji huu ugonjwa umekuwa ukiwarudia baada ya miaka kadhaa

Nilijaribu na baadhi ya dawa za mitishamba lakini bado hazikufua dafu bali vimbe ziliendelea kunitesa hadi ikafika kipindi nikakata tamaa

Lakini mwezi uliopita nililetewa na shangazi yangu dawa iliyo kwenye kichupa kidogo iliyo katika mfano wa maji maji

Nilipouliza nikaambiwa ni maji ya mgomba yalioandaliwa kwa kuchanganywa na mafuta ya mnyonyo kiasi.

Wakuu nimetumia ndani ya wiki vimbe zote zimepotea kabisaa.

Kama kwenu kuna migomba usikate aisee huwezi jua kesho yako

Nawasilisha
Kweli?
 
Mtoa mada tunaomba utufahamishe namna ya kukupata.. Kuna watu wengi wana tatizo hili tuwasaidie please
 
Mbali ya yote hayo unapopata mlo hakikisha, sahani nusu hadi robo tatu ijaze mboga mboga na matunda, wanga iwe robo ama nusu hiyo inasaidia sana maana choo kinakuwa kilaiini
 
Hii issue ni serious case.
Kuna ndugu yangu hawezi kukaa kwa zaidi ya dakika tatu,miezi kadhaa sasa. Analalamika kuna uvimbe mkubwa sana so akikaa unapasuka na kutoa damu. Hizo enusol zote kamaliza, aloevera nayo katumia sana.

Naomba mtoa mada atoe ufafanuzi vizuri jinsi ya kutengeneza hii dawa.
Mimi mwenyewe naona dalili kama kauvimbe kanaanza anza hivi.
Kuna jamaa alienda kwenye interview likampasukia huko huko suti yote nyuma damu kama hedhi.

Hii dawa inabidi ifanyiwe majaribio rasmi ijulikane vizuri.
 
Polleni sana inabidi kufanya mawasiriano na mleta mada ili awape taarifa vizur
 
Back
Top Bottom