Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

ni kwa sababu unakunywa damu za watu, acha u-vampire (nakutania,lol)
hemorrhoids (hivyo vinyama, kwa kiswahili vinaitwa bawaziri kama sikosei) vinatokana na presha inayojijenga kwenye mishipa ya damu kwenye utumbo mnene kwa sababu mbalimbali. mojawapo ikiwa kuwa na choo kigumu. kula mapapai kwa wingi na mboga za majani, lakini ni muhimu sana uonane na daktari mapema. ni tatizo linalotibika, na huenda ukahitaji upasuaji mdogo. the earlier,the better
pole sana

mkuu nakushauri haraka uwaone wataalamu kwa ushauri zaidi

Hvyo vinyama vinaitwa bawasiri, km vimekua sana utahtaji upasuaji kwanh kila uendapo haja huchubuka na kutoa damu kidogo au nyingi. Kula matunda na mboga za majani pia unywe maji mengi. Pole sana vamp!

kula sana mapapai tena yalioiva mpaka kukalibia kuoza ndio mazuri kila baada ya kila mlo..

p.o.l.e sana mkuu cha kukusaidia una tatizo la kuganda kwa choo,cha msingi kunywa maji mengi asubuhi then after 4hrs kunywa glass mbili za juice ya ukwaju,tatizo lako litaisha ila kwa ushauri zaidi mtafute dr.ndodi atakusaidia sana...pole kwa matatizo.

jaman nimekua na this problem muda sana natoa hiki choo,pia kinavo toka nakua naumia sana..mbaya zaidi nime otwa na vinyama katika njia ya haja na vinazidi kuongezeka..hivi vitu vinantesa sana napata shida sana nikiwa toilet...

ya ng'ombe ndo nzuri,lol!

sasa mkuu akitaka kufanyiwa opereshen il hvyo vinyama vikatwe atakaa style gan ya mbuz?!! Ha ha ha. (Utan). Ugua pole vampire.

j

na isingekua mfungo, wallah ningeviita mawaziri,lol! asante kwa sahihisho
Hvyo vinyama vinaitwa bawasiri, km vimekua sana utahtaji upasuaji kwanh kila uendapo haja huchubuka na kutoa damu kidogo au nyingi. Kula matunda na mboga za majani pia unywe maji mengi. Pole sana vamp!

Ni dalili kuwa unataka kuwa mbuzi
Nilikuwa na tatizo kama hilo liliisha kwa kunywa maji mengi, juisi ya ukwaju na mapapai

pole sna vampire..............matunda matunda,moga za majani na maji meeengi ikiwezekana per day maliza hata pipa

jaman nimekua na this problem muda sana natoa hiki choo,pia kinavo toka nakua naumia sana..mbaya zaidi nime otwa na vinyama katika njia ya haja na vinazidi kuongezeka..hivi vitu vinantesa sana napata shida sana nikiwa toilet...

pole mkuu niPM tafadhari

Habari wana jf
nina tatizo ambalo linanitokeaga na kupotea
zamani kidogo kama miaka 8 iliyopita ndo nililigundua tatizo hili
huwa kuna kipindi inafika haja kubwa inakuwa nguumu sana
nikienda kujisaidia napata maumivu na haja hiyo haitoki kirahisi
labda niinge chooni na nafuta mgando nijikaze huku napaka
natoka nasubiria najikaza mpaka haja inatoka ikiambatana na damu
kama vijiko vitatu vya chakula,
inafika muda hiyo hali inapotea hata mwaka mzima inarudi tena

hapa niandikapo nina kama mwezi mmoja hali hii inanisumbua kiasi kwamba
inaniathiri kisaikolojia
sababu nikipatwa na haja kubwa naanza kuyafikiria mateso hayo
nimejaribu mapapai yananisaidia kidogo saana nisaidieni nifanye nini?

Tatizo lako ni Ukosefu wa kupata haja kubwa kwa urahisi kwa lugha ya kizungu ugonjwa unaitwa (constipation) Na hiyo ndio imesababisha wewe kupatwa na ugonjwa unaoitwa Bawasiri au kwa lugha ya Kiingereza unaitwa
(Hemorrhoids)
Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri:
i. Nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
ii. Ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
• Tatizo sugu la kuharisha
• Kupata kinyesi kigumu
• Ujauzito
• Uzito kupita kiasi (obesity)
• Ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
• Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
• Umri mkubwa
Dalili za bawasiri;
• Damu kuchanganyika na kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
• Maumivu au usumbufu
• Kinyesi kuvuja
• Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
• Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
• Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri:
• Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
• Strangulated hemorrhoids
understandinghemorrhoidsbasics-hemorrhoids.jpg

Vipimo na uchunguzi:
i. Digital rectal examination
ii. Proctoscope
iii. Sigmoidoscope
Matibabu :
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
i. Rubber band ligation- Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
ii. Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
iii. Coagulation (infrared, laser and bipolar)
iv. Upasuaji;
-Hemorrhoidectomy
-Stapled hemorrhoidopexy
Jinsi ya kuzuia Bawasiri:
• High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
• Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
• Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.

Chanzo :Bawasiri (Hemorrhoids) – TanzMED(old) - Afya Kwa Wote

Nakushauri ufanye hivi Soma hapa chini

[TABLE="class: tborder, width: 100%, align: center"]
[TR]
[TD="class: alt1, bgcolor: [HASHTAG]#FFFFFF[/HASHTAG]"]

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’ muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

inatibikaje hivi wazee mana nimeskia ipo external na internal, how is it going?

kama ni very early stage unaweza kupata dawa. otherwise unaweza kuhitaji upasuaji mdogo. ni muhimu kuonana na dr ili uchunguzwe na kupata tiba sahihi.

Sio mambo hii ni ugonjwa wa kawaida kabisa ila unatibika na kupona kabisa...kama ni mwanzo watakupa dawa ya kunywa na kuingiza pale basi lakini kama umekomaa mpk wakate kile kieneo ina maumivu sana but after few days inakua safi na unaendelea na maisha,,,

inatibikaje hivi wazee mana nimeskia ipo external na internal, how is it going?
Inatibika kwa opareshein ya upasuaji nenda kamuone Daktari atakusaidia.

Back
Top Bottom