Tatizo lako linatokana na kutokunywa maji ya kutosha,hivyo imesababisha kuwa unapata kinyesi kigumu ambacho hulazimisha kupita katk njia ya haja kubwa na hivyo kusababisha michubuko/aina ya nyama kutoka kwa nje ikiambatana na damu.sasa yale maumivu ya sehemu ya haja kubwa na ile nyama ambayo mara nyingi huwa inapata vidonda ndio huwasha kila unapoenda haja kubwa na unaponawa maji.
usipoangalia unaweza kunawa maji mengi kwa sababu kila ukipitisha mkono unakuwa kama unakuna ile sehemu hivyo ukiacha ndio chanzo cha muwasho ambacho husababisha hata kutembea/kukaa kuwe kwa aina fulani.
ushauri:
1kunywa maji mengi wastani wa glass nane kwa siku.
2.Pendelea kula mataunda kwa wingi na hasa papai.
3.Epuka kula vyakula vigumu.
4.Kwa kipindi hiki unachowashwa usipende kuvaa nguo nyingi ili kuruhusu hewa kupita na kuponyesha vidonda.
Nahisi ntakuwa nimekusaidia kwa kiasi fulani