Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Habari za majukumu members,, samahani nasumbuliwa na ugonjwa wa bawasili(kuota vinyama sehemu ya haja kubwa) karibia mwaka wa pili sasa, mwenye kuweza kunisaidia dawa either ya hospitali au ya kienyeji ili niweze kutumia maana kinanisumbua sana wakati wa kukaa na ninapoenda haja kubwa,, Tafadhali naombeni msaada wenu!

Nitafute utapona kuna baadhi ya members wa humu wamepona nimewapatia dawa na ipo siku wataleta ushuhuda wao ,bawasir ni ugonjwa mbaya Sana na unaua
 
Kuna jamaa amefanyiwa upasuaji juzi tu and he is good now.Acha kuogopa kwn mficha maradhi kifo humuumbua.Nenda hospital kaka

Tatizo ukifanyiwa upasuaji vinyama vinaota tena ,sisi tuko na tiba lishe inayoviondoa kabisa na tatzo halirudi tena
 
Habari wapendwa. Nakosa hata nguvu za kuandika huu uzi kwani nateswa sana na huu ugonjwa unaitwa Bawasiri ambao unasababisha kuota kinyama kuzunguka mkunduni.

Nimetumia dawa za hospitali pamoja na kienyeji lakini inatulia kwa miez 3 mwisho inarudI taratibu. Pamoja na hilo nina shida ya tumbo kujaa gesi sasa sielewi hili nalo linasababishwa na hii Bawasiri au laaah. Pamoja na hilo hata performance yangu kimapenzi imeshuka sijisikii tena mhemuko wa kufanya mapenzi, hili nalo nahisi linaweza likawa limechangiwa na tatizo hili.

Ombi langu kwenu mwenye uwezo wa kunisaidia nikapata dawa ya asili ya gonjwa hili la aibu sana naomba anisaidie, nateseka kwel.

Moja ya athari za bawasiri(piles) ni kushindwa kumudu tendo la ndoa,watu wengine ukiwambia tiba ya bawasiri wengine wanaona ni gharama lakin kimbuka bila afya njema huwezi kufanya kaz yoyote,pia huu ugonjwa kadiri unavyoishi nao ipo siku utashindwa kukaa kabisa kutokana na maumivu saa nyingine kinyesi kinaweza kutoka bila utaratibu na ukiwa mbele za watu kitu ambacho ni aibu,ambaye yuko sereous anaitaji tiba ya uhakika dhidi ya maradhi haya anitafute kwa njia ya whats app ,akishatumia dawa yetu yeye atakuwa ushuhuda kwa kuwapa wengine nambar yangu ambayo ni 0714267658 tusifanye masihara na ugonjwa na kadiri mtu anavyochelewa kupata tiba bawasir inaweza kugeuka na kuwa kansa ,chukua hatua mapema,tuna ofsi dar,Dodoma,mwanza,na mbeya,unapewa utaratibu unafanya malipo kwa njia ya bank ,baada ya hapo unakuja na payslip ofsin unapewa ushauri na kuchukua dawa na ndan ya mda mfupi tatzo lako linaondoka kabisa na halirudi tena,hatufanyi upasuaji
 
Ili usipate bawasiri unatakiwa ule vyakula vyenye fibers nyingi,matunda na mbogamboga na uwe unakunywa maji yakutosha,mazoezi na epuka kukaa muda mrefu sehem moja,,,!
 
Ili usipate bawasiri unatakiwa ule vyakula vyenye fibers nyingi,matunda na mbogamboga na uwe unakunywa maji yakutosha,mazoezi na epuka kukaa muda mrefu sehem moja,,,!

Ukila mlo kamili na maji yakutosha Itakusaidia upate choo kilain nasio kukaa muda mrefu kujikamua mpaka mishipa inakuletea madhara.
 
Moja ya athari za bawasiri(piles) ni kushindwa kumudu tendo la ndoa,watu wengine ukiwambia tiba ya bawasiri wengine wanaona ni gharama lakin kimbuka bila afya njema huwezi kufanya kaz yoyote,pia huu ugonjwa kadiri unavyoishi nao ipo siku utashindwa kukaa kabisa kutokana na maumivu saa nyingine kinyesi kinaweza kutoka bila utaratibu na ukiwa mbele za watu kitu ambacho ni aibu,ambaye yuko sereous anaitaji tiba ya uhakika dhidi ya maradhi haya anitafute kwa njia ya whats app ,akishatumia dawa yetu yeye atakuwa ushuhuda kwa kuwapa wengine nambar yangu ambayo ni 0714267658 tusifanye masihara na ugonjwa na kadiri mtu anavyochelewa kupata tiba bawasir inaweza kugeuka na kuwa kansa ,chukua hatua mapema,tuna ofsi dar,Dodoma,mwanza,na mbeya,unapewa utaratibu unafanya malipo kwa njia ya bank ,baada ya hapo unakuja na payslip ofsin unapewa ushauri na kuchukua dawa na ndan ya mda mfupi tatzo lako linaondoka kabisa na halirudi tena,hatufanyi upasuaji
Mkuu are you serious?

Na gharama zenu ni ngapi? Na je kwa yule ambaye ugonjwa ume develop kwa kiasi fulani anapona?Aisee kuna ndugu yangu anateseka sn na anaficha
 

Naomba msaada wa hivi vinyama vilivyoniota pembezoni mwa shimo la haja kubwa vinaitwa piles kwa kimombo, kiswahili sijui. Hivi vidude huwa vinauma na kuacha, naweza kukaa miezi 8 hadi mwaka sivisikii ila vikianza kuuma nashindwa kukaa au hata kutembea. Naomba msaada wa dakatari yoyote anayevijua aniambia chanzo na matibabu yake. asanteni

BAADHI YA WADAU WANAOELEZA KUATHIRIKA NA TATIZO HILI


UNDANI WA TATIZO LA BAWASILI

Bawasiri yaweza kuwa moja ya topic ngumu sana kuzungumziwa kiuwazi na watu, hii ni kutokana na wagonjwa wengi kuona aibu pengine ni kwasababu tatizo husika hutokea mahala pa haja kubwa. Wengine huona aibu hata kueleza tatzo hili kwa Dactari ama muhudum wa afya, bawasili ni tatizo kuwa linawatokea wanaume kwa wanawake. Naweza kusema uwepo wa tatizo hili si ajabu ukianagalia wengi wetu wanakula vyakula zaidi vilivyosindikwa, hawafanyi mazoezi na wana msongo wa mawazo uliokithiri.

Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe. Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS na kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.

Tatizo la bawasili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50% ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 40 mpaka 50.

Kuna Aina kuu mbili za bawasiri

(A) Bawasili ya ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili,.Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA
Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI
Hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia

(3)DARAJA LA TATU
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe

(4)DARAJA LA NNE
Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

(B)Bawasili ya nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

Bawasili kwa kiasi kikubwa huletekezwa na kuongezeka kwa mganadamizi ama presha mara nyingi ni pale unapojikaza ili kutoa haja kubwa. Hivo bawasili huwatokea zaidi watu wenye matatizo ya mfumo wa umen’gemnyaji mfano unapata choo kigumu, tumbo kujaa gesi, kukosa choo kwa siku kadhaa.

Wamama wenye ujauzito pia huwa kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mtoto aliye tumboni kugandamiza tumbo la chakula na hivo kuathiri utoaji wa haja kubwa, kwa bahati nzuri bawasili inayosababishwa na ujauzito huanza kuisha pale tu mama anapojifungua. Watu wenye kitambi na uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasili kutokana na mwili kushindwa kutengeneza nishati ya kutosha kusukuma uchafu kwenye utumbo.

Wakati mwingine inatokea unaweza kuwa na bawasili lakini usipate dalili na baada ya mfupi ugonjwa huweza kupotea wenyewe. Dalili moja kubwa ambayo wagonjwa wetu wengi huipata kwa wenye bawasili ya ndani ni kuvuja kwa damu inatyoweza kuonekana kwenye toilet paper ama kinyesi, unapoona dalili kama hizi hakikisha unachukua hatua za haraka maana tayari umepata bawasiri.

Kama una bawasiri ya nje basi unaweza kupata viashiria kama uwepo wa nundu nyekundu iliyojaa damu pembeni mwa mahala pa haja kubwa, kitaalamu huitwa thrombosed hemorrhids na huambatana na maumivu makali sana wakati wa kutoa haja, kama utoaji wako wa haja ni wa kujikamua na kwenda haraka haraka, na kujisafisha kupita kiasi basi unaweza kuongeza tatizo, ianashauriwa kutotumia nguvu kubwa kujisaidia.

Si kila Unapoona kuna damu inavuja ni Bawasili
Unapoona kuna damu inavuja mahala pa haja kubwa ama unapotoa haja, basi nashauri nenda haraka hospital kuonana na Dactari na kufanya vipimo, hasa kama tatizo ni limekutokea kwa mara ya kwanza. Kuvuja kwa damu kwenye sehemu ya haja kubwa inaweza kuwa ni dalili za Saratani ya utumbo mpana . kitu kimoja cha kuvutia sana ni kwamba uwepo wa Vitamn D ya kutosha mwili hupunguza hatari ya kupata Bawasili kwa karibu 80%, kwahiyo kama tatizo linajirudia mara kwa mara basi fanya checkup kujua kama una Vitamn D ya kutosha.pia unaweza kutembelea stoo yetu ya virutubisho kwa kubonyeza hapa kupata kirutubisho chenye Vitamin zote.
  1. Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
  2. Kuharisha kwa muda mrefu
  3. Kukaa kitako kwa muda mrefu
  4. Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu
Dalili zingine za zitakazokusaidia kugundua kama una tatizo la bawasili ni;
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
  • Kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
  • Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
HATUA NNE ZA KUZUIA KUTOKEA KWA BAWASIRI
Hapo juu tumeona kwamba chanzo kikubwa cha tatizo hili ni matatizo ya mfumo wa umen’genyaji kama kukosa choo kwa mda mrefu, kupata choo kigumu, kuharisha mara kwa mara na tumbo kujaa gesi, hivo kwa kuzuia matatizo haya basi utakuwa umejikinga na bawasili. Hivo hakikisha unafanya yafuatayo;
  1. Kula mbogamboga za majani, na nafaka zisizokobolewa, matumizi ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa wingi husaidia kuongeza ukubwa wa kinyesi na hivo kurahisha utolewaji wake, kama mwanzo hukutumia vyakula vya nyuzinyuzi basi anza kuongeza taratibu kwenye mlo wako mpaka pale tumbo litakapozoea.
  2. Tumia machungwa kwa wingi, machungwa yana kiungo kinachoitwa flavonoids, kiungo hiki ni muhimu katika ustawi wa mishipa ya damu ya Veins, mishipa hii ndio huathirika na kuletekeza bawasiri.
  3. Kunywa maji ya kutosha kila siku, tumia kiu na rangi ya mkojo kama kiashiria cha kiasi gani cha maji unatakiwa kunywa, kama mkojo ni wa rangi ya njano inayokolea basi ni kiashiria kwamba mwili hauna maji ya kutosha na unatakiwa kunywa. Nyuzinyuzi na maji ya kutosha husaidia kulainisha choo chako na hivo kurahisisha utolewaji wake bila kujikamua.
  4. Hakikisha unapata virutubisho kwa ajili ya kusawazisha Bacteria wazuri ndani ya mfumo wa chakula, vyenye ubora wa hali ya juu usimeze kila kirutubisho.
ZINGATIA HAYA UNAPOKUWA CHOONI
1. Ruhusu mwili wako kufanya kazi kwa jinsi ulivoumbiwa, yaani pale unapojiskia haja basi hakikisha unaenda mara moja kujisaidia pasipo kujizuia, kujichelewesha kunaweza kusababisha Constipation.

2. Usikae mda mrefu chooni ukijisaidia, hii inaongeza mgandamizo katika eneo la chini kwenye mishipa ya damu na hivo kukuongeza hatari ya kupata bawasili. Tumia dakika 3 mpaka 5, ama subiri mpaka unapokuwa na haja, kama unajiskia kutoa uchafu lakni ukienda chooni kinyesi hakitoki basi tembea tembea ama fanya zoezi la Squats.

3. Usitumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tumia misuli ya tumbo kutoa haja taratibu.

4. Unapotoa haja basi hakikisha unachuchumaa kama miili yetu ilivoumbwa, watu wanaotumia njia hii mara chache sana huugua bawasili, lakini matumizi ya vyoo vya kukaa ni moja ya kihatarishi cha kupata bawasili kutokana na kwamba inahitajika utumie nguvu kubwa sana kujikamua.

TUMIA NJIA NZURI NA SALAMA KUJISAFISHA
  • Usitumie nguvu kubwa kujifuta kwa toilet paper ama wipes zingine baada ya kwenda haja, hii hufanya ngozi kulanika na kuvimba
  • Kama inawezekana jisafishe taratibu kwa kutumia maji bila sabuni, na kujifuta kwa taulo laini.
  • Kwa maeneo ambapo huwezi kutumia maji mfano kwenye vyoo vya umma, basi tumia wipes laini zenye unyevunyevu kwa umakini.
KUPUNGUZA ATHARI YA BAWASILI KAMA TAYARI UMEUGUA
Ushauri huu siyo kwamba hutakiwi kufika hospitali kupata huduma, ama kuonana na dactari wako, ni ushauri ambao tunawapa wagonjwa wetu wote kabla hawajafika Ofsini kwetu kupata huduma ya Dawa na Virutubisho.
  • Jaribu Sitz Bath, hii inajumuisha mgonjwa wa bawasili kuvua nguo na kukaa kwenye maji yenye uvuguvungu kwenye beseni kwa mda wa dak 15 mpaka 30, unaweza kukaa mara nyingi uwezavyo, hakiksha maji siyo ya moto ni ya vuguvugu, itakusaidia kupunguza maumivu.
  • Chukua kipande cha barafu kilichoganda na kukiweka mahala pa haja kubwa kwa dak 10 mpaka 15 kwa siku.
  • Chukua mmea wa Aloe-vera ukate kisha loweka kwenye maji, baada ya hapo chukua kitambaa laini loweka kwenye maji yenye aloe vera na upakae taratibu mahali pa haja kubwa.
MUHIMU: Ushauri huu ni kwa ajili ya kupata nafuu ya haraka, hivo hakikisha unafika hospitali kupata matibabu

Madhara Ya Tatizo La Bawasiri
1. Kupata upungufu wa damu (anemia)
2. Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo
3. Upungufu wa nguvu za kiumekwa wanaume na Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
4. Kuathirika kisaikolojia
5. Kukosa moral ya kufanya Kazi na maumivu makali

Matibabu ya bawasiri yamegawanyika katika sehemu mbili na hutegemea na aina ya bawasiri
1. Tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama ambayo hutoelewa hospital na kuendelea na lishe ya chakula. Hata hivyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia, ndiomana katika kituo chetu tunashauri kutibu chanzo cha tatizo.

2. Tiba ya tatizo hili kwa kutumia vidonge vilivyotengenezwa kwa mimea.

Credit: LIndaafya.com
Bawasiri ni moja ya tatizo linalosumbua sana na sababu kubwa n kutokana na mfumo wetu wa maisha kuanzia chakula tunachotumia hadi kazi tunazofanya .
Zijue njia tano bora ya kuzuia hili tatzo 5 ways to prevent hemorrhoids
 
Mkuu are you serious?

Na gharama zenu ni ngapi? Na je kwa yule ambaye ugonjwa ume develop kwa kiasi fulani anapona?Aisee kuna ndugu yangu anateseka sn na anaficha
Jamaa alinambia gharama ya dawa yake ni 250,000/=. Sijui alitaka kunipiga!
 
Akontroo uzito.

Anywe maji mengi mara kwa mara

Ale matunda kama maembe, papai..

Atumie Ndizi za kupikwa

Aepuke Nafaka kama Ulezi, mtama

Atumie mboga mboga, Nyama

Asikae na haja kubwa muda mrefu.


Bawasari izo hata kama ukiziondoa kwa upasuaji, ukishindwa kubadili maisha yako hususan Ulaji, Zinarudi kama kawaida .

Hazina dawa za kuponyesha tatizo.

Kubwa ni kubadili mfumo wa maisha ,zitapotea na hazirudi, ila akirudi kulekule aiseee nazo zinarudi.


Kwasasa atumie dawa za maumivu pia aendelee kutumia maji ya uvuguuvugu kujikanda njia ya haja kubwa .

#bawasiri zisikie tu, maumivu yake sio ya nchi hii!!
Mkuu yaani nakwambia kwamba sasa hivi napitia maumivu makubwa sana. Hivi hizi bawasili hazina tiba ya asili inayoweza kuziondosha moja kwa moja mkuu?
 
0712505049
Screenshot_20220203-204828.jpg
 
Back
Top Bottom