pepim
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 335
- 52
pole sana
ahsante sana mwanaweja
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
pole sana
(Hemorrhoids)
Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri:
i. Nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
ii. Ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
![]()
![]()
Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
• Tatizo sugu la kuharisha
• Kupata kinyesi kigumu
• Ujauzito
• Uzito kupita kiasi (obesity)
• Ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
• Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
• Umri mkubwa
Dalili za bawasiri;
• Damu kuchanganyika na kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
• Maumivu au usumbufu
• Kinyesi kuvuja
• Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
• Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
• Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri:
• Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
• Strangulated hemorrhoids
Vipimo na uchunguzi:
i. Digital rectal examination
ii. Proctoscope
iii. Sigmoidoscope
Matibabu :
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
i. Rubber band ligation- Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
ii. Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
iii. Coagulation (infrared, laser and bipolar)
iv. Upasuaji;
-Hemorrhoidectomy
-Stapled hemorrhoidopexy
Jinsi ya kuzuia Bawasiri:
• High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
• Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
• Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
.......................... gfsonwin ...................................... pepim
Ahsante aisee, vipo kwa nje(pembeni) katika ile mikunjo ya anus.
Habari JF Doctors
Msaada tafadhali, Mdogo wangu wa kiume umri 27 ameota nyama anadai siyo kubwa sana ni ndogo karibia na sehemu ya njia ya haja kubwa, ana lalamika maumivu makali na tumbo lina muuma sana.Je ni ugonjwa gani? na matibabu yake yako ya kienyeji au hospitali. msaada madokta. asante
nini cha ajabu ambacho dokta hana?si useme tu ni wewe??anyway ilo tatizo lipo pabay ajamani...........maan adokta lazima aone kwanza.......mamaaaaaaaaa
heheeeeeeeeee uschezee nyuchinini cha ajabu ambacho dokta hana?
si useme tu ni wewe??anyway ilo tatizo lipo pabay ajamani...........maan adokta lazima aone kwanza.......mamaaaaaaaaa