mjepo
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 4,913
- 919
mkuu niwekee namba ya simu nitakupigia tuongee mzee wangu anatibu kwa dawa za jadi lakini kama hutajali.Habari zenu wanajamvi? Jamani mimi nina tatizo, tatizo langu ni kwamba nina kauvimbe kilichopo kwenye tundu ya haja kubwa kwa ndani. Kauvimbe hako kimekaa upande mmoja kwenye round ila kwa ndani hivyo ukitaka kupagusa lazima utumbukize kidole. Kauvimbe haka kananinyima raha kabisa kwani kameufanya mwili wote uwe unauma, ikiwemo homa za mara kwa mara zikiambatana na baridi kali ambalo huanzia tumboni pamoja vidonda mdomoni, kunichosha mwili na vidonda mdomoni. Nimekwenda kwenye hospital mbalimbali na kupata dawa tofauti tofaut lakini bado sijapata nafuu yoyote. Baadh ya dawa nilizotumia ni anusol ambayo huitumbukiza sehemu hiyo ya haja kubwa. Jamani nimekuwa nakosa raha kabisa kwa tatizo hili hivyo kwa mwenye ufahamu wowote juu ya tatizo si vibaya ukatoa mchango wako hapa huenda ukawa na msaada kwangu ili kuondokana na tatizo hili kwani nadharirika pale ninapokwenda hospital na daktari hutaka kunichungulia ili ajiridhishe!