Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
The Boss, kama tumboni hamna kitu maji yatakaa kweli mkuu!
nini sababu ya kuvimba vinyama sehemu ya haja kubwa?
Weka picha
Jamani naonbeni msaada juu ya huu ugonjwa ningependa kujua unatokana na nini,madhara yake nini na tiba yake.
Mnasumbuwa watu tu, muwe mnasearch kwanza kabla ya kuanzisha thread. Hii kitu tumeijadili kwa kina miaka iliyopita na dawa zipo.
Sijakulazimisha ureply km nakuboa piga kimya co lazima u comment kila thread kaa ukijua sio kila mtu ksjoin humu mwaka juzi.
Huyu Matola ana kiherehere sana, kwa kweli sio mungwana Ana majibu ya watoto sana
Ana stress za kuchapiwa
Sijakulazimisha ureply km nakuboa piga kimya co lazima u comment kila thread kaa ukijua sio kila mtu ksjoin humu mwaka juzi.
BAWASIRI (HEMORRHOIDS)
![]()
Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
- Tatizo sugu la kuharisha
- Kupata kinyesi kigumu
- Ujauzito
- Uzito kupita kiasi (obesity)
- Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
- Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
- Umri mkubwa
Dalili za bawasiri
- Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
- Maumivu au usumbufu
- Kinyesi kuvuja
- Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
- Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
- Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
- Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
- Strangulated hemorrhoids
![]()
Vipimo na uchunguzi
- Digital rectal examination
- Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
- Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
- Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
- Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
- Coagulation (infrared, laser and bipolar)
- Upasuaji.@qn of sheba
Pole sana, Mzizi mkavu amejaribu kufafanua kwa undani tatizo hilo ambalo chanzo kikuu uwa ni tatizo la kukosa choo, linatatulika, bali ukichelewa upelekea tatizo kubwa zaidi la COLON CANCER au kifo.Jamani naonbeni msaada juu ya huu ugonjwa ningependa kujua unatokana na nini,madhara yake nini na tiba yake.