Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

leo siku yatatu namaumivu makali sana sehemu yahaja kubwa kwandani kidogo,naogopa hata kujisaidia ndio balaa hata kukaa nakaa kwashida.kwenda hospitali naona aibu,nimegoogle nimeona anal fissure inalingalingana maelezo yake na ninavyo umwa mimi naomba msaada wenu wamaelezo nadawa!

Pole sana mkuu. Tafuta magadi yachangaye na tangawizi. Sugua polepole halafu weka huo mchanganyo. Inauma sana lakini jikaze. Baada ya siku mbili itakuwa tayari. Pole sana nayajua maumivu yake. Mungu akutangulie upone haraka
 
Haya ndugu fuata ushauri huo wa wataalam hasa mzizi mkavu ninamuamini sana
 
leo siku yatatu namaumivu makali sana sehemu yahaja kubwa kwandani kidogo,naogopa hata kujisaidia ndio balaa hata kukaa nakaa kwashida.kwenda hospitali naona aibu,nimegoogle nimeona anal fissure inalingalingana maelezo yake na ninavyo umwa mimi naomba msaada wenu wamaelezo nadawa!

Pole sana mkuu, hilo ni tatizo ambalo lilinitesa sana na nimetoka hospital juzi baada ya kufanyiwa surgery na specialist, kama upo Dar nenda BURHAN utakutana na Daktari kwa uchunguzi zaid, usiogope mkuu kuwa muwazi upate tiba sahihi.
 
gedo pole sana. Kwanza wai hospitali na usiogope kumuonyesha dr sehemu iliyoathirika.Kama kuna kijipu kimetokeza basi hii ni fistulectomy. Hii ilinipata na mara ya kwanza nilivoenda hosp, walipasua ukatoka usaha umechanganyika na damu. Ndan ya wk 2 tatizo lilirudi kwa kasi. Nililazwa na kufanyiwa operatn. Baada ya miezi 2 tatizo lilirudi kwa kasi. Hapa dr wangu alishauri nisubili specialist. Nikiwa na miezi 6 tangu nipate tatizo, dr alinifanyia op na tatizo liliisha. Huu ni mwaka wa 7. Ukizembea ilo jipu litaama toka upande A kwenda upande B. Ukifanyiwa Op, inaitaji usafi wa hali ya juu na wakti unaenda chooni unaumia. Taadhari: watakuja waganga wengi kila mmoja anataja dawa yake, bila kwenda hosp haitapona.kama huko mwz kuna dr anaitwa filipo??? Nafikiri kama sijakosea jina huyu ndie surgion aliyenitibu.pole na zingatia ushauri
 
asanteni MziziMkavu nawengine wengi mlionisaidia kwahili,nimepata matibabu natumia suppositories,contramoxazole pamoja na skineal cream na ninaendelea vizuri kabisa.mbarikiwe sana.
 
Last edited by a moderator:
Je dawa ni ipi inayoponyesha kabisa maana upasuaji wengi wanaogopaa
 
Nasumbuliwa na bawasiri nilishatumia dawa za hospitali lakin hakukuwa na mabadiliko.nilisoma huku jf dawa ya asili ya ganda la mgomba na kulitwanga then maji yake kupaka kwenye unyeo kutwa mara tatu ikanisaidia coz maumivu yameisha ila shida uvimbe bado upo .naomba mnisaidie ndg zanguuu dawa ya kumaliza huu uvimbe..! I
 
BAWASIRI HEMORRHOIDS

8a2e34f0723702fe81970a9fc0a72c41.jpg

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;

  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri

  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

786813_f260.jpg
Vipimo na uchunguzi

  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy

Njia za kuzuia Bawasiri

  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa
 
Attachments

  • BAWASIRI.jpg
    BAWASIRI.jpg
    9.9 KB · Views: 120
DAWA YA MARADHI YA BAWASIRI ZA AINA ZOTE

Ndugu zangu kichwa hapo juu chaweza kumfanya mtu ajiulize swali, je bawasiri zipo za aina ngapi?

Jawabu ni kuwa bawasiri zipo za aina mbili.

1>> Aina inayotembea (Yaani ikitoka ndani na kurudi)

2>> Aina inayosimama (Yaani kinyama kinachoota kwenye dubuni).

Sasa bawasiri zote hizi tiba yake n hizi zifuatazo Inshallah!!

Kitunguu thaumu (Vijiko vitatu vya chakula)

Asali (Nusu lita)

Tangawizi (Vijiko vitatu vya chakula)

Figili (fijili) - (Vijiko vitatu vya chakula)

Matumizi: Madawa haya lazima yapimwe kwa idadi hiyo yakiwa tayari yamekuwa unga, kisha changanya pamoja, na dozi yake ni kama ifuatayo;

Kijiko kimoja cha unga wa madawa haya utakilamba asubuhi, mchana utafanya kama hivyo tena kisha jioni yaani (1 X 3) kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja (7 - 11).
 
Attachments

  • Hemroids-or-piles.jpg
    Hemroids-or-piles.jpg
    19 KB · Views: 122
  • Hemroidslysis.jpg
    Hemroidslysis.jpg
    20.5 KB · Views: 120
Asante@mzizi mkavu.bt wanadai ukifanyiwa operation kukatwa huo uvimbe kidonda hakiponi na hata kikipona huuma kila ujisaidiapo je kuna ukweli ndn yake...???
 
Dah pole sana mdogo angu anasumbuliwa pia na alimeza dawa ingawa analalamika uvimbe haujapona pia kama wewe na alipoambiwa anaumwa huo ugonjwa alikuja kuniuliza na mm pia nilikuwa siujui nikaja kuuliza humu nashukuru MziziMkavu kwa kuonyesha ushirikiano wake ingawa wengine kama kawaida yao walijishauashaua ni kagoogle pia nakumwelewesha dogo vizuri
 
Last edited by a moderator:
Qn of sheba @je uvimbe uliisha au bado upo? Alitumia dawa gani???

Hivi karibuni kaniambia kuwa uvimbe haujaisha dawa alizomeza sizijui maana alimeza tangu mwaka jana hivi. Na kuhusu operation yawezekana kweli maana housegal wetu pia bro wake alifanyiwa operation ya huo uvimbe maana alikuwa anasumbuliwa sn na tumbo tangu mwaka jana ila hadi leo kweli hajapona.
 
sasa naamini kila bina damu ana tatizo lake ama la nduguye alilo lificha moyoni/mbiyuniiii mwake...
 
DAWA YA MARADHI YA BAWASIRI ZA AINA ZOTE

Ndugu zangu kichwa hapo juu chaweza kumfanya mtu ajiulize swali, je bawasiri zipo za aina ngapi?

Jawabu ni kuwa bawasiri zipo za aina mbili.

1>> Aina inayotembea (Yaani ikitoka ndani na kurudi)

2>> Aina inayosimama (Yaani kinyama kinachoota kwenye dubuni).

Sasa bawasiri zote hizi tiba yake n hizi zifuatazo Inshallah!!

Kitunguu thaumu (Vijiko vitatu vya chakula)

Asali (Nusu lita)

Tangawizi (Vijiko vitatu vya chakula)

Figili (fijili) - (Vijiko vitatu vya chakula)

Matumizi: Madawa haya lazima yapimwe kwa idadi hiyo yakiwa tayari yamekuwa unga, kisha changanya pamoja, na dozi yake ni kama ifuatayo;

Kijiko kimoja cha unga wa madawa haya utakilamba asubuhi, mchana utafanya kama hivyo tena kisha jioni yaani (1 X 3) kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja (7 - 11).

Fijili ndo kitu gani boss, maana huu ugonjwa ulishakuwa ni sehem ya maisha yangu ni mwaka wa tatu sasa nahangaika. Perhaps hii dawa yaweza nisaidia.
 
Hivi karibuni kaniambia kuwa uvimbe haujaisha dawa alizomeza sizijui maana alimeza tangu mwaka jana hivi. Na kuhusu operation yawezekana kweli maana housegal wetu pia bro wake alifanyiwa operation ya huo uvimbe maana alikuwa anasumbuliwa sn na tumbo tangu mwaka jana ila hadi leo kweli hajapona.

Mh.! Mungu atusaidie nasikia kuna dawa ya asili xx sijui ni ipi?op siyo nzuri sana.!
 
Fijili ndo kitu gani boss, maana huu ugonjwa ulishakuwa ni sehem ya maisha yangu ni mwaka wa tatu sasa nahangaika. Perhaps hii dawa yaweza nisaidia.

Kwn bado una pata maumivu????mm yameisha kwa kukamulia maji ya ganda la mgomba bt uvimbe ndiyo bado.!
 
Back
Top Bottom