Uhai wa Taifa Letu unategemea Uwepo wa CCM Madarakani Muda Wote.

Mungu Hutumia watu kwa kuwainua na kuwapatia kibali kama ambavyo ameipatia kibali CCM
Yaani unazidi kupuyanga ,nani aliwapa kibali SISIEMU kuongoza? Uchafuzi wa 2020? ENL(M.A.P) 2015 alimtoa ngeu NZIRANKENDE ,hamjawahi kushinda kwenye BOX la kura ndiyo maana hamtaki kusikia katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi maana ndiyo KIBLA yenu.

Mamlaka huwekwa na Mungu lakini si NINYI wezi wa kura ,nyinyi ni madikteta mnakaa mdarakani kwa nguvu ya MITUTU.
 
Lini ambapo CCM haijashinda uchaguzi? Ingekuwa haishindi ni vipi ingekuwa inaungwa mkono na mamilioni ya watanzania?
 
CCM wanabebwa na kafara wanazotoa kila siku
 
Kwahiyo Mussa unamfananisha na Chama Cha siasa?

Wewe kweli ni Mnyonge 😂😂
 
Omba basi kiwe chama Kimoja,futa vyama vingi!Unaweweseka mkuu.
 
Kama kweli CCM wangekuwa wanamtegemea Mungu usingekuwa unaandika haya mabandiko yako ya kichawa, ungekuwa umetanguliza maslai ya Taifa mbele
 
Angalia CCM imetokea wapi ndugu yangu.unafahamu ya kuwa CCM ndio TANU na Ndio ASP? CCM ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM.huwezi kuvitenganisha.
Una kufuru na kama hujui unaitafutia CCM matatizo kwa muumba wa Mbingu na Nchi.
 
CCM inakabiliwa na changamoto kadhaa kubwa ambazo zinaweza kuathiri uwezo wake wa kuongoza na kuendeleza taifa.
Hapa kuna baadhi ya changamoto hizo:

1. Kukosekana kwa Uaminifu na Uhalali:
- Wakati mwingine, kuna hisia miongoni mwa wananchi kwamba chama hakiwawakilishi ipasavyo. Hii inaweza kupunguza uaminifu na kuathiri uhalali wake.

2. Ushindani Mkali wa Kisiasa:
- Kuongezeka kwa vyama vingine vya kisiasa na ushindani wao umekuwa changamoto, hasa katika uchaguzi. Hii inahitaji CCM kuboresha mikakati yake ili kushinda imani ya wapiga kura.

3. Masuala ya Kiuchumi:
- Uchumi wa Tanzania unakabiliwa na changamoto kama umaskini, ukosefu wa ajira, na mfumuko wa bei. CCM inahitaji mikakati imara ya kiuchumi ili kuboresha hali ya wananchi.

4. Ushughulikiaji wa Malalamiko ya Wananchi:
- Wananchi wanatarajia serikali kuwasikiliza na kutatua matatizo yao. Kukosekana kwa majibu ya haraka na sahihi kunaweza kuleta hisia za kutoridhika.

5. Ukatili wa Kijinsia na Haki za Binadamu:
- Kuna wasiwasi kuhusu haki za binadamu na ukatili, ambayo inaweza kuathiri picha ya CCM na kuleta upinzani.

6. Mabadiliko ya Teknolojia na Habari:
- Teknolojia inabadilika kwa kasi, na vyombo vya habari vya kijamii vinaweza kuathiri mtazamo wa umma kuhusu CCM. Chama kinahitaji kuwa na mikakati ya kuwasiliana na wananchi kupitia njia hizi.

7. Mabadiliko ya Tabianchi:
- Mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri kilimo na vyanzo vya maji ni changamoto inayohitaji CCM kutunga sera zinazofaa ili kukabiliana nayo.

Hitimisho
Changamoto hizi zinahitaji CCM kuchukua hatua za haraka na makini ili kuboresha hali ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii nchini Tanzania. Hii itasaidia kuongeza uhalali na uaminifu wa chama miongoni mwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…