Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Nilishaacha kuomba nafasi ya ifadhili mara mbili kwasababu ya kukosa pasport..naenda kuomba pasport ili nikaombe chuo alafu afisa moja wa uhamiaji ananiambia nilete barua ya chuo mara ujinga ujinga gani.

Nikamuuliza chuo ili niombe wanaitaji niwe na passport yeye anadai ili nipate passport ni lazima niwe na barua ya chuo.
Nikakumbuka tu kazini kwangu ninavyotoa huduma nzuri vile nianze kubishana na mtu. Ipo siku watabadilika na kutambua maana ya kutoa passport kwa raia bila malipo kuliko ukinga wa sasa pesa unatoa na ujinga unakua mwingi.
 
Sasa utaombaje passport kama huna matumizi nayo?

Si unakua na mpango wa safari ndio unatafuta passport!? Au nakosea ndugu zangu😃😃😃😃
Passport ni kitambulisho, kusema si kitambulisho wanakosea. Maana ya kitambulisho ni kwamba Passport inakutambulisha wewe ni nani, Una uraia gani, Ulikozaliwa, tarehe na Mwaka. Inatambulisha hadi wajihi wako. Ndo maana kumbukumbu ubaki katika machine za kielektroniki.
Pili, Passport ni haki ya watanzania wote. Uwezi mpangia mtu kuwa ukitaka kusafiri ndo uombe passport; hii ni kinyume na sheria za nchi na katiba. Katiba inaruhusu mtu ku move mahala popote bila kuvunja sheria.

Swala la kusafiri ni muda wowote. Mfano, mimi nipo Tanzania. Ni na ndugu yangu Peru, anataka baada ya wiki mbili nimtembelee. Hivi ndani ya wiki hizi mbili nitaweza pata Passport kwa hii Tanzania?
Ok, siku hizi vyuo vingi, pamoja na utafutaji wa kazi wanataka unajaza namba ya Passport na hata kutuma soft copy ya Passport. Hii itakuwezesha kupata kazi au kudailiwa chuoni.

Tanzania tunasema mpaka uwe unasafiri ebu tuache urasimu na ukiritimba. Dunia ni ya sayansi na teknolojia sie tunarudi ile miaka ya 80. Mambo yamebadilika sana. Nchi za Ulaya ukifikisha umri stahiki Passport ni haki ya kila Raia. Ndo maana Ulaya kila Raia ana Passport. Kusafiri ni muda wowote ule. Passport ni mali ya serikali lakini dhamana ipo mikononi mwa yule anae imiliki. Kwani unailipia na inaharama zako, sahihi na hata picha. Tusitishane.
Mie nadhani Uhamiaji wanatafuta kurejesha Rushwa kama zamani. Iwe kupata passport ni deal! Fikirieni mara mbili mbili nyie Uhamiaji.
 
Sasa hapa kipi kipya? mbona huu ni utaratibu wa siku zote? kilichoongezeka labda ni hiyo ada ya laki tano,na hiyo imewekwa makusudi ili tukumbuke kutunza pasi zetu, watu wa Ufipa acheni ushabiki wa kitoto,sio kila inachokifanya serikali ni kibaya,hamia Ubelgiji kaka kama unaona ikisu kikafu,kila siku ni kuloloma tu oh serikali imefanya hivi,oh serikali inafanya vile kwa mlengo wa kuleta chuki na taharuki isiyo na maana,nendeni vijijini mkatangaze sera
 
Hapa naambiwa mimi au Paulo Mselle ?
 
Hii si Ulaya kaka,halafu mualiko gani wa wiki mbili?hata ubalozini huwezi kuomba maombi ya viza kwa huo muda unaosema,ukiwa na safari angalau anza process mwezi kabla ya safari,sio sababu Ulaya wanafanya hivyo basi na sisi kama misukule tuwafuate ,mwishowe utasema mbona Ulaya mwanaume anamuoa mwanamume mwenzake au ,Ulaya mbona kuvaa bikini au vichupi ni kitu cha kawaida basi na sisi tuvae vichupi hadharani
 
Nilishaacha kufuata habari za uhamiaji tanzania, nikitaka natumia shortcut mchezo umeisha. Hao uhamiaji ni taasisi naichukia kuliko zote tanzania, wanaendesha kizamani sana. One day hao wazee wataondok kitakuja kizazi kingine hapo uhamiaji na milango itafunguka.
Uhamiaji wanaongeza umasikini tanzania kwa kuwanyima raia wake passport. Yaani kama unataka kwenda kufundisha kiswahili afrika kusini unaanza kuhangaika nao tena badala ya wao kuweka mazingira mazuri kwa kila mtanzania.
Short kati gani
 
Hii si Ulaya kaka,halafu mualiko gani wa wiki mbili?hata ubalozini huwezi kuomba maombi ya viza kwa huo muda unaosema,ukiwa na safari angalau anza process mwezi kabla ya safari,sio sababu Ulaya wanafanya hivyo basi na sisi kama misukule tuwafuate ,mwishowe utasema mbona Ulaya mwanaume anamuoa mwanamume mwenzake au ,Ulaya mbona kuvaa bikini au vichupi ni kitu cha kawaida basi na sisi tuvae vichupi hadharani
Hujanaielewa. Umekimbilia kukosoa na hata kuleta mifano ambayo haiendani na nilichokisema. Hapa tunaongelea Passport hayo yakuoa yametoka wapi. Nimetoa mifano yote kwa Passport. Si kila nchi inausumbufu wa Visa. Na ujue kuna nchi ambazo watanzania tunaingia bila visa na nyingine visa on arrival. Mfano nchi nyingi za America ya kusini Carrebian na nchi za Asia ya mbali tunapata visa on arrival. Tanzania tunaingia nchi yapata si chini ya 72 duniani tunaingia kwa visa on arrival. hatuhitaji kutuma maombi ya visa wewe huko Tayari kusafiri unaondoka.
Hakuna usumbufu wowote. Nakupa mfano, mie mwenyewe nimefanikiwa kusafiri nchi mbalimbali kwa mtindo huo. So ondoa mawazo yakuwa nchi zote lazima kuomba Visa kabla ya mwezi.
Swala la Passport ni swala la kimataifa, ndo maana nikaongelea kuwa tunahitaji kuendana na dunia hasa katika suala la passport. Unajua ni kwanini vyuo vingi au uombaji kazi katika nchi mbalimbali wanahitaji namba za Passport au nakala. Wanajua Passport ni haki ya mwananchi. So usitake badili hoja, na kukumbilia maswala ya kuoana kijinsia sijaongelea hilo na mfano wako huko nje ya topic.
Pia fahamu kuwa kuna nchi si chini ya 72 duniani Tanzania tunaruhusiwa kusafiri bila kuomba visa. Hivyo nikijisikia au nikipata mwaliko muda wowote ule nakwenda.
Unaposema si kama Ulaya unajua Tanzania na Africa ya Mashariki tulibadili Passport ziwe kwenye mfumo wa kielektroniki ili kukidhi matakwa ya kimataifa kama zilivyo passport zingine kwenye mataifa yaliyoendelea.
 
Nimekuelewa vizuri kiongozi
Kwahiyo muda wote ulikuwa umeshupaza shingo unabisha usichokielewa vizuri? Hili jambo la raia ana haki ya kupata passport bila hata kuwa na safari mbona tumeshalijadili humu miaka nenda miaka rudi, policy makers wapunguze ushamba na watafute exposure.

Hata hivyo hakuna kinachoshindikana uwe na sababu ya kusafiri au usiwe nayo ukitaka pass unapata tu, kinachoongezeka ni kuwa wanatengeneza mazingira ya rushwa, wakati ofisi zao zote wamebandika matangazo ya "USITOE RUSHWA HAPA, Serikali iliyojaa wanafiki, wanahubiri "maji"huku wao wanakunywa "maziwa".
 
Tanzania bhana viongozi mnabania maendeleo kwa Wananchi wenu bila kujua imefikia vijana wakipata passport wanafurahi kama vile wamepata kitu gani sijui mtu ni raia na swala passport ni haki yake kuea nayo ila mnaona kuwa na passport ni haki kwenu na watoto wenu wachanga Ila sio Watanzania ambao ni watu wazima wanaotaka kutafuta maisha nje mbaya sana kwa kweli na hamjui passport inaleta fedha za kigeni hilo ninyi hamjui ni roho mbaya tuu wabongo...
 
Ukiashafanya application ukipewa form inataka uandike namba ya passport unachukua hizo application form unaenda uhamiaji kuomba passport ili upate namba yako ujaze.
Sasa pale ambapo unakuta unatumia online portal mwanzoni tu hata kabla ya kuimaliza fomu kuijaza, unawekewa pa kujaza namba na huwezi songa mbele hadi ujaze sehemu hiyo ya kwanza ndio uende next.
 
Ukiashafanya application ukipewa form inataka uandike namba ya passport unachukua hizo application form unaenda uhamiaji kuomba passport ili upate namba yako ujaze.
Online fomu sio zote zina option ya ku print zina ya ku submit tu

Ni usumbuffu usio na sababu pia huwezi print nyingi zina option tu ya submit tu ukifika mwisho na kipengele husika ukifika usipojaza hupelekwi next

Usumbufu wote huo wa nini kitu cha kujaza online dakika kumi eti usubiri ukifika sehemu ya kujaza passport namba uende uhamiaji ukaombe passport usubiri siku 14 au wiki ndio urudi online kuendelea kujaza fomu .Kweli kazi ipo!!!!!
 
Hii si Ulaya kaka,halafu mualiko gani wa wiki mbili?hata ubalozini huwezi kuomba maombi ya viza kwa huo muda unaosema,ukiwa na safari angalau anza process mwezi kabla ya safari,sio sababu Ulaya wanafanya hivyo basi na sisi kama misukule tuwafuate ,mwishowe utasema mbona Ulaya mwanaume anamuoa mwanamume mwenzake au ,Ulaya mbona kuvaa bikini au vichupi ni kitu cha kawaida basi na sisi tuvae vichupi hadharani
Umejichanganya sana ! kila jambo ni lazima lihojiwe sababu yake nini , kwa mfano tukikufichulia kwamba mpango huu wa Uhamiaji umelenga kudhibiti wale wenye mipango ya kuondoka nchini baada ya kutishiwa maisha utabisha ?
 
Back
Top Bottom