Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Mshauri wa Masuala ya Mazingira katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)Ester Ibrahim Shemdoe, amesema mradi huo umeweka kipaumbele katika ulinzi na uhifadhi wa mazingira kwa kuzingatia sheria na viwango vya kitaifa na kimataifa vya mazingira.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi huo, amesema kwa kushirikiana na mkandarasi CCP, wamefanya tathmini mbalimbali za kimazingira zikiwemo za viumbe hai, udongo, mimea na wanyamapori ili kubaini athari zinazoweza kujitokeza na kuweka hatua za kuzidhibiti wakati wa shughuli za ujenzi.
Ameeleza kuwa katika hatua ya uchimbaji kwa ajili ya ulazaji wa bomba, tabaka la juu la udongo hutolewa na kuhifadhiwa kwa kufuata mapendekezo ya wataalamu, kisha hurejeshwa baada ya kazi kukamilika ili kuwezesha uoto wa asili kuendelea kustawi.
Kwa upande wa viumbe hatarishi, amesema mradi unatumia wataalamu maalumu wa wanyamapori wanaowakamata viumbe kama nyoka na kuwahamishia katika maeneo salama bila kuwaua ili kulinda bioanuwai wakati shughuli za ujenzi zikiendelea.