Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Asemwe usiku na mchana hatutaki matusi na ubaguzi wala uchokozi.

Wewe upo nje ya Tanzania halafu ni sukuma gang, tunakufahamu. Ndiyo nyinyi mnaochochea ujinga.
 
Kila mtu ana jambo lake ki maslahi, likiguswa atalalamika...
Jambo la DP World lina maslahi pande tofauti. Kila upande usikilizwe.
Hakuna kuona hawa ni hawa, wale ni wale...
Mkuu hivi umeisoma thd na kuielewa?

Mleta mada hajakataza watu wasitumie uhuru wao wa maoni bali ametaka wakati wa kutoa maoni,watu wasitumie lugha za kuudhi kama vile matusi,kejeli au kashfa ya udini coz hali hiyo inaweza kuleta madhara makubwa sana huko mbeleni.
 
Nani katukana?

Na kejeli kwa viongozi si jinai!

Maneno ya dharau si jinai.

Acheni watu waongee.

Kuwaziba watu midomo ni dalili ya kushindwa hoja.

Na unaposhindwa hoja basi unaanza kutumia maguvu tu.
Hiyo USA na Canada, siyo Tanzania.
 
Ona hii punguani,mleta mada ni wapi amekataza watu wasitoe maoni yao? Hivi umeisoma thd au umekurupuka tu kama chafya?
 
Mi nataka kumuwowa huyo Faizafoxy na tuone atakayepinga
 
Nimemuelewa. Hayo ya lugha ya maudhi yanatokana na kutokueleweka kwa wasemaji..Viongozo wakiwa na lugha moja wataeleweka. Huyu akisema hili na yule lile wananchi wanaona kuna uongo mahali "Watabweka"..
Jambo moja la bandari, bandari wanasema lao, waziri lake,Spika lake, waandishi lao, walioenda Dubai lao, Heeee..!!!!
Kwanini "mbwa asibweke" ...
 
Basi sawa,acha hao uliowaita mbwa waendelee kubweka.
 
Sawa kabisa, kila mmoja wetu ana maoni yake, na ni vizuri kwenye maoni tusijumuishe, uweke huyo mwana siasa na alichokifanya ambacho wewe hukioni sawa, ndiyo nguvu ya hoja.

lakini kutukana na kuchochea kwa lugha za maudhi kunajenga au kunabomoa?
Hizo lugha zenye staha ni muhimu sana kwenye kuvuna shamba la bibi. Business as usual
 
Hata hawa jf wenyewe ni wabaguzi na wachochezi, mie nyuzi zangu nyingi tu wamezifuta na wala hazina athari kihivyooooo, ila za wagalatia bwashee, pamoja na kua ni za hatari na za kuuwana bado wameendelea kuziacha na kuzisambaza
Nahisi kitu hapo sio bure
 
Kuna kuchokozwa kwa mwananchi zaidi ya kuambiwa uende Burundi na Wanaokutumikia ?

Mipaka ipo wapi ya Maoni - Ukiachia vitu subjectlve ndio viwe viashiria vya kuzibana midomo mwisho wa siku vinatumika kuziba watu midomo..

Kama watu wanavuka uhuru wa kuongoza kwa kukanyaga makubaliano na kubadilisha chochote inapokuwa convenient kwao sio wao watakaoleta maafa bali ni hao wanaondesha hii nchi kwa matakwa yao binafsi......

Naona kuna rungu la kuziba watu midomo lililotumika kuwaziba kina Ndugai (walivyosema tukiamka tutakuta tumeuzwa) au yule mfanyakazi wa TRC aliyelalamika kuhusu Tozo linataka kuendelea / kuanza kutumika

Tuambie ukweli tu, things are falling apart.... Na ukichekelea unapoambiwa unaupiga mwingi vumilia au jibu ni kwanini unalikoroga unapoambiwa unaharibu... (Heri muonesha Kero kuliko mnafiki anayekupaka mafuta kwa mgongo wa Chupa)
 
Kwa sasa asilimia kubwa wananchi ni wenye hasira kali, kwa sababu wakubwa hawawasikilizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…